TAKUKURU tunaomba Msaada: Kijana huyu alipata ajira Serikalini lakini akaporwa kituo cha kazi na kupewa mwingine

Status
Not open for further replies.

Liability

Member
Oct 20, 2019
75
100
UPDATE: MLALAMIKAJI AITWA KAZINI

-----
NAMNA KITUO CHA KAZI KILIVYOPORWA
Donald Mshani aliomba kazi serikalini mwezi February 2021 baada ya tangazo la nafasi ya MUHIFADHI WANYAMA PORI DARAJA LA 3 katika halmashauri ya wilaya ya Njombe. Alipata bahati ya kuiitwa kwenye usahili uliofanyika kuanzia tarehe10-14 April 2022 katika ofisi za Sekretariati ya ajira Dodoma (UDOM). Alihudhulia na kufanya usahili katika hatua zote kulingana na maelekezo ya wasahili.

Nafasi ya kuajiriwa ilikuwa ni moja tuu kwa halimashauri ya Njombe. 17/05/2021 Sekretariet ya ajira ilimtangaza DONALD Mshani kama mshindi wa nafasi ya Mhifadhi wanyamapori daraja LA tatu kituo Njombe. Tangazo hili la ushindi wa Donald Mshani lilitolewa kwenye mtandao wa ajira portal siku na tarehe tajwa hapo juu. Maelezo mengine kutoka kwenye mtandao huo ni kumtaka mshindi kuchukuwa barua sekretariet ya ajira ili akapangiwe majukumu ya kazi kwenye kituo chake cha kazi. Alianza safari 19/05/2021 na kufika Sekretariet ya ajira 20/05/2021. Alipewa barua na kuondoka ili akaripoti Njombe.

Aliondoka Dodoma ijumaa ya tarehe 21/05/2021 na kufika siku hiyohiyo lakn usiku hivyo hakuweza kuripoti kwa mkurugenzi. Alisubiri mpaka siku Jumatatu yaani tarehe 24/05/2021. Alipofika siku hiyo hakumkuta mkrugenzi na kulazika kuongea na wasaidizi wake.Waliguna baada ya kutoka maelezo na kuwapa barua yake ya ajira. Baada ya nusu SAA wakamuomba arejee tena ofisini. Alipofika wakamwambia mbona nafasi hii kuna MTU yupo kwenye mchakato wa kuajiriwa tangu mwezi April 2021.

Baada ya kuhoji uhali wa MTU huyo kwa muda mrefu sana akaambiwa amsubiri mkrugenzi. Kesho yake yaani tarehe 25/05/2021 alipata fursa ya kuonana Kaimu Mkurugenzi nakupewa maelezo kwamba nafasi ilishajazwa na MTU mwingne tangu 19/04/2021 na anaitwa SALUMU HAMISI MAKUI.

Aliandikiwa barua kurudi Dodoma Sekretariet ya ajira. Tarehe 26/05/2021 alifika ofisini kwa katibu Sekretariet ya ajira na kuambiwa ndani ya siku 3 atapangiwa kituo kingine cha kazi. Hakupangiwa kituo baada ya hizo siku 3 . Waliomba asubiri siku tatu zingne, alisubiri lakini hakupangiwa. Waliomba asubiri siku 7 alisubiri lakini hakupangiwa na akaambiwa arudi nyumban awe anatembelea sana mitandao anaweza kuona jina lake siku moja.

Kaka yake hakuridhika na majibu hivyo walirudi tena kwa Katibu Mkuu Sekretariet ya ajira na kumhoji maswali yafuatayo .

1) Kwanin umeajiri MTU ambae hakuitwa wala kufanya usahili? Jibu lake ni kwamba alikuwa kwenye database .

2) Kwanini umuitishe usahili kama mmeshapata MTU? Jibu kuna makosa yalifanyika hivyo ni ngumu kurekebisha.

3) Donald asubiri mpaka lini? Aendelee kumuomba Mungu IPO siku atapa.

4) Kwanini aajirwe aliyefeli usahili miaka ya nyuma? Jibu Usahili wao ulikuwa mgumu sana kuliko waliofanya akina Donald.

Tulilazimika kufika ofisi kuu za TAKUKURU Makao Makuu Dodoma karibu na uwanja wa Jamhuri siku ya Jumaa NNE 15/06/2021. Alitoa maelezo yote tangu mwanzo wa mgogoro huu. Lengo kuu la kwenda TAKUKURU ni kuchunguza kama hakuna viashilia vya rushwa na matumizi mabaya ya madaraka kwenye sakata hili.

Tangu siku hiyo hatujapata maelezo wala tumaini lolote kutoka kwao TAKUKURU. Baada ya ukimya huo alitafutwa Waziri wa Utumishi wa umma na utawala bora! Baada ya kupewa maelezo haya alitoa ushirikiano kwa kutushauri kuongea na Katibu Mkuu wake. Alitupa namba ya simu ya mkononi ya Katibu.

Baada ya kuwasiliana na katibu mkuu ,aliomba tutume vielelezo vyote pamoja malalamiko yangu. Tangu 28/06/ 2021 hajajibu wala kutueleza chochote kinachoendelea na hapokei simu. Tarehe 6/07/2021 nimewasiliana tena na Waziri MCHENGERWA akanisihi niwasiliane na Naibu Waziri wake. Naibu Waziri amarudia majibu yaleyale niliyokataa kwa kukuwa naye anataka nivute subira kwa muda usiojulikana.

Nimemjulisha tena Waziri MCHENGERWA kwamba sijaridhika kabisa na majibu ya watendaji wake lakni bado mpaka sasa hajasema chochote.

Sisi tumebaini mambo yafuatayo ambayo hatujapewa majibu
1) Aliyeajirwa kwenye nafasi yangu hakufanya usahili .

2) Ameajiliwa MTU aliyefeli usahili nimeachwa niliye fauli usahili.

3) Aliyeajiliwa hana sifa zilozo kuwa zimeainishwa wakati wa kuomba kazi.

4) SALUMU HAMISI MAKUI alifeli usahili wa TANAPA uliofanyika tarehe 11-24 April 2020 na namba yake ya usahili ilikuwa namba 1697.

5) Ni wazi wamedhamiria kunipora kituo cha kazi ndio maana wamemwajiri MTU ambaye hakukidhi vigezo.

Tangu 25/05/2021 nipo Dodoma nahangaika namna ya kupata haki yangu. Familia imepoteza rasimali fedha nyingi sana tangu kuibuka kwa sakata hili ambalo Mimi naamini ni UTAPELI NA UPORAJI wa kituo cha kazi.

UPDATES!
06/7/2021 nilimtafta waziri Mchengerwa na kumwambia sijaridhika wala kukubali majibu ya watumishi wake kwa kuwa wameshindwa kutatua mgogoro huu. Baada ya nusu SAA nilipigiwa simu na MTU aliyejitambulisha kama mtumishi kutoka wizara ya utumishi wa umma na utawala bora ili nimpe maelezo kuhusu shida yangu ya kuporwa kituo cha kazi.

Nilimtumia nyaraka zote tarehe 08/7/2021. Nilimpigia simu tarehe 09/7/2021 ilivkujua kinachoendelea baada ya kupokea nyaraka zangu na maelezo. Majibu yake ni kuwa kama nafasi ya kazi ikiwa ni dhalura huwa haitangazwi hivyo Mimi natakiwa kuajiriwa kwa kuwa nafasi ya kazi ilitangazwa na watu waliomba.

Utaratibu uliotumika kumwajiri bwana SALUMU MAKUI haukufuata utaratibu. Akaahidi kuwasiliana na watu wa Sekretarieti ya ajira ili kupata ufumbuzi. Tarehe 12/7/2021 nilimpigia simu ili nijue kama amepata ufumbuzi. Majibu yake ni kwamba nimeombewa kituo kipya cha kazi.

Majibu Haya nilikataa kwasababu hayana tofauti na ya awali, kwa kuwa haya yameboreshwa tuu ili nisiendelee kudai haki yangu. Nikamwambia majibu haya mpe Waziri ili nimwambie sijaridhika na majibu yako. Leo ni siku ya 8 nampigia Waziri Mchengerwa simu haipatkani japo SMS nikituma zinapokelewa lakini hajibu na whasspp iko ON lakini SMS hazisomwi.

Mchengerwa alitoa ushirikiano mzuri lakni amepata wapi kigugumizi cha kutatua mgogoro huu!?

Nilijaribu pia kuwasiliana na vyombo vya habari 2 tena vikubwa kabisa kupitia wawakilishi wao . Niliwatumia nyaraka zangu zote na walizisoma lakini hakuna aliyejaribu kuripoti taarifa hii pengeni kulingana ni uoga.

Nimekaa Dodoma siku 65 nikiwa napambana kudai haki yangu.Leo ndio nimeaanza safari ya kurudi kijijini kwetu nikiwa nimeongeza umasikini kwenye familia maskini.

IMG-20210721-WA0008.jpg


IMG-20210721-WA0007.jpg


IMG-20210721-WA0006.jpg


=====

UPDATES;

=====

Malalamiko yake Wahusikia wameyafanyia kazi. Asante.

Moderator rekebisheni ama uzi usimamishe maana kwenye majina ya leo mleta mada kapangiwa kituo cha kazi.

Kila la kheri kwake na akapige kazi.

Hongera kwako Liability utumishi wamesikia kilio chako.

View attachment 1864815
2854295_CE8D06A9-5AF9-4581-900A-E0B8E5117902.jpeg
 
Kwa jinsi nnavyoelewa urasimu was serikalini ulivyo hapo kesi ni ngumu kidogo

Na option iliyopo ni hiyo tu5ya kusubiri nafasi za dharura ili wakuweke hapo. Manaake sioni Kwa namna yoyote ile jamaa aliyepo kazini kutolewa upewe we we

Sijui ni nini haswa kilitokea mpaka wakajichanganya ila solution ndio hiyo moja tu

USHAURI: Komaa nao hivyo hivyo wasikusahau.Ukilegea tu itatokea nafasi nyingine watakuruka
 
Usikate tamaa, Nafasi ni yako au wakupeleke sehemu nyingine. Ila mchengerwa na yeye kazingua Ina maana yeye kama waziri kashindwa ku solve Hilo tatizo inaonyesha kukosa seriousness Hadi walio chini yake hawamweshimu.
Usikute dogo kapelekwa na kigogo hivyo kaona maji marefu usipime na kidole,

Nikikumbuka interview moja watu waliandika majina na kusaini kwamba walikuwepo lakini kesho yake jina la flani halipo kwamba hajahudhuria , ilipigwa simu moja matata ikabidi warejeshe jina
Daah
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom