Tafakuri ya FaizaFoxy 2: Korosho

Tafakuri ya FaizaFoxy 2: Korosho

We mama muogope Mungu
Sogea tu hapo Mkuranga,Kibiti,Ikwilili halafu uongee hizo kauli zako za dharau juu ya wasiolipwa pesa zao uone kama utabaki salama.
Watu hawajui hatima ya mashamba,sio palizi sio dawa vyote ni mtihani kwao na muda ndio huu umewadia.
Unapotetea jambo liweke katika muktadha wa dini na upime kama walichofanyiwa wakulima wa korosho ni haki au batili.

= ikwiriri

Nisogee wakati nipo Mkuranga.
Unanshangaza.

Ambae hajalipwa Majaliwa kishatoa ufafanuzi. Pitia uzi vizuri kabla hujalalamika.

Soma hiyooo: http://mtanzania.co.tz/majaliwa-ahadi-wakulima-wa-korosho-kulipwa-kabla-ya-juni-30/amp/
 
Ni ushauri mzuri hata hivyo korosho ya msimu ujao imeshapata mnunuzi na benki ya Mkombozi imeshatenga kiasi cha sh trilioni 1 kwa ajili ya zoezi hilo.

Ahsante kwa ushauri!
Ya mwaka huu atanunua nani? Ni sawa una watoto wawili,mmoja kafika umri wa kuanza shule halafu unamwambia kaa nyumbani eti utunze fedha za kumpeleka mdogo shule wakati hali ya mkubwa huijui.
Wakulima wa korosho waruhisiwe wauze korosho zao kwa bei elekezi. Wanaoumia ni wakulima.
 
Kwanza kumbuka kuwa kwenye mazao yapo aina mbili kuu, mazao ya chakula na mazao ya biashara.

Korosho ni zao la biashara, biashara ya korosho soko lengwa ni la Kimataifa ili mpate fedha za kigeni.

Korosho iliyobanguliwa na kufungashwa vizuri ina soko kubwa sana duniani. Hilo halina shaka.

Ushindani wa kibiashara utakuwepo, fitna na majungu yatakuwepo lakini mwisho wa siku biashara itafanyika tu kwani demand ipo.
Mku kumbuka hiyo demand iliyopo kuna kuharibika pia.
Kuna kauli aliwahi kuitoa Babu yangu wa kitaifa na mwasisi wa chama changu Ccm Mwalimu Nyerere yakuwa Vikao vya kidunia vikifanyika huwa wanajadili hata Korosho ya Mzaramo huku Afrika kwa hiyo kujadili kwao ni kutupangia bei ya kuinunua hiyo korosho.
Kwa maana hiyo hizi kauli nyingi zilizotoka kwa watu wanaojiita Wazalendo za kuwakejeli hawa wanunuzi kuwaita Mabeberu tutegemee kuendelea kususiwa hili zao au kama ilivyokuwa Mbaazi ambayo nayo imekosa soko baada wanunuzi kulisusia.
Hizi kauli tunatakiwa kuwa nazo na kuzitoa kwa umakini mkubwa.
Sio kila kinachotoka kinywani kila Mtu atakikubali atakikubali baada kukifanyia uchambuzi tusitumie sana mihemko isiyosaidia mwisho inatupeleka kwenye mkwamo
 
IFIKE HATUA KAMA KWELI WATU WANAONA TZ KUNA FURSA NZUURI YA KUTENGENEZA FEDHA BASI KILA MTU ATAJE MTU MMOJA KWENYE UKOO WAKE AU FAMILIA YAKE AU YEYE MWENYEWE ATUAMBIE AMEFANIKIWA KIASI GANI ILI NASI TUPATE MWANGA NA SIO KUTUTAJI AKINA MENGI, MO NA BAKHRESA
Kila mtu ana haki ya fursa zilizopo. Tazama vizuri post namba moja uone sababu zilizowataja Bakhrea na MO, tena kwa kukujuza tu kuna neno "kama".

Kama umeziona fursa unangoja nini?
 
Mku kumbuka hiyo demand iliyopo kuna kuharibika pia.
Kuna kauli aliwahi kuitoa Babu yangu wa kitaifa na mwasisi wa chama changu Ccm Mwalimu Nyerere yakuwa Vikao vya kidunia vikifanyika huwa wanajadili hata Korosho ya Mzaramo huku Afrika kwa hiyo kujadili kwao ni kutupangia bei ya kuinunua hiyo korosho.
Kwa maana hiyo hizi kauli nyingi zilizotoka kwa watu wanaojiita Wazalendo za kuwakejeli hawa wanunuzi kuwaita Mabeberu tutegemee kuendelea kususiwa hili zao au kama ilivyokuwa Mbaazi ambayo nayo imekosa soko baada wanunuzi kulisusia.
Hizi kauli tunatakiwa kuwa nazo na kuzitoa kwa umakini mkubwa.
Sio kila kinachotoka kinywani kila Mtu atakikubali atakikubali baada kukifanyia uchambuzi tusitumie sana mihemko isiyosaidia mwisho inatupeleka kwenye mkwamo
Hayo uyasemayo ndiyo sababu kuu ya mimi kuandika waachiwe wafanya biashara wakubwa wafanye biashara hizo na si serikali. Isome vizuri post namba moja.
 
Ya mwaka huu atanunua nani? Ni sawa una watoto wawili,mmoja kafika umri wa kuanza shule halafu unamwambia kaa nyumbani eti utunze fedha za kumpeleka mdogo shule wakati hali ya mkubwa huijui.
Wakulima wa korosho waruhisiwe wauze korosho zao kwa bei elekezi. Wanaoumia ni wakulima.
Waumizwe zaidi ya korosho za kununuliwa kwa bei ndogo?

Ni wakati muafaka ushauri wa bibi ufatwe.
 
Hao akina Bakhressa hawakopi wakafungie viwanda vya kusaka political millage, wanakopa na kufungua viwanda vinavyolipa. Mimi niliwahi kushauri kwakuwa sera ya viwanda ni ilani ya ccm, basi ccm waanze kuwa mfano, wao kuanzia rais na mawaziri wakope na kufungua viwanda kisha wazalishe, tukishaona mfano toka kwao tutavutika.

Maana wanaccm huwa tunawaona kwenye chaguzi kuanzia rais, wabunge na mawaziri wakitumia nguvu zao zote na kusaidiwa na vyombo vya dola kuhakikisha hawapotezi madaraka. Nguvu hizo hizo wazitumie kufungua viwanda tuone ubora wao maana viwanda vinalipa kuliko urais, uwaziri, ubunge nk. Sio ushauri akina Mo wakope kufungua viwanda, halafu nyie muue, mloge, mtoe rushwa kuhakikisha mnapata madaraka.

Kuna jamaa yangu hapa Zanzibar ni mfanya biashara amejiwa na Kigogo wa CCM anataka amuuzie mavitu yake , eti alifungua biashara akidhani ni rahisi hivyo lakini kaona kumbe ni kazi , mavitu yanakaribia kumuozea kaja kumuomba huyu mfanya biashara anunue mavitu yake amnusuru na kufilisika

WASWAHILI WANA MSEMO, UKIONA VYAELEA VIMEUNDWA
 
Nakumbuka kwenye uzinduzi wa fly over ya ubungo unayetaka ashauriwe Alisema haya “ mnahangaika kwenye Mitandao ya kijamii mnaposti hili mara lile kunipangia la kufanya, Mimi huwa sipangiwi na ukinipangia ni kama unaingilia uhuru wangu, hakuna aliyenichukulia fomu ili nigombee nilichukua mwenyewe. Mkinipangia/mkinishauri ndio mnaharibu kabisa” Bibi FaizaFoxy huyajui haya au CCM huwa mnafikiria kwa kutumia nini. Kulishauri jitu linalojifanya linajua kuliko watanzania wote ni UBOYA. Umechemka bibi.
 
Tanzania tumezoweshwa mambo "complicated" ndiyo eti mazuri. Binafsi naamini the "simpler the best".

Siupendi ukiritimba hata kwenye mawazo au maandishi.
Well then, umeeleweka mkuu. Zao la korosho kama yalivyo mazao muhimu ya biashara linahitaji mjadala mpana hasa kipindi hiki ambapo serikali "imechafua" utaratibu.. mawazo ya wanazuoni kama wewe na ukiwa mdau wa korosho ni muhimu ili kusaidia nini kifanyike katika kuendeleza zao hilo na utafutaji wa masoko etc. Huenda analysis yako ingesaidia wakulima kadhaa huku mtwara..(who knows?)
 
"Se non sta andando bene, chiama tua nonna." Hiyo ni methali maarufu ya Kitaliano ambayo nimepata tabu kidogo kutafuta ya Kiswahili inayofanana-nayo, sijafanikiwa kuipata. Kwa tafsiri isiyo rasmi inasema "ikiwa hakuna linalokwenda sawa, muone bibi".

Nafahamu Kitanzania ukisema "kumuona bibi" au "babu" wengi wengine huhusisha na kuwaona mabibi na mababu ili waongee na mizimu mambo yaende sawa. Wataliano kwa msemo wao huo hawamaanishi kama Watanzania, Wataliano wanamaanisha umuone bibi kwa hekima na busara zake. Labda niifananishe na methali yetu ya "uzee ni dawa".

Binafsi kama bibi, leo nimedhamiria kutoa tafakuri yangu kwenye zao la korosho na ufumbuzi wa "matatizo" ya zao hilo.

Kwanza napenda ku "declare interest" kuwa binafsi ni mdau wa korosho kwa kuwa na mikorosho, mingi tu, tiliyoirithi toka mashamba ya mabibi zetu ile mbegu ya asili ya kizamani mpaka tumejaribu kuiendeleza na kupanda ya kisasa na tunaliona tija nzuri tu.

Ushauri: Serikali ijitowe kimasomaso kuwakopesha bila riba wafanya biashara wakubwa wenye uzoefu wa viwanda kama vile akina Bakhresa na Mo kufunguwa viwanda vikubwa vya kisasa vya kubangua, kusindika na kufungasha korosho kwa kiwango cha Kimataifa na kuwasaidia kushindana na masoko ya Kimataifa.

Hiyo ni badala ya serikali kuingilia zao hilo.

Sababu kuu ni kuwa wafanya biashara hao tayari wana uzoefu mpana wa viwanda vya "food processing" na tayari wana mitaji katika nchi kadhaa za SADC na Afrika Mashariki.

Ni tafakuri tu ya FaizaFoxy .
Serikali ya kuteka, serikali ya visasi, au unamaanisha serikali IPI?

Hebu 2020 tufanye mabadiliko, alafu ndo uje ushari vinginevyo wazungu wanasema "you beat around/ about the bush"
 
Turudi tu kwenye issue ya korosho, wakulima hawaoni hali ni ngumu? Je, walizoea pesa zisizo halali?

Rais alipoongea na wafanyabiashara hakusikia kero na vilio vya wafanyabiashara? Hizo kero ndizo chanzo cha hali ngumu na pia mzunguko wa uchumi ni mdogo kwa mtu mmoja mmoja hivyo maisha kuwa magumu. Kumekuwa na kodi nyingi mno zisizo na utaratibu kiasi ambacho mtu aliyekopa hela za SACCOS au bank badala ya kusogea mbele kiuchumi, anarudi nyuma pengine uli mortgage nyumba au samani za ndani unajikuta unavipoteza ukiona.

Ni miaka minne sasa imepita utawala wa awamu ya 5, sikatai hela kuwepo enzi za JK lkn sidhani kama wote waliokuwa na hela walikuwa mafisadi.
Juzi Mheshimiwa Rais amesema wanaoona hali ngumu ni wale waliozowea pesa zisizo halali.
 
Ukishaiomba serikali ikopeshe bila riba ili kijengwe kiwanda ina maana tayari kuna chaos! Hilo umeliomba mwenyewe! Huoni tayari kuna shida mahali?
Soma para ya kwanza ya post namba moja. Kama hujaielewa soma para ya tatu kama hujaielewa soma upya post yote namba moja kisha endelea na posts za majibu, utaelewa tu.

Naona upo coco beach halafu unauliza baharini ni wapi?
 
Serikali ya kuteka, serikali ya visasi, au unamaanisha serikali IPI?

Hebu 2020 tufanye mabadiliko, alafu ndo uje ushari vinginevyo wazungu wanasema "you beat around/ about the bush"
Korosho ndiyo zimekuteka?

We kweli "mliberali".
 
Turudi tu kwenye issue ya korosho, wakulima hawaoni hali ni ngumu? Je, walizoea pesa zisizo halali?

Rais alipoongea na wafanyabiashara hakusikia kero na vilio vya wafanyabiashara? Hizo kero ndizo chanzo cha hali ngumu na pia mzunguko wa uchumi ni mdogo kwa mtu mmoja mmoja hivyo maisha kuwa magumu. Kumekuwa na kodi nyingi mno zisizo na utaratibu kiasi ambacho mtu aliyekopa hela za SACCOS au bank badala ya kusogea mbele kiuchumi, anarudi nyuma pengine uli mortgage nyumba au samani za ndani unajikuta unavipoteza ukiona.

Ni miaka minne sasa imepita utawala wa awamu ya 5, sikatai hela kuwepo enzi za JK lkn sidhani kama wote waliokuwa na hela walikuwa mafisadi.
Hata sasa wenye hela wapo. Hujawaona juzi wakiongea kero zao?
 
Well then, umeeleweka mkuu. Zao la korosho kama yalivyo mazao muhimu ya biashara linahitaji mjadala mpana hasa kipindi hiki ambapo serikali "imechafua" utaratibu.. mawazo ya wanazuoni kama wewe na ukiwa mdau wa korosho ni muhimu ili kusaidia nini kifanyike katika kuendeleza zao hilo na utafutaji wa masoko etc. Huenda analysis yako ingesaidia wakulima kadhaa huku mtwara..(who knows?)
Wakulima wanachotaka ni kuuza korosho zao hawajali nani anaezinunua. Iwe binaadam au shetani wao wanahitaji pesa tu.

Ninachoongelea hapa ni namna na njia pekee ya kuboresha kipato cha kutokana na korosho.

Hilo litasaidia kila mdau wa korosho, mkulima akiwa wa kwanza.
 
Nakumbuka kwenye uzinduzi wa fly over ya ubungo unayetaka ashauriwe Alisema haya “ mnahangaika kwenye Mitandao ya kijamii mnaposti hili mara lile kunipangia la kufanya, Mimi huwa sipangiwi na ukinipangia ni kama unaingilia uhuru wangu, hakuna aliyenichukulia fomu ili nigombee nilichukua mwenyewe. Mkinipangia/mkinishauri ndio mnaharibu kabisa” Bibi FaizaFoxy huyajui haya au CCM huwa mnafikiria kwa kutumia nini. Kulishauri jitu linalojifanya linajua kuliko watanzania wote ni UBOYA. Umechemka bibi.
Hiyo "mkinishauri" umeongezea wewe.

Asichotaka ni kupangiwa lakini ushauri anaupokea, sana tena.
 
KUNA WATU WAPUUZI SANA YAANI UKIZUNGUMZIA WATU HAWAFANIKIWI HAPA TZ KUTOKANA NA MAZINGIRA MABOVU NA SERA ZA ZISIZORAFIKI WATU KUTUSUA UTASIKIA MTU ANAKUTAJIA MENGI, BAKHRESA, MO LAKINI HATAJI HATA MTU MMOJA WA UKOO WAKE AU KABILA LAKE AU JIRANI YAKE ALEFANIKIWA, SWALI JE INAMAANA UKOO MZIMA HAWAHANGAIKI KUTAFUTA MAPENE? JE UKOO MZIMA NI MBUMBUMBU WA MAISHA JIBU JEPESI NI KWAMBA WATU WANHANGAIKA KADRI WAWEZAVYO TATIZO HAKUNA MAZINGIRA RAFIKI YA WATU KUTUSUA UKIFIKIA LEVEL FLANI VIKWAZO LUKUKI
Punguza kelele. Mbona unatupigia kelele na maandishi ya ilani?

Hivi shule uliyosoma ndivyo Mwalimu wako alikufundisha namna ya na au wapi pa kutumia herufi kubwa, au wapi pa kutumia herufi ndogo? Au ni "ubunifu" wako tu?
 
Back
Top Bottom