TAKUKURU tunaomba Msaada: Kijana huyu alipata ajira Serikalini lakini akaporwa kituo cha kazi na kupewa mwingine

Status
Not open for further replies.
Si utumishi wenyewe wamejibu kuwa ni mistake. Sasa mtoa mada analazimisha tuone kuwa rushwa imehusika.
Rushwa haijahusika hapa, wala undugu haujahusika
Hamna kitu kama hicho ndugu, au unamtetea ndugu yako, mistake imetoka wapi kwenye mambo muhimu kama haya, utatoaje jina bila kufanya verification ya kutosha , huu ni uhuni wengi tumehujumiwa kwa namna moja au nyingine, au una undugu na Jamaa aliyenunua nafasi ya mdau
 
Daaah, pole sana. Huyo Salum Makui ni wa Dini hiyo ya upande wa pili, kwahiyo tegemea lolote, maana wanasema na wao ni zamu yao kutesa, haijalishi kafeli usahili au nini, kikubwa ni kuitwa SALUM
Huu ujinga wa ukabila na udini umekufa kipindi Cha hayati
 
Dogo utumishi wa umma hautaki kiburi cha namna yako, naamini umeshaajiriwa na utapangiwa kituo kipya baada ya mkanganyiko uliotokea kumalizwa. Kwa aina yako ya kubwabwaja ovyo hakuna mwajiri yeyote atakeyependa kukuajiri, sio Serikalini tu hata huko private.
Acha kumtisha mtu, huu ni ujinga mtupu
 
Hana haki kwa kusema haki mkuu. Kwani ana mkataba tayari wa kuajiriwa kwamba alishaajiriwa??

Hata muajiri akisema sasa haajiri tena ameahirisha hakuna kitu anaweza akafanya hapo. Saa nyingine ni kuwa mpole na kuacha process ifanyike.

Kama nilivyosema hapo juu ninahisi kuna makosa yamefanyika seems ndomaana hii ishu inakua ngumu kushughulikiwa kwasababu kuyarekebisha kwake ni mpaka nafasi ipatikane na achomekwe yeye. Analoweza kufanya ni kukomaa nao kuendelea kuwakumbusha tu mara kwa mara. ILa sio kwa makelele namna hii mpaka hapa bado yuko kwenye hatua ya MAOMBI YA KAZI. Si muajiriwa na Maombi yanaweza kukubaliwa/kukubaliwa

Ameshafika hatua nzuri na nina uhakika ishu yake inashughulikiwa

Na kitu kingine sikuona haja ya kumuhusisha hadi mtu aliyeajiriwa nafasi yake kwa kumuweka jina hapa na taarifa zake. Uozo /Makosa yamefanyika utumishi imawezekana na mwenzake ni muhanga anamlaumu bure
Dust tupu , nyie ndo wapiga Dili kazi kutosha watu na kuvuta subira , uyo aliyefika hapo katoka wapi ,
 
Mkuu Liability pole kwa yote uliyopitia. Naomba usinipige mawe kwa nitayoandika hapa. Jambo lililokumba linaweza kabisa likawa ni kosa la kibinadamu tu na sio RUSHWA kama unavyodhani. Ukiangalia katika issue yako hakuna shaka yeyote katika hatua zote za awali (Usaili, kutangaza matokeo na uteuzi) unayoweza kuuelekeza TUME ya ajira. Ukiangalia kwa umakini utaona kwamba kilichotokea hapo ni kukosekana kwa mawasiliano mazuri kati ya maafisa wachache wa Tume ya Ajira na sio nia Ovu kama unavyodhani.

kilichotokea hapo ni kwamba Afisa mmoja anaita Interview ya nafasi fulani na Afisa mwingine anaangalia katika Database ya TUME na kumteua mwajiriwa wa nafasi ambayo watu wameitwa kwa interview. Unaweza usiniamini nilichoandika hapa lakini kama ukienda katika baadhi ya Taasisi za Serikali ukiwa kama raia wa kawaida jambo kama lako sio la ajabu.

Katika kujisomea kwangu kama mwananchi wa kawaida na ninapotembea banda la Utumishi katika maonyesho mbalimbali kuna kitu wanakiita maadili ya Watumishi/Utumishi wa Umma ambayo yamenifanya nipende kubakia tu Sekta binafsi na sio kukimbilia huko kwao. Kwa ulivyoandika hapo juu nachelea kusema kwamba huna maadili ya kuwa Mtumishi wa Umma. Nakushauri tu uungane na sisi katika Sekta binafsi.

Samahani kama nimetumia Lugha kali sana LAKINI hayo ndiyo mawazo yangu.

Ahsante
Hata wao hawana maadili ndio maana yake
 
Umeongea point hasa hapo kwenye MAADILI.

Nadhan hata wewe utaona kuna wakati mainjinia wanadhalilishwa na viongozi wa kisiasa hasa mawaziri lakini utaona wanakaa kimyaaaaa.

Na wengine mpaka wanatumbuliwa kabisa lakini baada ya siku kadhaa unawaona kazini tena!!

Hii issue ya maadili hii...

Na hapo wenda waka m-ref flag ma asishangae hata akipata nafasi hatakaa apewe nafasi za uteuzi kama ukuu wa idara etc..

Ila wenda mleta mada anaweza akapewa benefit of daught maana inawezekana bado hajaingia kwenye utumishi kwa hiyo bado haya mambo hayajui!!

Kama ikiwezekana afanye ufwatiliaji kimya kimya na ikiwezekana arudi tena utumishi uonane na mkuu wa utumishi umueleze kisa chake pia then atulie aache process ifwate!!

Pia ana option ya kudai kwa nguvu kama anavyo fanya lakin risk yake ndio hiyo, MAADILI!!
Acheni kutisha watu hapa , watu kibao wamefungua kesi za kifukuzwa kazi, kwamba wanakosa maadili, watumishi wengi mnafanya madudu hafu kazi yenu kutisha watu.
Pambania haki yako asikutishe mtu, hafu uje kuleta mrejesho hapa.
 
Moderator rekebisheni ama uzi usimamishe maana kwenye majina ya leo mleta mada kapangiwa kituo cha kazi.

Kila la kheri kwake na akapige kazi.

Hongera kwako Liability utumishi wamesikia kilio chako.

CE8D06A9-5AF9-4581-900A-E0B8E5117902.jpeg
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom