Tafakuri ya FaizaFoxy: CCM imetegwa ikategeka?

Tafakuri ya FaizaFoxy: CCM imetegwa ikategeka?

Kazi kweli kweli! Upinzani haupo Tanzania wote ni wasaka tonge tu.

Unakubali vipi kushiriki uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi ?

Wapinzani hawana mikakati thabiti they just act as opportunists to grab any thing comes their ways ,2020 watapigwa chini vibaya mno.

CCM bila polisi, usalama wa Taifa, Wakurugenzi, NEC-CCM ni wepesi kushinda unyoya
 
Kazi kweli kweli! Upinzani haupo Tanzania wote ni wasaka tonge tu.

Unakubali vipi kushiriki uchaguzi bila tume huru ya uchaguzi ?

Wapinzani hawana mikakati thabiti they just act as opportunists to grab any thing comes their ways ,2020 watapigwa chini vibaya mno.

Mkuu ww umefanya jitihada gani kuhakikisha kuna tume huru ya uchaguzi? Au nyie ndio wale mnaokejeli humu, kisha yakitokea machafuko kwa sababu ya haki kupindishwa mnaishia kusema amani ya nchi inapotea? Unaweza kijitapa wapinzani watapigwa chini vibaya mno huku ukijua fika dhuluma ndio inayopelekea hayo?
 
"Siyo Siasa wala maslahi binafsi".
Nimekuna kichwa nikiwaza. Sikupata jibu!

Itakuwa nini? Kutishwa? Kumpenda mtu binafsi? Hapa umenitoa shai!

KKwenye kile nilichoandika hukuyaona maneno haya "Soma alama za nyakati kwa kuangalia matukio"? Hiyo ndiyo key statement kwenye hicho nilichoandika. Asilimia 99% ya Wa-Tanzania huwa tunaona Siasa tu, tunasahau kwamba kuna mengine mengi nayo pia huwa yapo yanaendelea ila yanaonekana KAMA Siasa wakati katika Uhalisia siyo Siasa.Kwa mfano, zuio la mikutano ya siasa nayo pia ni Siasa, kisa kilichozuiwa ni mikutano ya Kisiasa? Angalia matukio!
 
Licha ya mchezo wa bao kuwepo takriban Tanzania nzima, lakini mchezo huo Kusini umekuwa maarufu zaidi kwa kuwa kwanza inajulikana wachongaji mabao mazuri ya nakshi ni wamakonde, na kusini ndiyo kwao. Pili, "mikete", miti ambayo hudondosha kokwa za kete zinazochezewa bao ipo mingi Kusini.

Faiza mara nyingi nilikuwa naona wewe ni islamist na hoja zako mara nyingine zililenga huko. Nafurahi sana kuona leo umejikumbuka kuwa ni Mtanzania, na nimefurahi kuona mwelekeo wako unabadilika kuelekea kuangalia nchi.

Nikija kwenye hoja yako, kwanza niseme mimi naunga mkono mambo yanbayoendelea kwenye chama hasa kutoka kwa mwenyekiti na katibu. Lakini nina wasiwasi kuwa udhati tunaouona unatoka kwa mwenyekiti, katibu na viongozi wachache wa juu. Naona bado CCM kuna majitu yana uchu yanataka turudi kule kule kwenye mambo ya ovyo.

Mchezo wa bao uliosema unaonesha kabisa kuwa wanasiasa wengi wa CCM wanalazimika kutakata, wanataka ili walau wawe kuwa na mtaji kwenye mchezo unaokuja. Napenda sana Bashiru anavyowalazimisha kutakata, na usafi wa serikali ya JPM umekula mitaji yao yote. Kila wanapojaribu naona wanaishia kugona tu. Kwa hiyo hata wawe na mikete kiasi gani, wataendelea kugona, kwa kuwa hawana mitaji.
 
Si kweli. Ingekuwa hivyo tusingeona wenyeviti wa serikali za mitaa, vijiji, madiwani na wabunge wa upinzani.
CCM ni chama cha kupigiwa mfano duniani.
Dunia ipi?chama kinachookoa millioni za kuchora twiga na kupoteza mabilioni kwa kugharamia uchaguzi wa kijing.a.
 
Dunia ipi?chama kinachookoa millioni za kuchora twiga na kupoteza mabilioni kwa kugharamia uchaguzi wa kijing.a.
Siku mgombea wako akishinda hutauona wa kuuhisi huo ujinga.

Kwa fikra kama zako kuna punguani ataewapigia kura kweli?
 
Unafahamu maana ya marehem na hayati?

Hayo maneno yote yametokana na Kiarabu na nnauhakika Kiarabu hukifahamu.
ninafahamu na kiarabu nakijua, ndio maana nimekurekebisha, labda Kama ulilenga kumdunisha tu Hayati baba wa taifa
 
Wapinzani hawana Mbinu kama hizo,na hawana uwezo wa kupanga suala kama hilo!!

Nashangaa uyatambui mambo kama haya, wao wako busy na siasa za matukio ya Muda mfupi mfupi
Kama vile., Magufuli hajui kizungu! Massele, CAG ,

Natamani tuupate upinzani imara usiokuwa na mizengwe,
Tutafurahi kama utauanzisha wewe huo upinzani makini unaouongelea. Kama hutaweza basi hauna sababu ya kuwalaumu hao wapinzani.
 
Back
Top Bottom