Tafakuri ya FaizaFoxy 2: Korosho

Jiwe si alisema hashauriwi?umeongea point sana,lkn ccm hawashauriki.pesa ya kurudia uchaguzi ingetosha kujenga viwanda had vi 4.wakiondoka yatawezekana
 
Hiyo "mkinishauri" umeongezea wewe.

Asichotaka ni kupangiwa lakini ushauri anaupokea, sana tena.
Keshakwambia haitaji vipost posti vyenu wala hajali, clip ipo you tube angalia. So he doesn’t give a f ..... about what you posting.
 
Mengine yote nakubaliana na wewe lakini Ushirika kwa maana ya vyama vya ushirika siyo suluhisho. Vyama vya ushirika ndiyo chanzo kikuu kilichoitoa nchi hii kutoka msafirishaji wa kwanza wa mazao nje wa Afrika hadi kufikia omba omba wa kwanza.

Ushirika kama kampuni, Bakhresa na MO ni mfano mzuri nimeweka juu hapo. Hiyo ndiyo solution.

Kuhusu teknolojia, hilo si tatizo kubwa sana ingawa tunalo. Makampuni binafsi yana njia zao za ki intelijensia binafsi za kutatua hayo, yatapopewa fursa yataweza tu.
Kama kawaida ya tabia yetu ilivyo. Tunapenda tu kupapasa papasa tatizo na hatutaki au hatuna uwezo wa kulitatua. Nimekupa mfano wa KCC hapo bado hutaki kuuona kwa vile ulishapofushwa na"Vyama vya ushirika ndiyo chanzo kikuu kilichotoa nchi kutoka msafirishaji wa kwanza wa mazao nje wa Afrika hadi kufikia omba omba wa kwanza", bila ya kuangalia yaliyochangia hali hiyo.

Na kwa nini tuendelee kuutazama 'ushirika' katika mrengo huo na usiwe ushirika unaofanya kazi ipasavyo kwa kwa vile tumeerevuka zaidi wakati huu kuliko wakati ule! Sizungumzii ushirika ulioundwa na serikali, huu ni ushirika wa wakulima wenye mali zao.
Bakresa na Mo hawajazuiwa kufanya kazi hiyo, lakini hawajaonyesha nia ya kuifanya kwa sababu zao wanazojua wenyewe. Wakulima waendelee kupata hasara wakisubiri ushirika wa watu wengine?
 
Hayo uyasemayo ndiyo sababu kuu ya mimi kuandika waachiwe wafanya biashara wakubwa wafanye biashara hizo na si serikali. Isome vizuri post namba moja.
Mku ni kweli.
Ila swali linakuja pale mkwamo wa maisha uliopo kwani kama mzunguko wa fedha mifukoni kwa RAIA haitasaidi sana kujikwamua ili kufikia lengo
 
Well then, umeeleweka mkuu. Zao la korosho kama yalivyo mazao muhimu ya biashara linahitaji mjadala mpana hasa kipindi hiki ambapo serikali "imechafua" utaratibu.. mawazo ya wanazuoni kama wewe na ukiwa mdau wa korosho ni muhimu ili kusaidia nini kifanyike katika kuendeleza zao hilo na utafutaji wa masoko etc. Huenda analysis yako ingesaidia wakulima kadhaa huku mtwara..(who knows?)
Mku sio zao la korosho tuu kumbuka kahawa nayo ili kuwa inaingiza fedha nyingi za kigeni lakini mwisho wake kahawa Uchagani waliing'oa na kuamua kuotesha migomba na mazao mengine ya muda mfupi ili mambo yaende lakini uchagani ya kipindi wanalima kahawa ni tofauti kimaisha kwani walingizwa kwenye umaskini.
Mpaka kahawa inafikia hapo ilipo kwa Moshi ni siasa ndizo zilizoadhiri hili Kilimo kwani Mrema kupitia kahawa uchagani au ile mikoa yote inayolima kahawa alikubalika sana kwani aliitafutia soko ambalo wakulima waliuza ktk bei ambayo hawakuwahi kulipwa tangu enzi hizo na hili mikoa Mrema alionekana tishio kukuu.
Mahali Mrema alionekana tishio ni pale alipoenda kumkabidhi Thomas Ngawai Jimbo la Ubunge Moshi Vijijini na yy Mrema akaenda kugombea Ubunge Temeke na haya majimbo yote Mrema alishinda kwa kishindo kikuu.
Kilichofuata ikaonekana huyu jamaa kahawa ndiyo imemfisha hapa alipo mwisho kilichotokea baadhi ya Dawa zilionekana zinaleta ugonjwa Kansa kwa hiyo Dawa zikapigwa marufuku na mpaka Leo haikupatikana Dawa mbadala ya hili zao kwa hiyo sio kwamba wachaga hawakumbuki wanalikumbuka vizuri kisa cha zao lao kufa mpaka leo ninaamini ipo siku wataamua kuacha siasa na kulifufua tena hili zao .
Kwa hiyo siasa zinaadhiri maisha ya watu sana kama wanaoshiriki haya mambo hawataangalia madhara ya baadaye kabla ya kutenda.
 
Korosho lazima uifungamanishe na masoko ya kimataifa kwanza haswa na walioshika hilo soko, hilo la nani atakuwa na kiwanda ni la mwisho.
 
Ya mwaka huu atanunua nani? Ni sawa una watoto wawili,mmoja kafika umri wa kuanza shule halafu unamwambia kaa nyumbani eti utunze fedha za kumpeleka mdogo shule wakati hali ya mkubwa huijui.
Wakulima wa korosho waruhisiwe wauze korosho zao kwa bei elekezi. Wanaoumia ni wakulima.
Kwani ff anatafuta mnunuzi wa korosho zilizoko ghalani?!
 
Bibi bana sasa mi mbona sijagundua ushauri wala suluhisho lako??

Bibi hebu elezea vizuri tafadhali ...Je, sumu ni kitugani au tulikosea wapi na dawa ni nini ... Hizo longolongo za serekali iwakopeshe private sector sijui blaa blaaa ... Ni kituko cha sufuria ya Abunnuwas iliyo zaa sufuria nyingine ...
 
Bibi bana sasa mi mbona sijagundua ushauri wala suluhisho lako??

Bibi hebu elezea vizuri tafadhali ...Je, sumu ni kitugani au tulikosea wapi na dawa ni nini ... Hizo longolongo za serekali iwakopeshe private sector sijui blaa blaaa ... Ni kituko cha sufuria ya Abunnuwas iliyo zaa sufuria nyingine ...
Soma post namba moja kuanzia para ya tano.
 
Serikali haina sababu ye kuwakopesha wafanyabiashara wakubwa maana wameona fursa wamepuuza, nakumbuka kuna wakati rais alimpa ofa ya ardhi ya bure Bahresa kama atakuwa tayari kulima miwa na kufungua kiwanda cha sukari hakujibiwa mpaka leo kimya, serikali ifungue viwanda vya kubangua korosho, wanajeshi wapo wanaweza kuendesha hivyo viwanda vizuri tu badala ya kuwatumia kukusanya na kuweka maghalani.
 
Serikali haina sababu ye kuwakopesha wafanyabiashara wakubwa maana wameona fursa wamepuuza, nakumbuka kuna wakati rais alimpa ofa ya ardhi ya bure Bahresa kama atakuwa tayari kulima miwa na kufungua kiwanda cha sukari hakujibiwa mpaka leo kimya, serikali ifungue viwanda vya kubangua korosho, wanajeshi wapo wanaweza kuendesha hivyo viwanda vizuri tu badala ya kuwatumia kukusanya na kuweka maghalani.
Uko wapi wewe? Duniani? Bakhresa si wa longolongo, ni kazi tu...




 
Zao la korosho limepata wanunuzi lakini ushauri wangu uko palepale. Tuiongezee thamani korosho.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom