DOKEZO Uchunguzi ufanyike Kituo cha Polisi Ilula Iringa. Kuna viashiria vya RUSHWA kukithiri na kusababisha ucheleweshwaji wa huduma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Nilipokea taarifa ya kifo cha baba baada ya kupata ajali ya pikipiki Februari 2024.

Nililazimika kuahirisha mitihani ya chuo iliyokuwa imeanza siku mbili kabla ya kupata taarifa ya kifo cha baba.

Nikarejea nyumbani kwaajili ya mazishi ya baba na taratibu zingine ikiwemo ufatiliaji wa hati ya kifo na kufatilia pikipiki iliyokuwepo Kituo cha Polisi tangu siku ya ajali.

Baada ya mazishi
Nikiwa na matarajio ya kuwahi kufatilia mapema na kurejea Moshi Kilimanjaro kwaajili ya Masomo.

Nilifika kituo cha Polisi nikapewa maelekezo namna ya kuweza kuipata ili angalau iweze kutusaidia katika shughuli mbalimbali za kiuchumi kwa kuendesha maisha ya familia.

Siku ya pili nilifika kituo cha Polisi mapema huku nikiwa na uhakika wa kumaliza mapema na kuondoka cha ajabu nikakabidhiwa viambatanishi nilivyokuwa nimeagizwa na nikaambiwa nisubiri mkaguzi kutoka wilayani aje afanye ukaguzi wa chombo kilichoharibika (pikipiki) kwahiyo nikaambiwa "njoo kesho itakuwa tayari".

Siku ya tatu nikafika mapema huku nikiwa na uhakika tena wa kufanikiwa na kuondoka mapema, nikafika mapema na kuambiwa hakufanikiwa kufika na kibaya zaidi kila nikifika ni Afisa Polisi mmoja tu naambiwa niongee naye.

Ghafla nikiwa na Afisa Polisi mwingine tofauti na ninayekutana naye siku zote akiwa ananipa maelezo mengine, yule wa siku zote Kila nikifika ndiyo anaingia akasema "Afande achana naye huyo, mwambie aje kwangu utatumia muda mrefu" huku akionesha viashiria vya kutaka RUSHWA ili niweze kuchukua muda huohuo nikitaka.

Kwasababu bado ni mwanafunzi lakini pia nimefanikiwa kufanya kazi na taasisi nyeti za tafiti na uchunguzi bila Afisa Polisi kujua anayezungumzana naye ni nani , niliongea naye kwa ujasiri mkubwa sana na kurudisha jibu la mwisho kwamba mkaguzi hakuja Tena.

Akasema kesho njoo itakuwa tayari na hapo ni siku ya nne imefika licha ya kuwa nipo kipindi kigumu cha uangalizi wa familia kama mtoto wa kwanza na maendeleo ya wadogo zangu waende shule, lakini bado nazungushwa.

Siku iliyofuata nikafika kama ilivyo kawaida mapema lakini bado nikapewa majibu yaleyale.

Nikachukua uamuzi wa kuitafuta njia mbadala ya mimi kuweza kuipata pikipiki mapema.

Kwa bahati nzuri niliwahi fanya kazi na Afisa Polisi mmoja katika mission ya uchunguzi nikiwa kama ICT Operator nikiwa Diploma mwaka wa pili 2022/2023.

Nilimtafuta na nikamueleza hali halisi akanielewa na kwasababu amekuwa na nafasi kubwa ya uongozi, moja kwa moja alimtafuta Mkuu wa Kituo cha Polisi Ilula na kuwasiliana naye kwa kumpa angalizo la ufanyaji kazi kwa weledi kwa kuzingatia haki za watu.

Nilifika kituoni hapo na kweli nilikuta pamoto maana kila afisa polisi anaondoka mapema baada ya kujulikana kwa tukio kama Hilo

Japo ilikuwa jioni kabisa nikiwa nimekaa nje kituoni hapo sikubanduka mpaka nihakikishe nimeitwa kwaajili ya makabidhiano.

Muda ukifika nikaitwa na afisa polisi mmoja akaniuliza "wewe ndiyo inahitaji pikipiki?" Nikamjibu yes ni Mimi na kunipeleka moja kwa moja kwa mkuu wa kituo Cha polisi naa kuhojiwaa baadhi ya maswali na hatimaye nikafanikiwa kutoka na pikipiki muda wa saa kumi na moja jioni.

Ombi langu kwa TAKUKURU , ufanyike uchunguzi wa Kina kwa kuokoa haki za watu zinazodhurumiwa na afisa polisi katika kituo Cha polisi Cha Ilula .
 
Back
Top Bottom