I wish 'Wapinzani' wangekuwa na uwezo wa kupanga mbinu kama hizo.
Hao unaowaona wakihama vyama vyao na kukimbilia 'CCM' ni baada ya kuona 'ulaji' waliokuwa wameandaliwa huko wanakopokelewa. Hakuna la zaidi ya hapo.
Akina Mkumbo, 'Tumbili', Mama Mgwai, na hasa watu kama Dr Mihogo walipojazwa matumbo, ni wachache tu walioko huko ndani ya upinzania ambao hawakutamani na wao wajaribu bahati yao.
Kwa hiyo, maoni yangu ni kwamba, wengi wa hao,kama sio wote waliohamia CCM kutoka upinzani ni watafuta fursa.
Napenda kuwekea uzito hoja yangu hii kwa tafakuri.
Kati ya hao waliohama, kuna mwanachama yeyote aliyezungumzia sababu yake ya kuhama iliyojikita kwenye imani yake katika jambo lolote mbali ya "kumuunga mkono Mwenyekiti?" Kuna yeyote aliyeelezea kwa kina 'sera' mpya zilizoibuliwa CCM kwamba ndizo zilizomfanya avutiwe nazo?
Hawa hawana chochote wanachokiamini katika siasa zao, bali kujaza matumbo yao.
Lawama kwa vyama vya upinzani - hawana tofauti kubwa na CCM, kwa sababu hawawaandai, na kuwapika wanachama wao wakaamini wanchokisimamia, mbali ya kuwaondoa CCM ili na wao wapate fursa ya kwenda kula!
(Itanibidi hapa niungame - hata kwa kujua hili, leo hii pakitokea uchaguzi nitawapigia wapinzani licha ya madhaifu yao). Sababu za kufanya hivyo ninazo, lakini huo ni mjadala mwingine.
Mh Lowassa alipohama CCM, hakuhama kwa sabau ya sera nzuri alizoziona huko kwenye vyama vya upinzani. Amerudi CCM, sio kwa sababu CCM sasa hivi ina sera nzuri zaidi ya zile alizokimbia wakati ule. Kama huyu mzee aliweza kufanya hivyo, hawa maskini wenye njaa wataacha kwenda kuliko na neema?
Nimalize habari hii, imekuwa ndefu: tuombe patokee muujiza Tanzania, 2020 (ndio utakuwa ni muujiza, kwa sababu haitegemewi itokee vyama vya upinzani washinde, kwa haki au kwa maguvu) Njaa itahamia CCM. Sijui tunaowaona leo hii wakijibaraguza huko watafanya sarakasi zipi ili wawe ndani ya (upinzani) ambao sasa ndio watakuwa wanagawia wenye matumbo yao shibe.