Tafakuri ya FaizaFoxy 2: Korosho

Tafakuri ya FaizaFoxy 2: Korosho

Faiza nakubaliana na ushauri wako. Pengine kuboresha huo ushauri Serikali ijikite zaidi kwenye kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara na kuwekeza. Utoaji wa mikopo ya kuwekeza na kuendesha hizo biashara liwe jukumu la mabenki na taasisi nyingine za fedha. Kutokana na data zilizopo mabenki nchini yana uwezo mkubwa wa kutoa mikopo kwenye sekta mbalimbali ikiwemo kilimo ikiwa ni pamoja na mikopo ya kuongeza thamani mazao ya kilimo kama korosho. Hadi kufikia 31 May 2019 mabenki nchini yametoa mikopo zaidi ya shilingi za Kitanzania trilioni 17, kilimo kikiwa ni miongoni mwa sekta zilizochini kabisa kwenye kupata mikopo. Kama mazingira wezeshi yakiwekwa na zao la korosho likapewa asilimia 5 tuu ya mikopo hii, utakuwa ni ukombozi mkubwa kwa wadau wa zao hili.
 
Pita pita zangu humu nimekutana na huu uzi na nimesoma mchango wako kuhusu zao la korosho ushahuri wako ni wa ujenzi.

Mimi napita naenda kunywa kahawa na kashata za karanga.


Ahsanta...

Duuu uko hai, au nyie ndio mlikuwa wapiga deal enzi za JK saa hii mnalimia meno?
 
Hii ya Tanzania kuanza ku add value ktk bidhaa zake ghafi mfano korosho ili nchi ifaidike basi pawepo mkakati wa mapindunzi ya viwanda vyetu (industrial revolution ) kwa mpana mkubwa zaidi ktk sekta zote.

Mfano Jiwe la mgodi wa chuma Liganga ligeuzwe hapahapa Tanzania kuwa mataruma au njia ya reli, sikurubu, nati n.k

Barabara zijengwe kwa nondo na zege toka ktk machimbo na viwanda vyetu vya Tanzania.

Nadharia ya Masomo / ujuzi wa vyuoni na ktk karakana za Ufundi, uhandisi, maabara ziweze kutoa ufumbuzi wa changamoto ktk mazingira yetu kiuhalisia na kwa uwingi mkubwa na siyo vyeti vya kuhitimu kupamba kuta za ofisi na nyumba bila kuleta mapinduzi ktk mazingira yetu.
 
Faiza nakubaliana na ushauri wako. Pengine kuboresha huo ushauri Serikali ijikite zaidi kwenye kuweka mazingira wezeshi ya kufanya biashara na kuwekeza. Utoaji wa mikopo ya kuwekeza na kuendesha hizo biashara liwe jukumu la mabenki na taasisi nyingine za fedha. Kutokana na data zilizopo mabenki nchini yan
Hilo naunga mkono unakuta kiongozi ana ngangani kushindana na wafanyabiashara kujenga vitega uchumi badala ya kukusanya ushuru Mkurugenzi ana waza kujenga hoteli ya 5 Star mjini katikati Paradise cinema Dodoma wananchi wanampigia makofi hiyo hotel ikifilisika na helazetu zimekwenda umiliki usimamizi waachiwe wenye taaluma serikali fuatilia tozo kodi
 
Mtoa mada upo sawa, serikali inabidi itoe support sector binafsi. Risk ni nyingi katika Biashara. Ilifanyika dhambi kuwabeza sector binafsi sakata la Korosho. Waombwe radhi tufungue ukurasa mpya. Wengi wenu kijani mlifisia sana maamuzi yale ya dharula yasiyo na tija.
Mku kwa hali ilivyo hatawakitokea ikaisaidi sects binafsi hakuna unafuu wowote kwani RAIA fedha za kununua hizi bidhaa zitakazozalishwa.
Watazalisha then watabaki na bidhaa kwenye mastoo mpaka muda wa matumizi utaisha mwisho wanapeka dampo baada ya kukosa wanunuzi.
Mzunguko ukirudi kila kitu kitawezekana kabisa shida fedha hakuna
 
Excellent thought, you have hit the point.

Tuombe serekali yetu iamke.
 
Shukran Fayza kwa uzi mzuri
Korosho kama korosho sio tatizo, ni dalili ya matatizo makubwa kwa Wakulima mbali mbali wa mazao yanayoitwa ya biashara ingawa siku hizi hakuna mazao ya biashara na yasiyo ya biashara kila zao ni la biashara
Juzi nimemaliza kusoma kitabu cha Dr. Mengi bahati nzuri ameonyesha jinsi gani yeye mwenyewe alivyonufaika na chama cha Ushirika cha wakulima wa kahawa Kilimanjaro. Sisi wenyewe ni mashahidi kwa upande wa previous generation jinsi gani baadhi ya wazee wetu hivyo vyama vilivyosaidia jamii husika hasa katika mikoa ile ambayo ilikuwa na mazao ya biashara
Dr. Mengi ameonyesha jinsi gani hivi vyama ilikuwa threats kwa wanasiasa ambao walikuwa na wasiwasi kwamba kama Waafrika wangeshiba na kuelimika jinsi gani ingekuwa vigumu kuwaburuza kisiasa
Hilo wazo lako ulilolitoa kuna maelfu ya watu washalitoa na sio kwa korosho tu. Tatizo kubwa ni mseto wa maamuzi ya kiuchumi yanayofanywa kisiasa, chunguza sana hilo utaliona kwenye Karafuu, Kahawa, Pamba na mengineyo. Dr Mengi ameonyesha jinsi gani Tz kuwa siyo masikini bali Watanzania ndio maskini kwa mfano kuna sehemu anasema


"Studies show that the Ruvu Basin can feed the other EA countries, the Kilombero area can feed the whole of Central Africa with rice, Kyela district can produce enough rice to feed the whole of West Africa, the Rufiji Basin can feed North Africa including the Sudan, Ethiopia and Somalia, and Wami and Arusha Chini areas can produce enough rice to feed the whole of Southern Africa. In other words, Tanzania has adequate arable land and water to produce enough food to feed the whole of Africa"
I can, I must, I will
Reginald Abraham Mengi

Yaani kwa kifupi katika haya mabonde ambayo tunayo Tanzania tunaweza kuilisha Africa nzima

Previous week nimeona clip moja kijana mmoja wa UAE anaulizwa na Mwandishi wa Habari mwenye asili ya Nigeria kwanini nchi yao imepiga hatua kiasi kikubwa kiuchumi. Alitoa jibu moja tu ==> Leadership
Akaeleza jinsi gani Nigeria ilivyoanza kugundua mafuta kwanza miaka 10 kabla ya UAE na jinsi gani Nigeria ilivyo na resources nyingine nyiingi ukilinganisha na UAE l

Tuwaachie wachumi, wataalamu wa vyama vya ushirika, wadau wa kilimo na Wanasiasa wafanye maamuzi ya kilimo kwa pamoja. Wala wasiachiwe wanasiasa peke yao watatufikisha hapa tulipo

Natokea ktk mkoa mmojawapo unaozalisha Kahawa, tokea miaka ya 1970s mpaka sasa ni mazungumzo ya kawaida /household talk kusikia wazee wakizungumzia mikasa ya jamaa mbalimbali kule kijijini jinsi gani wanavyohangaika kuivusha kahawa nchi jirani ambako kunasemekana kuna bei nzuri zaidi kuliko wakiuza kwetu. Najaribu kupima
* Ujasiri wa Kuivusha kahawa
* Gharama za Kuivusha
Bado inapatikana bei nzuri zaidi kuliko kwanini ?
* Jee hao nchi jirani si wanaipitisha kwenye Bandari yetu. Then kwanini wao wana bei kubwa kuliko sisi
Mbona hata wanasiasa hata wa upinzani hatuwasikii kuzungumzia hili ??

Hayo utayaona kwenye Mazao yote hapa kwetu Tanzania
 
Kwa ukweli huu mapinduzi ya kiviwanda ni changamoto kufikiwa

 
Usemayo ni mawazo duni sana. Mbona kuna Watanzania wengi sana wamefanikiwa? Bakhresa ni mfano mzuri sana, alikuwa ana kiduka tu cha kushona makubadhi pale mtaa wa Uhuru.

Kila unapoona matatizo ufahamu kuwa kuna fursa, nnakushangaa sana wewe unashindwa kuziona fursa na unayaona makaburi tu.
Kama unaziona fursa kelele za nini? Nenda kafunguwe kiwanda ubangue korosho uuze Saudia. Shida za hii nchi zinaletwa na wazee wa itikadi. Sioni KIPYA kwenye mada yako cha kukiita ushauri.
 
Ushauri: Serikali ijitowe kimasomaso kuwakopesha bila riba wafanya biashara wakubwa wenye uzoefu wa viwanda kama vile akina Bakhresa na Mo kufunguwa viwanda vikubwa vya kisasa vya kubangua, kusindika na kufungasha korosho kwa kiwango cha Kimataifa na kuwasaidia kushindana na masoko ya Kimataifa.
Ni ushauri (wazo) ambalo bila shaka hao hao wafanya biashara wangekuwa na nia ya kuifanya biashara hiyo wasingekuwa wamesita kukopa kwenye mabenki na kwingineko, kama mashirika ya fedha duniani yanayokopesha na hata kuingia ushirika na wafanya biashara, kama International Finance Corp.(IFC) sehemu ya WB.

Wafanya biashara wakubwa kama hao uliowataja, wasingehitaji kamwe kutikiswa ili waione fursa iliyopo bwe(lele) (rere?) kama hiyo. Hawa wangekuwa wameichangamkia siku nyingi.
Nadhani kuna umhimu wa wanaojua biashara hii ya korosho, watueleze kwa nini inakuwa ngumu kiasi hiki.

Huko nyuma tuliwahi kuwa na viwanda kadha vya kubangua korosho, hivi viwanda ilikuwaje hadi ikashindikana visifanye kazi?
Wakulima wa korosho na mazao mengine, kwa vipi hawawezi kuunda ushirika imara na kuendesha shughuli kama hizi ili kufanikisha mazao yao?

Hapa ngoja nitoe mfano hai. KCC (Kenya Creameries Co-operative) wanatuuzia maziwa yao kwa wingi hapa kwetu. Hawa sasa karibia wanasindika Lita milioni mbili kwa siku za maziwa, na wanapambana kikwelikweli na Brookeside ya Kenyatta. Kwa nini sisi imekuwa shida sana katika kila jambo?

Tafakuri ni nzuri, lakini wazo la serikali kugawa hela ya kodi kwa hawa wafanya biashara wenye uwezo mkubwa, nasita kuukubali.
Wakopeshwe wakulima na wapewe mafunzo yanayostahili ya uendeshaji wa shughuli zao, ikiwa ni pamoja na hivyo viwanda.
 
Kama unaziona fursa kelele za nini? Nenda kafunguwe kiwanda ubangue korosho uuze Saudia. Shida za hii nchi zinaletwa na wazee wa itikadi. Sioni KIPYA kwenye mada yako cha kukiita ushauri.
Aiseee, wewe una lako jambo. Mbona huu ni mjadala mzuri tu wa kupeana mbinu?
 
Wazo Murua (Kiswahili fasaha?) kuhusu kukopesha wakulima wa korosho bila riba, nashauri pia hata mazao mengine ya biashara, wakulima wawezeshwe. Ingawa nilipoona kuhusu "tafakuri", nilitarajia kusoma andiko pana na lenye kila aina ya uchambuzi na udadavuaji, ajenda ikiwa zao la korosho. Unfortunately, mwandishi ametoa suruhisho rahisi kwa maada ngumu na pana. chonde chonde Madam Faiza..you're better than this....@FaizaFoxy
 
Aiseee, wewe una lako jambo. Mbona huu ni mjadala mzuri tu wa kupeana mbinu?
Matatizo ya nchi hii hayako kwenye mitaji, yapo kwenye sera. Post yangu ilikuwa inajibu post yake ambayo ilikuwa inajibu post ya member mwingine kwa kuyaita mawazo yake ni mawazo duni.

Shida yetu ni kupenda kufumba macho na kuvuka barabara tukijisahaulisha uwepo wa magari. Tunashuhudia biashara ngapi zikifungwa na 'wazee wa itikadi' wanaishia kusema hao walikuwa wapiga dili?

Tumeshasikia matamko mangapi yenye ukakasi ambayo hamkani yakaleta kigugumizi kwa wawekezaji kuwekeza hapa nchini? Tatizo halipo hapo anaposema. Hivi kuna serikali hapa duniani ambayo haijui umuhimu wa kuwawezesha raia wake kutumia fursa zinazopatikana ndani ya nchi husika?

Hata ile ahadi ya MILIONI 50 KILA KIJIJI si ililenga muktadha huu? That means wanajua. Ndugu yangu, mambo ni mengi...muda ndio mchache. Kama tuna balozi India, na India ndio inaongoza kwa kula dengu na mbaazi, umeshawahi kujiuliza ni zipi kazi za mabalozi wetu huko nje?
 
Mku kwa hali ilivyo hatawakitokea ikaisaidi sects binafsi hakuna unafuu wowote kwani RAIA fedha za kununua hizi bidhaa zitakazozalishwa.
Watazalisha then watabaki na bidhaa kwenye mastoo mpaka muda wa matumizi utaisha mwisho wanapeka dampo baada ya kukosa wanunuzi.
Mzunguko ukirudi kila kitu kitawezekana kabisa shida fedha hakuna
Kwanza kumbuka kuwa kwenye mazao yapo aina mbili kuu, mazao ya chakula na mazao ya biashara.

Korosho ni zao la biashara, biashara ya korosho soko lengwa ni la Kimataifa ili mpate fedha za kigeni.

Korosho iliyobanguliwa na kufungashwa vizuri ina soko kubwa sana duniani. Hilo halina shaka.

Ushindani wa kibiashara utakuwepo, fitna na majungu yatakuwepo lakini mwisho wa siku biashara itafanyika tu kwani demand ipo.
 
Wazo Murua (Kiswahili fasaha?) kuhusu kukopesha wakulima wa korosho bila riba, nashauri pia hata mazao mengine ya biashara, wakulima wawezeshwe. Ingawa nilipoona kuhusu "tafakuri", nilitarajia kusoma andiko pana na lenye kila aina ya uchambuzi na udadavuaji, ajenda ikiwa zao la korosho. Unfortunately, mwandishi ametoa suruhisho rahisi kwa maada ngumu na pana. chonde chonde Madam Faiza..you're better than this....@FaizaFoxy
Tanzania tumezoweshwa mambo "complicated" ndiyo eti mazuri. Binafsi naamini the "simpler the best".

Siupendi ukiritimba hata kwenye mawazo au maandishi.
 
Nikidhani tafakuri "WANALIPWAJE"?
Tuangalie tumejikwaa wapi kabla ya kuangalia tulipoangukia...
Ni wazo jema "kuwakopesha hao wafanyibiashara" lakini kila mfanyibiashara ana soko na malengo yake "KWANINI HAWATAKI KUJENGA WALA KUJIHUSISHA NA UBANGUAJI KOROSHO?" "KWANINI WANAONUNUA KOROSHO GHAFI ZINAPELEKWA INDIA KUBANGULIWA?" Tukipata jawabu kwa maswali hayo tutapata mwanga...
Cha msingi TUACHE POROJO NA SIASA WAKULIMA WALIPWE ILI WASIJE KUSUSA AMA KUCHUKIA ZAO HILO.
 
Nikidhani tafakuri "WANALIPWAJE"?
Tuangalie tumejikwaa wapi kabla ya kuangalia tulipoangukia...
Ni wazo jema "kuwakopesha hao wafanyibiashara" lakini kila mfanyibiashara ana soko na malengo yake "KWANINI HAWATAKI KUJENGA WALA KUJIHUSISHA NA UBANGUAJI KOROSHO?" "KWANINI WANAONUNUA KOROSHO GHAFI ZINAPELEKWA INDIA KUBANGULIWA?" Tukipata jawabu kwa maswali hayo tutapata mwanga...
Cha msingi TUACHE POROJO NA SIASA WAKULIMA WALIPWE ILI WASIJE KUSUSA AMA KUCHUKIA ZAO HILO.

Kuhusu malipo Kassim Majaliwa ameshatolea ufafanuzi na kwa sasa siyo issue tena.

India ndiyo moja ya soko kuu la asili la mazao yetu, historia inatufundisha hata Vasco Da Gama alikuta tayari tuna biashara kati ya India na Kilwa toka enzi na enzi.

Unapokuwa na soko la zamani namna hiyo si hasha unakuwa umejijengea uwezo, uaminifu, mbinu na wateja wa kudumu wa biashara zako.

Mambo matatu makuu India imejijengea kwenye zao la korosho, uaminifu ambao wateja wao wanaamini kuwapa pesa za manunuzi mpaka asilimia mia moja "in advance". Gharama nafuu za ubanguaji kwa mkono kutumia watu kubangua badala ya mashine (hili siku zinavyokwenda linaanza kutoweka huko India). Nidhamu ya kazi na matumizi.

Hizo ndiyo sababu kuu za India kuwa kitovu cha biashara ya korosho.

Sababu hizo ni rahisi kuzipata kwa wafanya biashara wachache wazoefu Tanzania. Tuwatumie.
 
Yaani unataka akina Bakhresa wapewe pesa zetu, kodi za wananchi wajenge viwanda vyao?
Kama ni hivyo basi pesa tupewe sote na sisi tukanunue majiko ya kukaangia korosho ili tuziuze!.
Kwa nini wapewe akina Mo na Bakhresa peke yao?
 
Back
Top Bottom