tpaul
Platinum Member
- Feb 3, 2008
- 27,197
- 27,817
Leo asubuhi nimepita mahali fulani hapa Dar nikawashuhudia watu wamevaa kininja na vilemba vya kigaidi wakifanya mazoezi ya kungfu na kareti bila wasiwasi wowote.
Mwalimu wao mwenye asili ya kisomali alisikika akiwapa maelekezo kwa lugha ya kiarabu huku akiwa mkali kwa wale walioonekana kukosea maelekezo yake. Kikundi hiki ni cha watu wasiopungua 15.
Hatuwezi kujua vikundi hivi viko vingapi hapa jijini na kama mafunzo haya ya kigaidi wanayopata wataenda kuyatekeleza wapi. Hivyo ni jukumu la kila mmoja wetu kuwa makini na kuchukua tahadhari pindi atakapoona vikundi kama hivi.
Ulinzi na amani ya Taifa letu ni jukumu la kila raia. Juzi kati tumeshuhudia mtanzania mwenzetu akikamatwa kwa sababu za kigaidi. Huenda ugaidi huu amejifunzia hapahapa Tanzania. Chukua tahadhari kabla ya hatari!
UPDATE
tukio limeisharipotiwa kituo cha polisi na wanausalama hao wameahidi kulichunguza kwa umakini na kunipa mrejesho. tuendelee kuwa watulivu wakati polisi wakifanya uchunguzi wao. wote mnaonitukana nimewapuuza.