DOKEZO TAKUKURU na Usalama wa Taifa, fuatilieni haya; nchi inahujumiwa. Kuna rushwa, urasimu na ufisadi mkubwa

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
Mm nasema kwa nia njema haya yooote mama hajui na wala hana nia njema na tanganyika yetu.
Mpk sasa yy yuko majuu. Napia alisema YY ameziba masikio.
 
We lazimisha mazoea ya kishamba na ya hovyo na huyo mwamba.

Hakunaga urafiki wa raia na askari sasa jibalaguze akuoneshe true-color ndo utajua kilichomnyima kuku kukojoa
Ww nawe umevurugwa wewehai TISS si watu TU km wewe!!!atanifanya Nini Kwa mfano sasaa!!!!
Kaaahh....Yaani mtu kaka angu wa damu afu unasema nyenyenye Hapa ..hebu nipishe na stress zako
 
Kwa hali hii ambayo nchi inapitia, uongozi mbovu, rushwa, ubinafsi, ufisadi, nepotism na vetting mbovu, uonevu nk tatizo ni TISS.

Chanzo cha tatizo ni muundo usiofaa tulio nao, yaani tunachagua mtu mmoja (Rais)wakati wa uchaguzi mkuu halafu anakuta pale ikulu timu ya watu (TISS) wengine wana miaka hata 20 wako hapo.

Cha kushangaza TISS siku zote wanadai kazi zao ni ngumu, hivi kuna mtu anapenda kufanya kazi ngumu kwa muda mrefu, hata km analipwa vizuri, kwanini hatuoni wao TISS kuomba kubadilishiwa kazi kwa sabab ya kazi ngumu wanazofanya? hapa kuna hila na Kati ya mambo wanamwambia Rais mpya ni kuwa wao (TISS) ndio wamefanya yeye Rais afike hapo, maana yake, bila wao asingefika hapo na hivyo wao ndio wanao urais wake.

Rejea maneno ya Rais wa awamu ya 5 akilalamikia kuwa anachomekewa watu wasiofaa kwenye uteuzi(waziri mpya kushindwa kusoma kiapo) na imetokea Rais mstaafu anakuwa na watu wake wengi ndani ya TISS ili aendelee kuongoza ndicho kinachotokea Tanzania na inavyoonekana TISS inaundwa na kundi kubwa la vijana yaani ni under age kulingana na nature ya kazi wanazopaswa kufanya TISS kwa nchi, ndii maana uonevu ni mwingi sana Tanzania.

Kuna nchi moja ndani ya SADC Rais mpya alipoingia ikulu kwanza alibadilisha intelligence team yote, tumeona hata Rais Tinubu amefanya hivyo..

Pili, Rais huyo mpya aliteua intelligence team wote wapya na kazi ya kwanza aliyowaambia wafanye ni kwenda kila kata na kijiji ndani nchi kufanya mikutano ya hadhara ili kuwaambia wananchi KAZI ZAO NI ZIPI KWA NCHI.

Hivi tunavyoongea Rais mstaafu wa nchi hiyo na baadhi ya maafisa wakubwa wastaafu akiwemo chifu wa intelligence mstaafu wako uhamishoni wamekimbia nchi.

Hivi ndivyo wanaojua uongozi na wana ajenda ya maendeleo wanapochaguliwa hufanya mara tu wanapoanza urais.

Tanzania imekwama sabab kubwa ni vested interest za wastaafu kupitia TISS angalia baadhi ya mawaziri hata tu tathmini ndogo ya face value judgement kuona km wanastahili kuwa mawaziri inakupa jibu HAWASTAHILI..lakini hao ndio TISS inawataka wale wasiojielewa anasukumwa tu km boya!

Hii shida ya bandari kutokuwa na tija inayopelekea kutafuta wawekezaji chanzo ni TISS angalia huyo DG wa sasa wa TPA bado mtoto hana sifa kabisa za nafasi hiyo, na sabab za kuweka mtu wa aina hii ni wao TISS kuwa na access ya kuinfluence utendaji na maamuzi yake throughout, a similar case hata kwa spika wa bunge, taifa lenye umri zaidi ya miaka 60 eti halina watu wazima wenye sifa za kuwa spika au DG wa TPA..si kweli!

Dawa ni wananchi kudeal na issue ya TISS wanavyopatikana wakati Rais mpya akichaguliwa na kazi zao kwa ujumla..tusipofanya hivi, nchi itakwama zaidi ya hapa tulipo.
Kule Tanesco walimleta muuza ving'amuzi na ambaye ofisi yake ina wafanyakazi hawafiki 50 nchi nzima.
 
Back
Top Bottom