Taifa kwanza: Rais na mawaziri 2015

Taifa kwanza: Rais na mawaziri 2015

Hakuna Rais wa Tanzania kwenye hiyo list yako hapo kwa sababu zifuatazo;

1.Lowassa-Richmond, Dowans,Kaskazini hatoki Rais(Tamko CCM Pwani) na Makundi yake(Atamwaga Ugali)
2.Samuel Sitta-Visa na mikasa ya kukiaibisha chama Bunge la Tisa na makundi yake vs Lowassa(Atamwaga Mboga)
3.Mwandosya -Hana nguvu yoyote ndani ya CCM na hawamuelewi kama Atawalinda au Atawatosa mafisadi wenye CCM
4.Frederick Sumaye-Kaskazini Haitoi Rais,JK analo jina la mgombea(Tamko CCM Pwani) na uozo wake na Mkapa 1995-2005
4.Hussein Mwinyi- Kashfa za mabomu na changamoto za muungano kama uwepo usiwepo zinamnyima nafasi
5.Benard K. Membe- Aaaah!Nani anataka Rais mwingine mswahili na sharobaro muuza sura,Haturudii makosa ya 2005 na 2010.

CCM labda wajaribu J.P Magufuli angalau anaweza kupunguza kura za Rais Mtarajiwa His Excelence Dr.Wilbrod Peter Slaa

Nimeipenda hii analysis. Tuendelee kuwajadili wale wanaojipanga ikiwa ni pamoja na kuwachomekea wenzao wakiwahisi ni washindani.
 
Nitaungana na atakependekeza kiongozi nje ya hawa wanasiasa wa sasa wanaogombania posho MJENGONI.
 
seriously, huenda nitagombea kama mgombea huru iwapo hukumu ya mahakama ya Afrika italazimisha serikali iruhusu wagombea binafsi. Baraza langu litakuwa na watu wa kuaminika tu, na huenda PM wangu akawa Willie @NYC,USA iwapo atajivua kutoka kwenye gamba. Sitapenda kuhusisha wanachama wa chama chochote katika serikali yangu kwa sababu vyama vya siasa ndiyo chanzo cha ugonnjwa wa nchi hii. Wabunge wa CCM wamekuwa wanapitisha jambo lolote linalotolewa na serikali kwa sababu inaongozwa na mwenyekeiti wao.
 
W.J. Malecela,

Utaomba kila unachoomba na kuchambua watu kama karanga lakini the fact remains tunahitaji kwanza kuwaondoa Mtandao - the cartel, ambao najua fika haitakuwa kazi rahisi.

Labda nikukumbushe tena kwamba hawa jamaa wamechukua madaraka wakijua fika kwamba watatawala milele na sii kwa awamu moja ama mbili na ndio maana wamemweka JK kiti kikubwa kutokana na mfumo mbovu wa kiutawala tulokuwa nao. Sasa pigeni mahesabu ya rais sijui mawaziri mtakavyo lakini mfumo wanchi hii unamilikiwa na kiti kikubwa na kwa maarifa makubwa mtandao yaa hii cartel imehakikisha kiti kikubwa kinashikwa na kabuntas! mtu ambaye wananchi hawawezi kumhusisha na Ufisadi, mwenye roho mbaya, asiyeuzika na kadhalika, wakati wao wakiwa behind the scene..

Kwa hiyo, tukirudi na kujifunza kutokana na historia, Mtandao upande wa serikali wachezaji wakubwa ni RACHEL na bila kumsahau Six ambaye leo tunamwona kaokoka, lakini nawataarifu tu kwamba ktk mahesabu ya bao langu namwona Sitta kama ndiye mgombea atakayesimamishwa mwaka 2015 kama mgombea urais wa CCM kwa sababu amekoshwa tayari kwa wananchi kumpokea mwaka 2015 wakidhania ni msafi kama tulivyofikiria kwa JK.

Mimi nadhani Sitta ameondolewa makusudi na kusafishwa ili kusubiri 2015, hivyo itakuwa kazi kubwa sana kuwashinda mtandao kwa dhana ya kujiandaa kutafuta Utaifa kwanza kabla hatujamshinda adui aliyepo mbele yetu. Uzalendo ni ari ya kupambana na adui aliyepo na kumwondoa kurudisha usalama na viongozi bora ni wale watakaokuwa mstari wa mbele kupambana na adui huyo kifikra na kimwili. Dr.Slaa, Zitto, Kigoda, Mwandosya, Lipumba wote hawa sii lolote sii chochote ikiwa hatuelekezi nguvu zetu ktk kumwondoa adui yetu - Mtandao madarakani, na haitawezekana kwa kupitia sanduku la kura kwani Mtandano wamejipanga wanajipanga na wataendelea kujipanga ktk maandalizi ya uchaguzi mkuu wa 2015.

Mkuu, unapoongelea Cartel basi mtoe EL, vinginevyo ndio hao hao waliomkwamisha 2005. Kama ungefanyika uchaguzi leo, Six ana nafasi nzuri zaidi ya wengine lakini 2015 ni mbali lolote linaweza kutokea.
 
seriously, huenda nitagombea kama mgombea huru iwapo hukumu ya mahakama ya Afrika italazimisha serikali iruhusu wagombea binafsi. Baraza langu litakuwa na watu wa kuaminika tu, na huenda PM wangu akawa Willie @NYC,USA iwapo atajivua kutoka kwenye gamba. Sitapenda kuhusisha wanachama wa chama chochote katika serikali yangu kwa sababu vyama vya siasa ndiyo chanzo cha ugonnjwa wa nchi hii. Wabunge wa CCM wamekuwa wanapitisha jambo lolote linalotolewa na serikali kwa sababu inaongozwa na mwenyekeiti wao.
hapo penye red, unanitafutia ban. bora tuongozwe na kuku kuliko huyo mpuuzi
 
Mhe. Mwai Kibaki wa Kenya kwa mara ya kwanza aliibuka mshindi kupitia NARC na kumbwaga mpinzani wake kutoka chama tawala cha KANU Bw. Uhuru Kenyatta aliyepandikizwa ili kulinda maovu ya viongozi waliopita ingawa hata Kibaki alipoingia Ikulu hakuna aliyeshughulikiwa kama ilivyohofiwa hapo awali.

Miezi kadhaa baadaye Kibaki huyo huyo aliitisha kura ya maoni kuhusu mapendekezo ya katiba mpya ya Kenya, yeye akawa upande wa 'banana' na wengine upande wa 'Orange', sote tunakumbuka kwamba upande wa 'Orange uliibuka kidedea.

Wakati huo nilikuwa Shinyanga nikakutana na Mkenya mmoja aitwaye Mr. Mike aliyekuwa anahusika katika ujenzi wa barabara ya Mza/Shy Border - Tinde (yeye alisafiri kutoka Shinyanga kwenda Kisumu kupiga hiyo kura ya maoni), nilimwuliza kwa nini wamembwaga Mhe. Kibaki katika kura ya maoni ilhali walimchagua kwenye uchaguzi mkuu kuwa rais anayefaa kuwaongoza?

Mr. Mike alinijibu kuwa Kibaki alipata kura nyingi za Wakenya kwa lengo la kuondoa utawala dhalimu wa chama cha KANU uliodumu tangu uhuru wa nchi hiyo, hivyo ilikuwa ni lazima KANU iondoke madarakani! Siyo kwamba Kibaki alikuwa na sifa njema saana za kuwa rais!

Wakati umefika kwa Watanzania kujifunza kitu fulani hapa, kwamba ili tuweze kufikia demokrasia na maendeleo ya kweli hoja yetu iwe ni kukiondoa chama tawala madarakani, bila hivyo tusitegemee miujiza ya aina yoyote kuhusu mawaziri na watendaji wengine wa serikali watakaoteuliwa. Uwezo wa kuleta mabadiliko tunao sisi wananchi wenyewe, huu ni muda muafaka wa kupeleka mbiu hii kwa ndugu, jamaa na marafiki popote walipo watumie kura zao vizuri 'to Vote out the ruling party'. Natambua changamoto zilizopo kuwafikia wananchi walioko vijijini ambao kila wakiambiwa 'tieni kwa moyo mmoja' wanafanya hivyo hivyo bila kuzingatia ubora wa watu wanaowachagua.

Kama wana JF 20,000 tu ambao wanauchungu na nchi hii wakiingia mitaani kupeleka mbiu hii kila mmoja atahitaji kuwafikia watu angalau 1,000 tu kwa miaka minne iliyosalia maana yake ni kwamba kwa mwaka mmoja angalau awafikie watu 250 tu wenye sifa za kupiga kura, jambo ambalo linawezekana!
 
Tatizo kubwa linalokwamisha maendeleo ya nchi ni rushwa, kisakologia imeaffect watu wengi sana kuanzia mfanyakazi wa ngazi za chini mpka wa juu.

Mkapa alikuwa anasema maendeleo yataletwa na wananchi wenyewe kwa kufanya kazi kwa bidii lakini mfanyakazi wa TRA aliyoko mkoani anajiuliza kwa nini nifanye bidii kukusanya kodi wakati italiwa huko juu na mfanyabiasha wa mahindi nae anajiuliza kwa nini nilipe kodi wakati wakati wawekezaji wakubwa hawalipi, wote wanaishia kuangalia jinsi ya kupokea au kutoa rushwa.

Mimi binafsi kigezo kikubwa nitakacho tumia kuelekea 2015 ni mtu yoyote ambaye AMESHATOA MCHANGO WAKE WA KUPAMBANA NA RUSHWA bila kuogopa na sio wanaotaka urais kwa kwa kuvizia .

Katika ya walioshatajwa tajwa ;
1) Dkt Slaa
2) Dkt Mwakyembe
3) Dkt Magufuli
4) Sitta (Msimamo wake sasa hivi unaridhisha)
 
Back
Top Bottom