Tafakuri ya FaizaFoxy 2: Korosho

FaizaFoxy

Platinum Member
Apr 13, 2011
92,147
107,669
"Se non sta andando bene, chiama tua nonna." Hiyo ni methali maarufu ya Kitaliano ambayo nimepata tabu kidogo kutafuta ya Kiswahili inayofanana-nayo, sijafanikiwa kuipata. Kwa tafsiri isiyo rasmi inasema "ikiwa hakuna linalokwenda sawa, muone bibi".

Nafahamu Kitanzania ukisema "kumuona bibi" au "babu" wengi wengine huhusisha na kuwaona mabibi na mababu ili waongee na mizimu mambo yaende sawa. Wataliano kwa msemo wao huo hawamaanishi kama Watanzania, Wataliano wanamaanisha umuone bibi kwa hekima na busara zake. Labda niifananishe na methali yetu ya "uzee ni dawa".

Binafsi kama bibi, leo nimedhamiria kutoa tafakuri yangu kwenye zao la korosho na ufumbuzi wa "matatizo" ya zao hilo.

Kwanza napenda ku "declare interest" kuwa binafsi ni mdau wa korosho kwa kuwa na mikorosho, mingi tu, tiliyoirithi toka mashamba ya mabibi zetu ile mbegu ya asili ya kizamani mpaka tumejaribu kuiendeleza na kupanda ya kisasa na tunaliona tija nzuri tu.

Ushauri: Serikali ijitowe kimasomaso kuwakopesha bila riba wafanya biashara wakubwa wenye uzoefu wa viwanda kama vile akina Bakhresa na Mo kufunguwa viwanda vikubwa vya kisasa vya kubangua, kusindika na kufungasha korosho kwa kiwango cha Kimataifa na kuwasaidia kushindana na masoko ya Kimataifa.

Hiyo ni badala ya serikali kuingilia zao hilo.

Sababu kuu ni kuwa wafanya biashara hao tayari wana uzoefu mpana wa viwanda vya "food processing" na tayari wana mitaji katika nchi kadhaa za SADC na Afrika Mashariki.

Ni tafakuri tu ya FaizaFoxy .
 
Viatu vimempwaya mr john
Mr%20Paul%2020190603_133218.jpeg
 
Pole bibi, hakuna ushauri ambao haujawahi kutolewa kwa nchi hii toka uhuru ila jambo zuri huwa tunapokea ushauri kama hauna faida kwa chama chetu CCM tunaweka jalalani..

Siri kubwa iliyojificha ndani ya CCM na ni ngumu kuwekwa wazi ni hii, CCM haihitaji watanzania walio wengi wafanikiwe kimaisha maana mafanikio kimaisha ndio chanzo cha kujitambua na watu kujitambua ndio kaburi la CCM..
 
Kweli kabisa viongozi wateuliwa awamu ya tano wamefanya mlolongo wa maamuzi yasiyo na tija kwa ki-Spaniola tuna kausemi : Estar como una cabra.

Ushauri wako FaizaFoxy, wauzingatie maana wameshafanya maamuzi mengi yanayoligharimu taifa kiuchumi na kijamii na sasa hali ni mbaya sana.
 
Mtoa mada upo sawa, serikali inabidi itoe support sector binafsi. Risk ni nyingi katika Biashara. Ilifanyika dhambi kuwabeza sector binafsi sakata la Korosho. Waombwe radhi tufungue ukurasa mpya. Wengi wenu kijani mlifisia sana maamuzi yale ya dharula yasiyo na tija.
 
Pole bibi, hakuna ushauri ambao haujawahi kutolewa kwa nchi hii toka uhuru ila jambo zuri huwa tunapokea ushauri kama hauna faida kwa chama chetu CCM tunaweka jalalani..

Siri kubwa iliyojificha ndani ya CCM na ni ngumu kuwekwa wazi ni hii, CCM haihitaji watanzania walio wengi wafanikiwe kimaisha maana mafanikio kimaisha ndio chanzo cha kujitambua na watu kujitambua ndio kaburi la CCM..
Usemayo ni mawazo duni sana. Mbona kuna Watanzania wengi sana wamefanikiwa? Bakhresa ni mfano mzuri sana, alikuwa ana kiduka tu cha kushona makubadhi pale mtaa wa Uhuru.

Kila unapoona matatizo ufahamu kuwa kuna fursa, nnakushangaa sana wewe unashindwa kuziona fursa na unayaona makaburi tu.
 
Hao akina Bakhressa hawakopi wakafungie viwanda vya kusaka political millage, wanakopa na kufungua viwanda vinavyolipa. Mimi niliwahi kushauri kwakuwa sera ya viwanda ni ilani ya ccm, basi ccm waanze kuwa mfano, wao kuanzia rais na mawaziri wakope na kufungua viwanda kisha wazalishe, tukishaona mfano toka kwao tutavutika.

Maana wanaccm huwa tunawaona kwenye chaguzi kuanzia rais, wabunge na mawaziri wakitumia nguvu zao zote na kusaidiwa na vyombo vya dola kuhakikisha hawapotezi madaraka. Nguvu hizo hizo wazitumie kufungua viwanda tuone ubora wao maana viwanda vinalipa kuliko urais, uwaziri, ubunge nk. Sio ushauri akina Mo wakope kufungua viwanda, halafu nyie muue, mloge, mtoe rushwa kuhakikisha mnapata madaraka.
 
Kweli kabisa viongozi wateuliwa awamu ya tano wamefanya mlolongo wa maamuzi yasiyo na tija kwa ki-Spaniola tuna kausemi : Estar como una cabra.

Ushauri wako FaizaFoxy, wauzingatie maana wameshafanya maamuzi mengi yanayoligharimu taifa kiuchumi na kijamii na sasa hali ni mbaya sana.
Juzi Mheshimiwa Rais amesema wanaoona hali ngumu ni wale waliozowea pesa zisizo halali.
 
Hao akina Bakhressa hawakopi wakafungie viwanda vya kusaka political millage, wanakopa na kufungua viwanda vinavyolipa. Mimi niliwahi kushauri kwakuwa sera ya viwanda ni ilani ya ccm, basi ccm waanze kuwa mfano, wao kuanzia rais na mawaziri wakope na kufungua viwanda kisha wazalishe, tukishaona mfano toka kwao tutavutika.

Maana wanaccm huwa tunawaona kwenye chaguzi kuanzia rais, wabunge na mawaziri wakitumia nguvu zao zote na kusaidiwa na vyombo vya dola kuhakikisha hawapotezi madaraka. Nguvu hizo hizo wazitumie kufungua viwanda tuone ubora wao maana viwanda vinalipa kuliko urais, uwaziri, ubunge nk. Sio ushauri akina Mo wakope kufungua viwanda, halafu nyie muue, mloge, mtoe rushwa kuhakikisha mnapata madaraka.
Ndiyo maana nikasema wakopeshwe bila riba, ili wasitumie mitaji yao waliyopanga kufanya mengine.
 
Ni ushauri mzuri hata hivyo korosho ya msimu ujao imeshapata mnunuzi na benki ya Mkombozi imeshatenga kiasi cha sh trilioni 1 kwa ajili ya zoezi hilo.

Ahsante kwa ushauri!
Sawa, lakini tujielekeze kwenye ku add value ya zao hilo. Kwani japo wanunuzi wanachofanya ni kuibangua na kufungasha vizuri na kuiuza (processing). Serikali ilishindwa zamani mpaka viwanda vyake vikafa. Ni wakati muafaka wafanya biashara wazoefu wawezeshwe ili tu add value ya zao hilo.
 
47 Reactions
Reply
Back
Top Bottom