Tafakuri ya FaizaFoxy: CCM imetegwa ikategeka?

Tafakuri ya FaizaFoxy: CCM imetegwa ikategeka?

Wakati wa JK sio ninyi watanzania mlimtuhumu kuwa amekigawa chama kwa makundi ya wanamtandao na ccm nyingine sijui zalendo?
Leo tena jk was better than?
Akiondoka jpm nina hakika atakaekuja atasemwa ni the baddest...sisi watanzania kituelewa yataka digirii ya unafiki.
Hata kinyesi kina harufu tofauti lakini unafuu huo haundoi sifa kuwa vyote ni vinyesi
 
Ukiwa kwenye madaraka ya kuendesha nchi kuna mengi sana unayoyajuwa kuliko ukiwa nje ya madaraka ya nchi, kuna mengine fitna kuna mengine kweli.

Nnakumbuka Kikwete aliwahi kusema kuna watu "wana viwanda vya uongo". Kwa hiyo usifikiri kila baya linafanywa na chama tawala, kuna watu wana mitego ili tu wakuchafulie. Pia kuna watu wako so "aggressive" wanaweza kufanya chochote ili wakupokonye tonge lako.

Fikra za kuwa mtu anakwenda kwenye kibanda cha kupigia kura huku analazimishwa mpigie fulani ni potofu. Waliochaguliwa ni watu na wamechaguliwa na watu kwa kura za halali kabisa.

Mbona kuna wapinzani bungeni, na wengi walikuwa CCM walipohamia upinzani wakachaguliwa vile vile? Kungekuwa kuna mabavu ungewaona akina Bulaya, Slaa, Shibuda bungeni?

Fikiri.
KONGOLE KWAKO DADA, NIMEZIMIS SANA NONDO ZAKO::: Nikadhani umetingwa na majukumu ya uteuzi wako maana ulikuwa haukosekani kwenye jukwaa pendwa kabla ya majukumu rasmi ya ujenzi wa nchi yetu pendwa unaoendelea kwa kasi ya mionzi ya x-ray. Waache aendelee kujipanga kwenye safu za uongozi kwa kutumia ndoto. Wamuulize Malema wa S/A kilichomtokea hakuamini hadi sasa. Ushindi wa mwaka 2020 utakuwa kama wa sunami, wajiandae kisaikolojia mwaka huu katika serikali za mitaa hiyo itawapa picha wapi tunapoelekea
 
Yaani hizo pumba kwako ndio nondo? Ama kweli ganda la muwa la jana chungu huona kivuno.

Hapa unazungumzia uchanguzi upi ambao ambao kina Bulaya na wengine walishinda?

Hicho kilikuwa kipindi kingine kabisa . Kama kweli wewe ni mkweli wa nafsi yako ,hebu angalia changuzi za hivi karibuni uone nini kimetokea.
 
Yaani hizo pumba kwako ndio nondo? Ama kweli ganda la muwa la jana chungu huona kivuno.

Ndiyo maana yake, hauoni kama tayari zimeshawagonga vichwa hadi mnatafutana wapi pakukimbilia
 
Maana jinsi Magufuli na Bashiri walivyousambaratisha upinzani na tunavyoona jinsi wimbi la upinzani lililorudi CCM, inatisha, inabidi mtu ujiulize na kufikiri nje ya boksi.
Kwa huu "uzushi" wa Magufuli na Bashiru kusambaratisha upinzani, mada yako imebaki inaelea.
 
Kenge kweli wewe huu upuuzi umgonge nani? Makamongo akili zenu huwa mnamkabidhi kamongo mkuu so sikushangai
Ndiyo maana yake, hauoni kama tayari zimeshawagonga vichwa hadi mnatafutana wapi pakukimbilia
 
Kuanzia mwaka 2016 mpaka Leo kuna hujuma kubwa sana kwa wafanyabiashara hasa wale waliokuwa wanamshangilia Team nywele nyeupe au wazee wa mabadiliko, Utafanyiwa kila aina ya fugisu za kodi na utasalimu amri tu,

Kadi imenifanya nionekane nipo Team pendwa kwa sasa, wakisikia mzigo wa mtoto wa fulani haina shida

Kumbuka kwa biashara zetu Tanzania ni wachache wanaweza kodi meli yote peke yako, Tunashare meli sasa watu wakiona Team nywele nyeupe kwenye mzigo utapata tabu sana

HIZI BIASHARA ZINAFUNGWA KUNA MAMBO MENGI FAIZA, MENGINE TUNAUMIA NDANI, KUSEMA TUNAOGOPA
FITINA NA UJINGA UMEJAA KATI YA TIMU MBILI ZA MPIRA

Nchi moja tumeamua kuharibu biashara kisa Team za mpira za 2015
Kuna busara nazichota hapa mkuu wangu endelea kutiririka.
 
Si kweli. Ingekuwa hivyo tusingeona wenyeviti wa serikali za mitaa, vijiji, madiwani na wabunge wa upinzani.

CCM ni chama cha kupigiwa mfano duniani.
Ondoa neno Duniani tafadhali huu ni mwezi mtukufu!😎
 
Kuanzia mwaka 2016 mpaka Leo kuna hujuma kubwa sana kwa wafanyabiashara hasa wale waliokuwa wanamshangilia Team nywele nyeupe au wazee wa mabadiliko, Utafanyiwa kila aina ya fugisu za kodi na utasalimu amri tu,

Kadi imenifanya nionekane nipo Team pendwa kwa sasa, wakisikia mzigo wa mtoto wa fulani haina shida

Kumbuka kwa biashara zetu Tanzania ni wachache wanaweza kodi meli yote peke yako, Tunashare meli sasa watu wakiona Team nywele nyeupe kwenye mzigo utapata tabu sana

HIZI BIASHARA ZINAFUNGWA KUNA MAMBO MENGI FAIZA, MENGINE TUNAUMIA NDANI, KUSEMA TUNAOGOPA
FITINA NA UJINGA UMEJAA KATI YA TIMU MBILI ZA MPIRA

Nchi moja tumeamua kuharibu biashara kisa Team za mpira za 2015
Chai
 
Athari yake ndani ya ccm ni furaha kwetu sisi wapenda mabadiliko! maana utakapowadia muda wa uchaguzi mkuu hasa ule wa 2025, iwapo Rais wa sasa atakubali kuondoka madarakani kwa mujibu wa sheria, basi tutegemee ccm kupitia kipindi kigumu zaidi ya kile cha 2015.
Mkuu Tate, ingawa nakubaliana na mengi uliyoandika kuhusu vyama vyetu vya siasa, hili la CCM 2025 'kuondoka madarakani' ni gumu kuliamini kwa sasa.
Kama ilivyo kawaida yake, wakati huo ukiwadia wanatumia mbinu zile zile za kuwapumbaza waTanzania wanazozitumia miaka yote. Na kwa vile CCM inawafahamu vizuri wananchi wa nchi hii, haipati shida ya kuwachota akili zao kwa njia mbalimbali, ikiwemo pamoja na kutumia nguvu za dola.
Watatafuta mtu wao mmoja, kama Makamba hivi na kumpamba na sifa utadhani ametoka sayari mpya na kuuza kwa waTanzania. Jambo dogo la plastiki tu, umeanza kuona hata humu JF wapambe walivyokuja kivyao kupamba utadhani kafanya jambo la ajabu sana.
Wapinzani, kwa mbinu wanazotumia sasa hivi hawana nafasi ya kuiondoa madarakani CCM.
 
Naweza kusema kuwa zaidi ya asilimia 90% ya watu waliohama kutoka upinzani kwenda CCM, ikiwa ni pamoja na wale walioteuliwa moja kwa moja kutokea upinzani, hawakufanya hivyo kwa sababu za kisiasa au maslahi binafsi. Soma alama za nyakati kwa kuangalia matukio. Siyo Siasa wala maslahi binafsi
"Siyo Siasa wala maslahi binafsi".
Nimekuna kichwa nikiwaza. Sikupata jibu!

Itakuwa nini? Kutishwa? Kumpenda mtu binafsi? Hapa umenitoa shai!
 
Si kweli. Ingekuwa hivyo tusingeona wenyeviti wa serikali za mitaa, vijiji, madiwani na wabunge wa upinzani.

CCM ni chama cha kupigiwa mfano duniani.
Kama ni hivyo kwanini mnasigina katiba kwa kupinga hukumu ya mahakama iliyowatupa wakurugenzi ambao imethibitika ni wanaccm ?
 
Hakuna hujuma yoyote. Ukisoma ilani ya uchaguzi ya CCM utagundua kuwa awamu hii imefikia katika kupambana na ufisadi na hata kwenye ilani kuna mpaka kufunguliwa mahakama ya ufisadi. Na ndicho serikali inachokifanya.

Serikali inajitahidi kupambana na kuzini mia nay ya ufisadi (corruption). Unataka kunambia hakuna wana CCM walioshikwa kwa ufisadi?

Bado hujanijibu, bandarini ukienda kuitoa mizigo yako unaulizwa kadi ya CCM?

Hama hama inatokana na demokrasia yetu kuwa changa. Tanzania bado demokrasia inatumika vibaya mfano wafanyabiashara wanaoenda upinzani wanalalamika kuwekewa mizegwe na hii inasababisha wahamiaji wengi kuhama kwa maslahi tu wala sio sera. Hii ndiyo sababu wakihama wanasema kuunga jitihada! tu. Sijawahi kusikia mtu aliyehama akaeleza sababu za msingi za kisera zaidi ya kuunga mkono jitihada sasa angalieni waliohama wamefanya nini mpaka sasa kuunga mkono jitihada yaani kuhama peke yake inasaidia nini?
 
[QUOTE=" Jee, huu siyo mtego wa upinzani kupandikiza mapandikizi ya kuja kuisambaratisha CCM? Jee, CCM imetegwa ikategeka? CCM tunachezewa "chess" au bao?

Upinzani wa Tanzania unaweza kuwa na vichwa na mahesabu na mitago ya kisiasa kama mahesabu na mitego ya mabingwa wa bao kama Mzee Nyerere, vya kuweza kutega mizunguko mitano ijayo?

Ni tafakuri tu ya FaizaFoxy.[/QUOTE]

Nimependa maswali yako lakini hao waluofanya biashara ya kununua wapinzani wanatakiwa wakujibu maswali yako.

Wali waninua wapinzani wakiwa na malengo gani jee, ni kuimarisha ccm au ni kudoofisha upinzani?
 
Waliorudi CCM ni waliwale walioondoka na Lowasa na wote wamesharejea nyumbani
Kwa mtu yeyote aneifahamu Kusini ya mkoa wa Dar Es Salaam ataelewa kuwa ukianza kufika Mtoni (kwa Aziz Ali) kushuka Kusini utakutana na mchezo wa bao la kete (solo).

Bao la kete Kusini ya Tanzania ni mchezo unaochezwa na takriban jamii nzima, kuanzia watoto, vijana hadi wazee, wote, akina mama na akina baba. Bao lina aina ya michezo mingi tofauti. Lakini maarufu ni ule wa kusafiri, kutaka ta, kutembea, kulala na kuulinda Miraji. Ambao hufanyiwa mashindano ya kitaifa. Marehemu Mzee Nyerere alikuwa ni mpenzi wa mchezo huu wa bao.

Licha ya mchezo wa bao kuwepo takriban Tanzania nzima, lakini mchezo huo Kusini umekuwa maarufu zaidi kwa kuwa kwanza inajulikana wachongaji mabao mazuri ya nakshi ni wamakonde, na kusini ndiyo kwao. Pili, mikete, miti ambayo hudondosha kokwa za kete zinazochezewa bao ipo mingi Kusini.

Kwanini nimelikumbuka bao? Bao Lina mitago na mahesabu ya hali ya juu sana kwa wenye kulijuwa kulicheza vizuri, wanaweza kumtega mtu mpaka mizunguko mitano ijayo na kila mzunguko aliyetegwa atakuwa anahisi anashinda tu lakini ndiyo anazidi kumtengenezea njia ya ushindi aliyemtega.

CCM siku za nyuma kidogo imepokea wapinzani wengi sana waliotokea vyama vya upinzani kutoka kada mbali mbali, kuanzia washabiki na wanachama wa kawaida, wenyeviti wa serikali za mitaa, madiwani, wabunge na wengi wengine.

Jee, huu siyo mtego wa upinzani kupandikiza mapandikizi ya kuja kuisambaratisha CCM? Jee, CCM imetegwa ikategeka? CCM tunachezewa "chess" au bao?

Upinzani wa Tanzania unaweza kuwa na vichwa na mahesabu na mitago ya kisiasa kama mahesabu na mitego ya mabingwa wa bao kama Mzee Nyerere, vya kuweza kutega mizunguko mitano ijayo?

Ni tafakuri tu ya FaizaFoxy.
 
Si kweli. Ingekuwa hivyo tusingeona wenyeviti wa serikali za mitaa, vijiji, madiwani na wabunge wa upinzani. CCM ni chama cha kupigiwa mfano duniani.
Hata muuaji mwenye leseni hawezi kuua wote akawamaliza, wako watakaobakia. Hata saa mbovu iliyosimama, mara mbili kutwa husema kweli. Eti CCM ni chama cha kupigiwa mfano duniani...kwa lipi? Kwa kutamalaki mataahira? Utakuwa umeshiba ubwabwa wewe!
 
Hata muuaji mwenye leseni hawezi kuua wote akawaliza, wako watakaobakia. Hata saa mbovu iliyosimama, mara mbili kutwa husema kweli. Eti CCM ni chama cha kupigiwa mfano duniani...kwa lipi? Kwa kutamalaki mataahira? Utakuwa umeshiba ubwabwa wewe!
Aiseeee
 
Bibi kizee naye kaamka kutoka kwenye usingizi wa pono wa kijani kibichi ,si alikuwa anafikiri ccm haikosei inapatia kila kitu hasa chini ya uongozi wa malaika mkuu .
 
Back
Top Bottom