DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

CWR2016

JF-Expert Member
Dec 14, 2017
2,760
6,294
Ni usiku mnene. Naamua kuandika DOKEZO hili.

Kwa uchungu wa yanayoendelea katika nchi yangu.

Katika mada hii, nitaomba wachangiaji kujadili kwa uwazi kabisa, na kuongezea mifano mingine baada ya hii nitakayokuwa nimeiweka hapa.

Lengo ni Nia njema kabisa kurekebisha pale tulipokosea na kusaidia WaTz ambao wanakosa kufaidi matunda ya nchi yao.

Hapa chini ni jinsi ambavyo mambo ya ovyo yanafanywa wazi na TISS wala TAKUKURU hawafanyi kazi yao iliyotukuka.

1. NIDA na Utoaji wa NAMBA/Vitambulisho vya Taifa.

Hili jambo ni kubwa sana. Mimi nimelithibitisha. Na wote wanaofika kuhudumiwa katika ofisi zote za NIDA nchi nzima wanasema wazi.

Iko hivi, huwezi kufanikisha kupata namba ya NIDA ikiwa huna kiasi fulani cha fedha. Na huwezi kupata ile ID ikiwa huna kiasi kikubwa zaidi cha fedha.

Yani utaenda utafuata taratibu zote na kuwa na viambatanisho vyote, lakini huwezi kupata kimojawapo kati ya hivyo bila fedha. Kiufupi hadi mlinzi wa getini anajua hilo.

Baadhi ya Ofisi za NIDA DSM kupata namba ya NIDA inaanzia sh. 150,000/-. Kupata ID ni kuanzia sh. 500,000/-
Lakini kadri utakavyoongeza dau maana yake utawahishiwa zaidi mchakato wako.

Kwanza hakuna huduma pale, zaidi ukifika upangwe foleni na walinzi, ukiingia unakuta mtu anachat tu, hadi jioni uambiwe njoo tena kesho.

Haya yana muda mrefu yanafanywa wazi kabisa. Hatari hii ni kwamba sasa hata mgeni je, akiwa na milion zake mbili si anapewa zake ID kama MTz??

Mh. Rais wetu ni msikivu, je, ulishasikia amepewa ripoti hii akashindwa kuifanyia kazi?!

Nani wa kumpelekea ripoti kama sio TISS?


2. Mradi wa mwendokasi Mbagala

Huu mradi nendeni mchunguze, ni mbovu na umejengwa chini ya viwango vibaya mno.

Uchunguzi unaonesha baadhi ya miundombinu kuanza kuharibika hata kabla ya matumizi rasmi kuanza.
Wasichokijua ni kwamba hii miradi ya miundombinu ya barabara huwa na zaidi ya miaka 20 ya uhai kabla ya marekebisho.

Sasa ukifika pale ukakuta baadhi ya beacon zimeanguka, kumeguka, n.k, Unajiuliza shida ni nini? Bajeti ndogo ya ujenzi? Lakini hilo linakataa kwa sababu hizi fedha ni mkopo tumepata kutoka Benki ya Dunia (WB), hawawezi kutenga fedha chini ya inayotakiwa.!

Sasa vile vituo vya abiria ndio utacheka kabisa. Mabati ni chini ya viwango, hizo frame walizichomelea ni chini ya viwango, uchomeleaji wenyewe ni wa dizaini za fundi maiko.

Hata wakibisha, nawahakikishieni, barabara ya mwendokasi ya Posta KIMARA itadumu, na hii ya Mbagala itakuja kuharibika mapema kabla yake. Tuko hapa mtakuja kuthibitisha panapo uhai.

Sasa kwa hali hii, utasema Rais wetu alivyo msikivu, ana hii ripoti mezani kweli? Na hatujasikia akichukua hatua zozote?


3. UHABA wa Petroli sasa hivi nchini.

Hapa siandiki sana.

Fahamuni kwamba mafuta yapo. Si mlisikia hata Waziri anasema hakuna upungufu wa petrol. Si amesema mara nyingi tu!

Sasa Mimi na wewe tuulizane, Waziri anasema yapo, vituoni ukifika hakuna, yapo wapi? Eeh...

Jamaa wana mafuta, ila hawatoi kuyauza. Wanasubiri bei mpya za August, zipande usiku wa leo tarehe 31/07/2023 ndio wataanza kutoa mafuta.

Sasa "syndicate" ya namna hii, hapo unasema TISS wapo na wananchi, au wametuma ripoti Rais hajachukua hatua?!

Achaneni na mambo ya ooh Dola $ kuadimika, hiyo inaathiri uagizaji wa mzigo mpya. Sio stock iliyopo ambayo huagizwa miezi mitatu au zaidi nyuma.

4. Nauli za mabasi za LATRA.

Hivi mnajua mabasi yote ya mikoani katika stendi zote za mikoani wanachaji nauli zaidi ya zile zilizoidhinishwa na LATRA?!

USHAHIDI upo.

Hapa namaanisha hata LATRA na mapolisi wanalijua hilo. Je, ni fungu wanapewa au kuamua kuacha tu unyang'anyi huu uendelee?!

Nasisitiza iko hivyo, stendi zote, mikoa yote.

Nenda Dsm, Mwanza, Morogoro, Iringa, Dodoma, Tabora, Kagera, Mbeya, Arusha, Tanga, Mtwara, Kigoma, n.k, kote huko wana 'overcharge'.

Sasa kama watu wa mabasi wanaona nauli zilizopangwa ni ndogo, haziwapi faida, si bora LATRA ipitishe hizo hizo wanazolipishwa wananchi ili ifahamike moja.

Je, unataka kusema ripoti za haya zipo mezani kwa mh. Rais ila jinsi alivyo anajali watu wake kweli asichukue hatua.?!

Narudia ripoti hii ni kwa nia njema ya kujenga Taifa letu.

Ukweli huduma za umma zimezorota kiasi kikubwa, tusifiche tatizo na wananchi wengi wanaumia sana na hili.

Naomba kuhitimisha hapo kwa leo.

Karibuni wachangiaji kwa mengi zaidi.
 
Nimesoma ripoti yote hakuna la uongo hata moja

1. Kwenye hilo la NIDA mpaka 50 watu wanapokea.. Rushwa!

2. La Nbagala hili lilishasemwa sasa! Mpaka namna tenda ilivyopatikana.. Rushwa!

3. La petrol kuna andiko limeichambua vizuri mno.. Rushwa!

4. La LATRA ni mulemule.. Rushwa..!

Ni rushwa ni rushwa ni rushwa mwanzo mwisho! Lakini si tunakumbuka angalizo la mkuu wa kaya kuhusu kula kwa urefu wa kamba? Dosari ilianzia hapo
 
Kwa hali hii ambayo nchi inapitia, uongozi mbovu, rushwa, ubinafsi, ufisadi, nepotism na vetting mbovu, uonevu nk tatizo ni TISS.

Chanzo cha tatizo ni muundo usiofaa tulio nao, yaani tunachagua mtu mmoja (Rais)wakati wa uchaguzi mkuu halafu anakuta pale ikulu timu ya watu (TISS) wengine wana miaka hata 20 wako hapo.

Cha kushangaza TISS siku zote wanadai kazi zao ni ngumu, hivi kuna mtu anapenda kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu, hata km analipwa vizuri, kwanini hatuoni wao TISS kuomba kubadilishiwa kazi kwa sabab ya kazi ngumu wanazofanya? hapa kuna hila na Kati ya mambo wanamwambia Rais mpya ni kuwa wao (TISS) ndio wamefanya yeye Rais afike hapo, maana yake, bila wao asingefika hapo na hivyo wao ndio wanao urais wake.

Rejea maneno ya Rais wa awamu ya 5 akilalamikia kuwa anachomekewa watu wasiofaa kwenye uteuzi(waziri mpya kushindwa kusoma kiapo) na imetokea Rais mstaafu anakuwa na watu wake wengi ndani ya TISS ili aendelee kuongoza ndicho kinachotokea Tanzania na inavyoonekana TISS inaundwa na kundi kubwa la vijana yaani ni under age kulingana na nature ya kazi wanazopaswa kufanya TISS kwa nchi, ndii maana uonevu ni mwingi sana Tanzania.

Kuna nchi moja ndani ya SADC Rais mpya alipoingia ikulu kwanza alibadilisha intelligence team yote, tumeona hata Rais Tinubu amefanya hivyo..

Pili, Rais huyo mpya aliteua intelligence team wote wapya na kazi ya kwanza aliyowaambia wafanye ni kwenda kila kata na kijiji ndani nchi kufanya mikutano ya hadhara ili kuwaambia wananchi KAZI ZAO NI ZIPI KWA NCHI.

Hivi tunavyoongea Rais mstaafu wa nchi hiyo na baadhi ya maafisa wakubwa wastaafu akiwemo chifu wa intelligence mstaafu wako uhamishoni wamekimbia nchi.

Hivi ndivyo wanaojua uongozi na wana ajenda ya maendeleo wanapochaguliwa hufanya mara tu wanapoanza urais.

Tanzania imekwama sabab kubwa ni vested interest za wastaafu kupitia TISS angalia baadhi ya mawaziri hata tu tathmini ndogo ya face value judgement kuona km wanastahili kuwa mawaziri inakupa jibu HAWASTAHILI..lakini hao ndio TISS inawataka wale wasiojielewa anasukumwa tu km boya!

Hii shida ya bandari kutokuwa na tija inayopelekea kutafuta wawekezaji chanzo ni TISS angalia huyo DG wa sasa wa TPA bado mtoto hana sifa kabisa za nafasi hiyo, na sabab za kuweka mtu wa aina hii ni wao TISS kuwa na access ya kuinfluence utendaji na maamuzi yake throughout, a similar case hata kwa spika wa bunge, taifa lenye umri zaidi ya miaka 60 eti halina watu wazima wenye sifa za kuwa spika au DG wa TPA..si kweli!

Dawa ni wananchi kudeal na issue ya TISS wanavyopatikana wakati Rais mpya akichaguliwa na kazi zao kwa ujumla..tusipofanya hivi, nchi itakwama zaidi ya hapa tulipo.
 
Matatizo na mambo uliyo yaelezea ndiyo Urefu wa kamba

Hivyo ukiona kimya!! Basi huo Urefu wa kamba ni ruksa kama DPW alivyo ruhusiwa kwani kamba inamruhusi aliye bariki!!
 
Back
Top Bottom