FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,506
- 123,802
Kwa mtu yeyote aneifahamu Kusini ya mkoa wa Dar Es Salaam ataelewa kuwa ukianza kufika Mtoni (kwa Aziz Ali) kushuka Kusini utakutana na mchezo wa bao la kete (solo).
Bao la kete Kusini ya Tanzania ni mchezo unaochezwa na takriban jamii nzima, kuanzia watoto, vijana hadi wazee, wote, akina mama na akina baba. Bao lina aina ya michezo mingi tofauti. Lakini maarufu ni ule wa kusafiri, kutakata, kutembea, kulala na kuulinda mtaji. Ambao hufanyiwa mashindano ya kitaifa. Marehemu Mzee Nyerere alikuwa ni mpenzi wa mchezo huu wa bao na alikuwa bingwa.
Licha ya mchezo wa bao kuwepo takriban Tanzania nzima, lakini mchezo huo Kusini umekuwa maarufu zaidi kwa kuwa kwanza inajulikana wachongaji mabao mazuri ya nakshi ni wamakonde, na kusini ndiyo kwao. Pili, "mikete", miti ambayo hudondosha kokwa za kete zinazochezewa bao ipo mingi Kusini.
Kwanini nimelikumbuka bao? Bao Lina mitego na mahesabu ya hali ya juu sana kwa wenye kulijuwa kulicheza vizuri, wanaweza kumtega mtu mpaka mizunguko mitano ijayo na kila mzunguko aliyetegwa atakuwa anahisi anashinda tu lakini ndiyo anazidi kumtengenezea njia ya ushindi aliyemtega.
CCM siku za nyuma kidogo imepokea wapinzani wengi sana waliotokea vyama vya upinzani kutoka kada mbali mbali, kuanzia washabiki na wanachama wa kawaida, wenyeviti wa serikali za mitaa, madiwani, wabunge na wengi wengine.
Jee, huu siyo mtego wa upinzani kupandikiza mapandikizi ya kuja kuisambaratisha CCM? Jee, CCM imetegwa ikategeka? CCM tunachezewa "chess" au bao?
Upinzani wa Tanzania unaweza kuwa na vichwa na mahesabu na mitago ya kisiasa kama mahesabu na mitego ya mabingwa wa bao kama Mzee Nyerere, vya kuweza kutega mizunguko mitano ijayo?
Ni tafakuri tu ya FaizaFoxy.