ANGALIZO: -/ ziko shule mbalimbali huko ilala na temeke na pembezoni mwa mji zinazofundisha mashuleni KUNG FU KWELI NI MCHEZO LAKINI KWA SASA IMEKUWA TOO MUCH KWA NINI MICHEZO HII ISICHEZW3 KATIKA MABARAZA YA MICHEZO YANAYOTAMBULIKA ,KWANINI KUNG FU INASISITIZWA KTK MASHUL3 YA KIDINI TU HASA YA KIISLAMU / QUIET DANGEROUS/ MICHEZO HII IEUHUSIWW KTK SEHEMU ZINAZOTAMBULIKA RASMK
Extra curricular activities !! Michezo mbalimbali kama Mpira, Volleyball, basketball, Tennis, Karate, Judo, Kung-fu na mengineyo haijakatazwa na sheria yoyote kufundishwa katika mashule, madrasa au misikitini. Laiti kama Nchi yetu ingekuwa na utaratibu maalumu, vijana kama hao wangeweza kuliwakilisha Taifa katika Kungfu, Judo, Karate na kuliletea Medali tofauti.
Shule hizo kimsingi zinatekeleza Sera ya Taifa ya Michezo ambayo inatoa umuhimu wa michezo kama hiyo;
"Michezo ikiwa ni kiungo muhimu cha utamaduni katika jamii yetu, umuhimu wake nikama ifuatavyo:-
i) Kujenga na kuimarisha afya njema na maisha bora kwa wote;
ii) Kujenga tabia ya ushirikiano, upendo, udugu na uzalendo;
iii) Kujenga taifa lenye nidhamu;
iv) Kujenga uhusiano, uelewano na mshikamano wa Taifa;
v) Kujenga moyo wa kishujaa na kujihami kukuza ukakamavu ujasiri na kujiamini;
vi) Kuwapatia wananchi burudani;
vii) Kulitambulisha na kulitangaza taifa nje ya mipaka yake;
viii) Kumjenga mchezaji kuwa mtu kamili kimwili, kiakili na kiroho kuanzia utotoni hadi uzeeni "
KWA NINI MICHEZO HII ISICHEZW3 KATIKA MABARAZA YA MICHEZO YANAYOTAMBULIKA
Kwa kuwa tuna BMT, Tusaidie majina ya Vyama Rasmi vinavyohusika na Michezo ya Kareti ili vijana wajiunge au wafundishe namna gani wanaweza kuunda vyama vyao ili watambuliwe kisheria, licha ya hivyo, Shule ni sehemu inayotambulika Rasmi, mingi katika misikiti na madrasa zina usajili, hivyo zinatambulika, na kwa hali hiyo kwa kuwa wanatekeleza sera katika sera za michezo bila ya kuvunja sheria wala Amani hakuna haja ya kuwadhania tofauti.
KWANINI KUNG FU INASISITIZWA KTK MASHUL3 YA KIDINI TU HASA YA KIISLAMU
Shule nyinginezo hazijakatazwa, tena tuwashauri wajenge na wao Dojo za kutosha tu tuwaokoe vijana wetu katika shughuli zisizo na tija kama ya Ku BET na kuwajenga katika ukakamavu na ujasiri hata kabla hawajaenda JKT.
Pitia Sera ya Taifa ya Michezo
HAPA