Narudia tena, ilani ya viwanda ni ya ccm, na viwanda vinalipa kuliko udiwani, ubunge na urais. Kwakuwa wanaccm huwa tunaona wanafanya lolote kuhakikisha wanapata madaraka, kwanini wasikope bila riba wafungue hivyo viwanda kisha tuone matokeo ya wanachoamini?
Tena kwa kuanzia mawaziri wajiunge wanne wanne kila kundi lianzishe kiwanda watoe ajira tuone matokeo. Na funga kazi rais ajiunge na mawaziri watatu wa viwanda, wawili aliowatumbua na huyu mpya wajenge kiwanda kisha tuone mfano halisi wa hicho wanachohubiri. Akina Mo, Bakhresa and the likes hawahitaji ushauri wako kwenye viwanda maana tayari wanavyo, hawa wanaohubiri sasa ndio watoe shamba darasa la mahubiri yao.