Serikali ya mseto? Au Makamba atkuwa amehamia CDM? Au Zitto atakuwa CCM? Ndani ya CCM hii ya sasa hakuna mgombea Urais mwenye sifa. Labda waje kama wagombea binafsi. Kwangu mimi Dr. Slaa, Fredrick Sumaye, Edward Lowassa na Salim Ahmed Salim ndio wanaofaa kugombea Urais lakini kwa sasa nchi inahitaji mtu kama Dr. Slaa
Kwanini?
1.Dr. Slaa- Anaonyesha kwa vitendo kwamba anasimamia yale anayoyasema, ana upeo mkubwa, ana uwezo wa kufanya maamuzi magumu (Ambao ni ugonjwa sugu wa Taifa), mwadilifu, hardworker, anachukia ufisadi kwa vitendo na ana sifa ya kuwa kiongozi (anaweza kwaongoza wengine)
2. Sumaye- Ana uzoefu wa uongozi, Elimu ya kutosha, akiwa Waziri Mkuu (miaka 10) walau nchi mafanikio yalikuwepo chini ya Rais Mkapa
3.Edward Lowassa- Anaweza kuamua na kusimamia maamuzi magumu (hata kama yatamgharimu), linapotokea tatizo kubwa anatafuta suluhu kama kiongozi, anajua dhana ya kuwajibika anapokosea (Ugonjwa mwingine kwa Tanzania), anaweza kuwasimamia watendaji walio chini yake, mvumilivu n.k
4.Dr.Salim Ahmed Salim- Kiongozi mzoefu, msomi, amebobea kwenye uongozi wa ndani na nje ya nchi, ana busara, pamoja na kuongoza taasisi kubwa za kimataifa hana doa lolote
Hata hivyo hawa watu wa mwisho watafaa ikiwa wanakuwa wagombea binafsi au wakiwa kwenye vyama lakini kwa KATIBA mpya itakayo punguza mamlaka ya Rais na kuruhusu Rais ashtakiwe kwa makosa aliyoyafanya akiwa madarakani. Aidha watafaa endapo Bunge na mahkama pia vitapewa meno ya kuwa independent na kuwa na uwezo kufanya Impeachement kwa Rais akiwa madarakani.