Tafakuri ya FaizaFoxy: CCM imetegwa ikategeka?

Tafakuri ya FaizaFoxy: CCM imetegwa ikategeka?

Mapenzi yanahusu nini? Kuna mapenzi kwenye siasa? Labda ya Esther na Halima.
Your IQ Capacity is at work....
Hahahahah... CCM ni zaidi ya kinyesi[emoji216].
[emoji3][emoji16][emoji23][emoji3][emoji16][emoji23][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23]
 
Kuanzia mwaka 2016 mpaka Leo kuna hujuma kubwa sana kwa wafanyabiashara hasa wale waliokuwa wanamshangilia Team nywele nyeupe au wazee wa mabadiliko, Utafanyiwa kila aina ya fugisu za kodi na utasalimu amri tu,

Kadi imenifanya nionekane nipo Team pendwa kwa sasa, wakisikia mzigo wa mtoto wa fulani haina shida

Kumbuka kwa biashara zetu Tanzania ni wachache wanaweza kodi meli yote peke yako, Tunashare meli sasa watu wakiona Team nywele nyeupe kwenye mzigo utapata tabu sana

HIZI BIASHARA ZINAFUNGWA KUNA MAMBO MENGI FAIZA, MENGINE TUNAUMIA NDANI, KUSEMA TUNAOGOPA
FITINA NA UJINGA UMEJAA KATI YA TIMU MBILI ZA MPIRA

Nchi moja tumeamua kuharibu biashara kisa Team za mpira za 2015
Nakubaliana na wewe kabisa
 
Your IQ Capacity is at work....
Hahahahah... CCM ni zaidi ya kinyesi[emoji216].
[emoji3][emoji16][emoji23][emoji3][emoji16][emoji23][emoji16][emoji16][emoji23][emoji23]
Jifikirie wewe sasa ubaetawaliwa na kinyesi, tukuite nani? Kipindupindu?
 
Kwa mtu yeyote aneifahamu Kusini ya mkoa wa Dar Es Salaam ataelewa kuwa ukianza kufika Mtoni (kwa Aziz Ali) kushuka Kusini utakutana na mchezo wa bao la kete (solo).

Bao la kete Kusini ya Tanzania ni mchezo unaochezwa na takriban jamii nzima, kuanzia watoto, vijana hadi wazee, wote, akina mama na akina baba. Bao lina aina ya michezo mingi tofauti. Lakini maarufu ni ule wa kusafiri, kutakata, kutembea, kulala na kuulinda mtaji. Ambao hufanyiwa mashindano ya kitaifa. Marehemu Mzee Nyerere alikuwa ni mpenzi wa mchezo huu wa bao na alikuwa bingwa.

Licha ya mchezo wa bao kuwepo takriban Tanzania nzima, lakini mchezo huo Kusini umekuwa maarufu zaidi kwa kuwa kwanza inajulikana wachongaji mabao mazuri ya nakshi ni wamakonde, na kusini ndiyo kwao. Pili, "mikete", miti ambayo hudondosha kokwa za kete zinazochezewa bao ipo mingi Kusini.

Kwanini nimelikumbuka bao? Bao Lina mitego na mahesabu ya hali ya juu sana kwa wenye kulijuwa kulicheza vizuri, wanaweza kumtega mtu mpaka mizunguko mitano ijayo na kila mzunguko aliyetegwa atakuwa anahisi anashinda tu lakini ndiyo anazidi kumtengenezea njia ya ushindi aliyemtega.

CCM siku za nyuma kidogo imepokea wapinzani wengi sana waliotokea vyama vya upinzani kutoka kada mbali mbali, kuanzia washabiki na wanachama wa kawaida, wenyeviti wa serikali za mitaa, madiwani, wabunge na wengi wengine.

Jee, huu siyo mtego wa upinzani kupandikiza mapandikizi ya kuja kuisambaratisha CCM? Jee, CCM imetegwa ikategeka? CCM tunachezewa "chess" au bao?

Upinzani wa Tanzania unaweza kuwa na vichwa na mahesabu na mitago ya kisiasa kama mahesabu na mitego ya mabingwa wa bao kama Mzee Nyerere, vya kuweza kutega mizunguko mitano ijayo?

Ni tafakuri tu ya FaizaFoxy.
 
Si kweli. Ingekuwa hivyo tusingeona wenyeviti wa serikali za mitaa, vijiji, madiwani na wabunge wa upinzani.

CCM ni chama cha kupigiwa mfano duniani.
Mchangiaji kasema Bila TIS,POLICCM, kwa ufupi U-Dolaism. jibu lako hali jaonesha chama hicho kutosaidiwa na Dola, hao uliowataja hawamaanishi chama kimejitenga na Udolaism.
 
Maana jinsi Magufuli na Bashiri walivyousambaratisha upinzani na tunavyoona jinsi wimbi la upinzani lililorudi CCM, inatisha, inabidi mtu ujiulize na kufikiri nje ya boksi.
Mnauaminisha umma CCM kipo vizuri huku mna Nag'ang'ana na MBELEKO Ya Ma DED hahahahaaaaa ......, kama mnajiamini Acheni tume iwe huru. Ondoeni hao makada kwenye usimamizi..... alafu mshinde ,hapo walau mnaweza ongea.....,
Eti kada wa chama ndio msimamizi mkuu wa uchaguzi ....Mnashinda watu mnajigamba hamuoni aibu[emoji40] [emoji40] [emoji40]
 
Mimi binafsi nimetafuta kadi ya CCM kwa shinikizo la Mzee wangu, Mwaka 2015 nyumba nzima Yeye pekee alikuwa anasifia ccm kisa anapata pesa na cheo kupitia huko ccm

Leo hii yeye anakumbuka bora angetusikiliza, maana alikuwa mbogo hata kwa mke wake, Anaona chama kinaharibika kimeingiliwa na mamluki wageni

Mimi binafsi nashukuru baada ya kuwa na kadi, Mzee akanitambulisha baadhi ya maeneo ya wana ccm mkakati sasa Biashara na mambo yangu yamenyooka, Sisumbuliwi sana kutoa vitu bandari

Nitaponda ccm lakini kuna muda nasifia kuangalia maslahi yangu binafsi yasiharibike
Wengi wao ni kama Wewe, Tumbo kwanza HAKI
na UKWELI baadae. full usheitwan......
 
Mnauaminisha umma CCM kipo vizuri huku mna Nag'ang'ana na MBELEKO Ya Ma DED hahahahaaaaa ......, kama mnajiamini Acheni tume iwe huru. Ondoeni hao makada kwenye usimamizi..... alafu mshinde ,hapo walau mnaweza ongea.....,
Eti kada wa chama ndio msimamizi mkuu wa uchaguzi ....Mnashinda watu mnajigamba hamuoni aibu[emoji40] [emoji40] [emoji40]
CCM hata isimamishe mgombea hewa itapita.

Hivi CCM ishindwe na chama kipi cha upinzani kwa sasa?
 
Mchangiaji kasema Bila TIS,POLICCM, kwa ufupi U-Dolaism. jibu lako hali jaonesha chama hicho kutosaidiwa na Dola, hao uliowataja hawamaanishi chama kimejitenga na Udolaism.

Ni kama unasema "Mwalim, una wanao wanasoma darasa unalofundisha, usiwafundishe!" Badala ya kusema "Mwalim ana wanawe wanasoma darasa lile lile na wanangu ngoja nifanye bidii ña kazi ya ziyada wanangu wàshinde".
 
Back
Top Bottom