Tafakuri ya FaizaFoxy 2: Korosho

Tafakuri ya FaizaFoxy 2: Korosho

Usemayo ni mawazo duni sana. Mbona kuna Watanzania wengi sana wamefanikiwa? Bakhresa ni mfano mzuri sana, alikuwa ana kiduka tu cha kushona makubadhi pale mtaa wa Uhuru.

Kila unapoona matatizo ufahamu kuwa kuna fursa, nnakushangaa sana wewe unashindwa kuziona fursa na unayaona makaburi tu.
UMEMTAJA BAKHRESSA INAMAANA KTK UKOO WENU HAKUNA HATA MMOJA WA KUMTOLEA MFANO, HII INAONYESHA KTK UKOO MZIMA HAKUNA ALETUSUA NA WEWE UKIWAMO, HII INANIKUMBUSHA SHULE FLANI AMBAPO WANAOFANYA MTIHANI NI 100 LAKINI WANAOFAULU VIZURI NI WANNE JE UTASEMA WALOBAKI NI WAZEMBE? MBONA ZIPO SHULE WANAOPIGA PEPA NI 100 NA WANAOFAULU NI 90 INAMAANA KUNA MAZINGIRA BORA YA KILA MTU KUFANYA VYEMA
 
Wamelipwa???

😀 😀 😀 ikifika zamu ya dhalimu kupitia haki yako utapanua kinywa kuliko anayeng'olewa gego. Watu hawajalipwa na waliolipwa hawajalipwa kiasi ulichokitaja HONGERENI.
Endelea na siasa ila pembe la ng'ombe halifichiki!!!
Siku zote masufahaa hujiita werevu halinishangazi.
Ukisoma post namba moja utaelewa kuwa Mimi ni mdau wa korosho. Ndiyo nimelipwa tena nashukuru, vizuri kuliko nilivyotarajia. Hakukuwa na makato Safari hii. Mungu atupe nini zaidi?

Anaekubali kudhulumiwa ni baradhuli.

Umewahi kuwa mdau wa korosho au upo hapa kupinga tu kijingajinga?
 
Ni ushauri mzuri hata hivyo korosho ya msimu ujao imeshapata mnunuzi na benki ya Mkombozi imeshatenga kiasi cha sh trilioni 1 kwa ajili ya zoezi hilo.

Ahsante kwa ushauri!
Hapana mkombozi nibenki ya wakristo na korosho inalimwa sana na waislam pengine benki ya waislam ingefaa zaidi (....bifaiza Hugo kimoyomoyo).
Soko la korosho limedorora kidunia maana uzalishaji umezidi kwa wenzetu wanaojua kulima kiuhakika, hata ivorycoast wanahangaika hawajui wafanyaje. Hakuna cha Bahresa wala Mo hapa wadau wote wa korosho waliokuwa wanaiuza wakalishwe chini waungane waone namna ya kuanzisha viwanda na serikali iwatizame kuhusu kodi,waitengenezea soko korosho wakianza na landani (korosho zakula moja kwa moja) na za nje kulingana na uhitaji. Lazima wabunge na mawaziri waungane na wataalamu waache siasa uchwara kwenye hili na mengine kama haya
 
Hivi yule dada wa nyumbani kwako aliyekuwa anampenda Magu mpaka akawa anajishaua bibi bibi hatujawahi pata rais kama huyu bado unaye au ndo ushamtumbua

Samahani kwa kutoka nje ya mada maana mimi ata mkorosho sijawahi kuuona mimi najua mibuni ya kahawa ambayo ma ccm yaliua basi tena kila mtu apambane kivyake

Samahani bibi kwa kutoka nje ya mada
I expected more
 
Tatizo lako kubwa ni muono duni na kukosa ubunifu. Utajiendeleza kwa kuendelea kuuza korosho ghafi?

Kujiendekeza ndiyo huko. Soma post namba moja ikuingie.
Ukishaiomba serikali ikopeshe bila riba ili kijengwe kiwanda ina maana tayari kuna chaos! Hilo umeliomba mwenyewe! Huoni tayari kuna shida mahali?
 
KUNA WATU WAPUUZI SANA YAANI UKIZUNGUMZIA WATU HAWAFANIKIWI HAPA TZ KUTOKANA NA MAZINGIRA MABOVU NA SERA ZA ZISIZORAFIKI WATU KUTUSUA UTASIKIA MTU ANAKUTAJIA MENGI, BAKHRESA, MO LAKINI HATAJI HATA MTU MMOJA WA UKOO WAKE AU KABILA LAKE AU JIRANI YAKE ALEFANIKIWA, SWALI JE INAMAANA UKOO MZIMA HAWAHANGAIKI KUTAFUTA MAPENE? JE UKOO MZIMA NI MBUMBUMBU WA MAISHA JIBU JEPESI NI KWAMBA WATU WANHANGAIKA KADRI WAWEZAVYO TATIZO HAKUNA MAZINGIRA RAFIKI YA WATU KUTUSUA UKIFIKIA LEVEL FLANI VIKWAZO LUKUKI
 
Ukisoma post namba moja utaelewa kuwa Mimi ni mdau wa korosho. Ndiyo nimelipwa tend nashukuru, vizuri kuliko nilivyotarajia. Hakukuwa na makato Safari hii. Mungu atupe nini zaidi?

Anaekubali kudhulumiwa ni baradhuli.

Umewahi kuwa mdau wa korosho au upo hapa kupinga tu kijingajinga?
Wewe lazima ulipwe sababu ni kibaraka wao huko kusini......kumbe hadi wewe una unafiki wa kujikombakomba!! Duh
 
IFIKE HATUA KAMA KWELI WATU WANAONA TZ KUNA FURSA NZUURI YA KUTENGENEZA FEDHA BASI KILA MTU ATAJE MTU MMOJA KWENYE UKOO WAKE AU FAMILIA YAKE AU YEYE MWENYEWE ATUAMBIE AMEFANIKIWA KIASI GANI ILI NASI TUPATE MWANGA NA SIO KUTUTAJI AKINA MENGI, MO NA BAKHRESA
 
Jifikirie unaeshindwa kwa kura na CCM kila kukicha, lazima utakuwa ni mama la ujinga.
Mpo madarakani zaidi ya nusu karne... hamkuyajua? Hamkupata kuwa na viwanda? Kwanini mlifeli? Hamjiulizi mnakurupuka tena na viwanda!!!
Haviki kama uyoga... sera ziwe rafiki kwanza... kuanziaha ama kumiliki kiwanda si kama kumiliki mdomo ambap kila mtu anao NI MIPANGO MIKUBWA VIWANDA HAVIKURUPUKIWI
 
Hao akina Bakhressa hawakopi wakafungie viwanda vya kusaka political millage, wanakopa na kufungua viwanda vinavyolipa. ......................................................................Sio ushauri akina Mo wakope kufungua viwanda, halafu nyie muue, mloge, mtoe rushwa kuhakikisha mnapata madaraka.
Umesahau point moja muhimu, ya kuwaletea 'Wazungu wanaoongea lugha za Kusini mwa Afrika' kuja kuwateka na kuwadhalilisha na baadaye kumpeleka mahakamani teksi dreva 'Mtanzania' asiyezungumza lugha za Kusini mwa Afruka!
 
Usemayo ni mawazo duni sana. Mbona kuna Watanzania wengi sana wamefanikiwa? Bakhresa ni mfano mzuri sana, alikuwa ana kiduka tu cha kushona makubadhi pale mtaa wa Uhuru.

Kila unapoona matatizo ufahamu kuwa kuna fursa, nnakushangaa sana wewe unashindwa kuziona fursa na unayaona makaburi tu.
mzee Tz hakuna fursa yoyote chini ya ccm ni usenge mtupu ikiwa dangote kashindwa kwa kweli mafanikiyo ya baharesa ni miujiza tu kuweza kufanikiwa nchini ya CCM
 
Mku kwa hali ilivyo hatawakitokea ikaisaidi sects binafsi hakuna unafuu wowote kwani RAIA fedha za kununua hizi bidhaa zitakazozalishwa.
Watazalisha then watabaki na bidhaa kwenye mastoo mpaka muda wa matumizi utaisha mwisho wanapeka dampo baada ya kukosa wanunuzi.
Mzunguko ukirudi kila kitu kitawezekana kabisa shida fedha hakuna

Korosho zikishakuwa packed huwa naona zinauzwa kuanzia buku mpk 10,000 na zaidi ya hapo kwa idadi ya kilo utakazohitaji. kwa soko la ndani Raia wanaweza kununua.

Mi nadhani hoja ya bibi ni ya msingi sana kuhakikisha serikali kwa sasa inatenga au kuwezesha upatikanaji wa hata Trilion 2 (my estimate) kuhakikisha hawa wenye uzoefu na processing industries kama Bakhresa, MO na Kina ASAS wanapewa mikopo isiyokuwa na riba kama mitaji ya kufungua viwanda vitakavyokuwa na tija katika cashewnut products.

Lengo kuu kama anavyosema bibi ni ku add value;

Hii itawezesha mambo mengi sana ikiwamo ;

1. soko la ndani- kurahisisha uuzwaji wa korosho kutoka kwa wakulima kuja kwenye viwanda husika na processing direct au hata kwa vyama vilivyopo vya ushirika.

2. Wenye viwanda wana experience na soko la nje na mahitaji ya soko, kuanzia ktk quality ya processed cashews, packaging, na au hata wakiamua kuuza un processed based na mahitaji.

3. Processing hizo cashewnut hapa hapa na kuzi export ni faida kubwa kwa uchumi wetu. Ajira zitaongezeka

4. Importing processed cashewnut afterwards iwe discouraged kwa kutumia hizo fiscal measures
 
Shukran Fayza kwa uzi mzuri
Korosho kama korosho sio tatizo, ni dalili ya matatizo makubwa kwa Wakulima mbali mbali wa mazao yanayoitwa ya biashara ingawa siku hizi hakuna mazao ya biashara na yasiyo ya biashara kila zao ni la biashara
Juzi nimemaliza kusoma kitabu cha Dr. Mengi bahati nzuri ameonyesha jinsi gani yeye mwenyewe alivyonufaika na chama cha Ushirika cha wakulima wa kahawa Kilimanjaro. Sisi wenyewe ni mashahidi kwa upande wa previous generation jinsi gani baadhi ya wazee wetu hivyo vyama vilivyosaidia jamii husika hasa katika mikoa ile ambayo ilikuwa na mazao ya biashara
Dr. Mengi ameonyesha jinsi gani hivi vyama ilikuwa threats kwa wanasiasa ambao walikuwa na wasiwasi kwamba kama Waafrika wangeshiba na kuelimika jinsi gani ingekuwa vigumu kuwaburuza kisiasa
Hilo wazo lako ulilolitoa kuna maelfu ya watu washalitoa na sio kwa korosho tu. Tatizo kubwa ni mseto wa maamuzi ya kiuchumi yanayofanywa kisiasa, chunguza sana hilo utaliona kwenye Karafuu, Kahawa, Pamba na mengineyo. Dr Mengi ameonyesha jinsi gani Tz kuwa siyo masikini bali Watanzania ndio maskini kwa mfano kuna sehemu anasema


"Studies show that the Ruvu Basin can feed the other EA countries, the Kilombero area can feed the whole of Central Africa with rice, Kyela district can produce enough rice to feed the whole of West Africa, the Rufiji Basin can feed North Africa including the Sudan, Ethiopia and Somalia, and Wami and Arusha Chini areas can produce enough rice to feed the whole of Southern Africa. In other words, Tanzania has adequate arable land and water to produce enough food to feed the whole of Africa"
I can, I must, I will
Reginald Abraham Mengi

Yaani kwa kifupi katika haya mabonde ambayo tunayo Tanzania tunaweza kuilisha Africa nzima

Previous week nimeona clip moja kijana mmoja wa UAE anaulizwa na Mwandishi wa Habari mwenye asili ya Nigeria kwanini nchi yao imepiga hatua kiasi kikubwa kiuchumi. Alitoa jibu moja tu ==> Leadership
Akaeleza jinsi gani Nigeria ilivyoanza kugundua mafuta kwanza miaka 10 kabla ya UAE na jinsi gani Nigeria ilivyo na resources nyingine nyiingi ukilinganisha na UAE l

Tuwaachie wachumi, wataalamu wa vyama vya ushirika, wadau wa kilimo na Wanasiasa wafanye maamuzi ya kilimo kwa pamoja. Wala wasiachiwe wanasiasa peke yao watatufikisha hapa tulipo

Natokea ktk mkoa mmojawapo unaozalisha Kahawa, tokea miaka ya 1970s mpaka sasa ni mazungumzo ya kawaida /household talk kusikia wazee wakizungumzia mikasa ya jamaa mbalimbali kule kijijini jinsi gani wanavyohangaika kuivusha kahawa nchi jirani ambako kunasemekana kuna bei nzuri zaidi kuliko wakiuza kwetu. Najaribu kupima
* Ujasiri wa Kuivusha kahawa
* Gharama za Kuivusha
Bado inapatikana bei nzuri zaidi kuliko kwanini ?
* Jee hao nchi jirani si wanaipitisha kwenye Bandari yetu. Then kwanini wao wana bei kubwa kuliko sisi
Mbona hata wanasiasa hata wa upinzani hatuwasikii kuzungumzia hili ??

Hayo utayaona kwenye Mazao yote hapa kwetu Tanzania

In other words, Tanzania has adequate arable land and water to produce enough food to feed the whole of Africa"


I can, I must, I will
Reginald Abraham Mengi

Yaani kwa kifupi katika haya mabonde ambayo tunayo Tanzania tunaweza kuilisha Africa nzima


The country has been engaged in the production of the cash crop since before independence in the years 1960s,

however, poor regulation and lack of reliable payments to farmers have posed significant challenges to the Cashew Nut farming industry in Tanzania.

Guinea-Bissau, a country a tenth of the area of Tanzania's, has a significantly greater yield.

More than ninety percent of the exports are destined for India and almost entirely in raw form.

The lack of domestic processing firms costs the country vital foreign revenues and thousands of jobs.

The Tanzanian government has been facing challenges for finding potential investors in order to revive the cashew processing industry in Tanzania.

(Wikipedia)
 
"Se non sta andando bene, chiama tua nonna." Hiyo ni methali maarufu ya Kitaliano ambayo nimepata tabu kidogo kutafuta ya Kiswahili inayofanana-nayo, sijafanikiwa kuipata. Kwa tafsiri isiyo rasmi inasema "ikiwa hakuna linalokwenda sawa, muone bibi".

Nafahamu Kitanzania ukisema "kumuona bibi" au "babu" wengi wengine huhusisha na kuwaona mabibi na mababu ili waongee na mizimu mambo yaende sawa. Wataliano kwa msemo wao huo hawamaanishi kama Watanzania, Wataliano wanamaanisha umuone bibi kwa hekima na busara zake. Labda niifananishe na methali yetu ya "uzee ni dawa".

Binafsi kama bibi, leo nimedhamiria kutoa tafakuri yangu kwenye zao la korosho na ufumbuzi wa "matatizo" ya zao hilo.

Kwanza napenda ku "declare interest" kuwa binafsi ni mdau wa korosho kwa kuwa na mikorosho, mingi tu, tiliyoirithi toka mashamba ya mabibi zetu ile mbegu ya asili ya kizamani mpaka tumejaribu kuiendeleza na kupanda ya kisasa na tunaliona tija nzuri tu.

Ushauri: Serikali ijitowe kimasomaso kuwakopesha bila riba wafanya biashara wakubwa wenye uzoefu wa viwanda kama vile akina Bakhresa na Mo kufunguwa viwanda vikubwa vya kisasa vya kubangua, kusindika na kufungasha korosho kwa kiwango cha Kimataifa na kuwasaidia kushindana na masoko ya Kimataifa.

Hiyo ni badala ya serikali kuingilia zao hilo.

Sababu kuu ni kuwa wafanya biashara hao tayari wana uzoefu mpana wa viwanda vya "food processing" na tayari wana mitaji katika nchi kadhaa za SADC na Afrika Mashariki.

Ni tafakuri tu ya FaizaFoxy .
Katiba ya Jamhuri ya Muungano inayoongozwa na chama cha Ccm inasema Rais halazimiki kufata ushauri wa mtu yeyote,hata FaizaFoxy
 
IFIKE HATUA KAMA KWELI WATU WANAONA TZ KUNA FURSA NZUURI YA KUTENGENEZA FEDHA BASI KILA MTU ATAJE MTU MMOJA KWENYE UKOO WAKE AU FAMILIA YAKE AU YEYE MWENYEWE ATUAMBIE AMEFANIKIWA KIASI GANI ILI NASI TUPATE MWANGA NA SIO KUTUTAJI AKINA MENGI, MO NA BAKHRESA
NDANI YA FISIEMU UBUNIFU WA FURSA ULISHAPOTEA WAMEBAKI KUKARIRI... NDANI YA FISIEMU UWEZESHAJI UMEBAKI KWENYE MATABAKA SI UWEZO.
MIJADALA MINGI KUHUSU UBORESHAJI MAZAO NA MALIGHAFI ILISHAFANYIKA HAKUNA KILICHOFUATA ZAIDI YA MAKARATASI KUTUNZWA...
 
Ukisoma post namba moja utaelewa kuwa Mimi ni mdau wa korosho. Ndiyo nimelipwa tend nashukuru, vizuri kuliko nilivyotarajia. Hakukuwa na makato Safari hii. Mungu atupe nini zaidi?

Anaekubali kudhulumiwa ni baradhuli.

Umewahi kuwa mdau wa korosho au upo hapa kupinga tu kijingajinga?

We mama muogope Mungu
Sogea tu hapo Mkuranga,Kibiti,Ikwilili halafu uongee hizo kauli zako za dharau juu ya wasiolipwa pesa zao uone kama utabaki salama.
Watu hawajui hatima ya mashamba,sio palizi sio dawa vyote ni mtihani kwao na muda ndio huu umewadia.
Unapotetea jambo liweke katika muktadha wa dini na upime kama walichofanyiwa wakulima wa korosho ni haki au batili.
 
IFIKE HATUA KAMA KWELI WATU WANAONA TZ KUNA FURSA NZUURI YA KUTENGENEZA FEDHA BASI KILA MTU ATAJE MTU MMOJA KWENYE UKOO WAKE AU FAMILIA YAKE AU YEYE MWENYEWE ATUAMBIE AMEFANIKIWA KIASI GANI ILI NASI TUPATE MWANGA NA SIO KUTUTAJI AKINA MENGI, MO NA BAKHRESA
NDANI YA FISIEMU UBUNIFU WA FURSA ULISHAPOTEA WAMEBAKI KUKARIRI... NDANI YA FISIEMU UWEZESHAJI UMEBAKI KWENYE MATABAKA SI UWEZO.
MIJADALA MINGI KUHrUSU UBORESHAJI MAZAO NA MALIGHAFI ILISHAFANYIKA HAKUNA KILICHOFUATA ZAIDI YA MAKARATASI KUTUNZWA...
 
We mama muogope Mungu
Sogea tu hapo Mkuranga,Kibiti,Ikwilili halafu uongee hizo kauli zako za dharau juu ya wasiolipwa pesa zao uone kama utabaki salama.
Watu hawajui hatima ya mashamba,sio palizi sio dawa vyote ni mtihani kwao na muda ndio huu umewadia.
Unapotetea jambo liweke katika muktadha wa dini na upime kama walichofanyiwa wakulima wa korosho ni haki au batili.
Ni mjinga huyu,anashabikia ccm kuliko maslahi ya taifa,don't waste your time kwa buku saba kama faiza
 
Back
Top Bottom