Sikonge umeona comments za Jamaa yetu Mjegwa? baada ya kutembelea kwetu, cha kushangaza hajasifia uoto wa asili hii ni pamoja na kimvuli vya miembe katika barabara kuu zote hasa ile inayoenda station, ngome kuu zamani, ofisi za mkoa hadi kitete hospital.
Ni kweli wananchi wa Tabora hawana utamaduni wa kupanda daladala sababu vitongoji vyake vipo jirani sana, kwa hiyo huhitaji kupanda gari kwa mfano toka Mjini kwenda kitete, kanyenye, ng'ambo, Tambukareli huhitaji daladala -- hata mie nikenda likizo natembea tu sababu kwanza hakuna joto kama hapa kwenu Dar. Hoja ya Umaskini na udhaifu wa kubuni miradi ya maendeleo isihusihwe na hili na kutembea kwa miguu na matumizi ya baskeli - huu ni utamaduni tu wa mkoa wetu kama ilivyo Tanga.
Ni kweli hali ya uchumi inazidi kudidimia hasa baada ya Reli ya kati kufa kifo kibaya, wengi tulisikitika kwani ndiyo ilirahisisha kukuza uchumi ukizingatia Tabora ilikuwa kiungo cha usafiri wa Reli toka Kigoma, Mwanza hadi Dar.
Pia kumbukani Tabora haijaunganishwa na mikoa mingine ambayo imepakana nayo kwa njia ya barabara, hii pia inachangia mkoa ukose nguvu ya kiuchumi na biashara kwa wakazi wa Tabora kuwa ndoto ya mchana. Kwa mfano Tabora ingeweza kuunganishwa na Mbeya, Kigoma via Mpanda (Kwa waziri Mkuu wetu), Nzega (Wilaya ambayo ina nguvu ya uchumi sababu ya madini na pia barabara kuu ya Dar Mwanza inapitia hapo), Siginda via Itigi na ile ya Tabara Kahama, Geita hadi mwanza, kama mnavyojua Kahama ni mji wenye madini na kilimo hasa cha mpunga na mahindi.
Mbali na kilimo cha zao la Tumbaku na Uvunaji wa mbao aina na Mninga kwa wingi zaidi Tanzania, Ikumbukwe pia Mkoa wa Tabora ni mkoa pekee unaotoa zao na Asali na Nta ambayo ina soko kubwa sana nchi ya arabuni na ulaya, kama kweli serikali ingelifufua kiwanda cha nyuki ili kuwafanya wananchi wa mkoa huu ambao 80% ni wakulima wadogo wadogo na wale wavunaji wa asali basi ingesaidia sana kukuza uchumi wa mkoa huu.
Mwandishi kapita Tabara mjini tu, lakini ningemshauri kama angekuwa na nafasi angesafiri katika wilaya ndani ya mkoa huu kuona fursa nyingi tu ambazo kama kweli tungezitilia mkazo kama Taifa basi zingeweza kuongeza pato la taifa na pia kuwafanya wenyeji wa Tabora kunyenyuka ki-uchumi.
Kwa kuanza ningeomba sana mwandishi tuwasiliane ili tuanze kulifanyika kazi hili la Zao la Asali - nina uhakika ni Tabora pekee inatoa Mamillion ya lita ila zinaishia mikononi kwa kina MO na wengine wenye mitaji wanaowalalia wananchi wa mkoa huu.
Pia viwanda vingi vinatakiwa kufufuliwa -- nakumbuka vichache tu ambavyo vimekufa kifo cha mende kama kiwanda cha nyuzi na SIDO ambapo vijana waliweza kupata ajira miaka hiyo. Pia kufufua vyuo ambavyo vimekufa au kama vipo basi ni mahututi kama chuo cha Nyuki; chuo cha ardhi; Reli na hata kile chuo cha kihistoria cha Uhazil.
Mwisho natoa wito kwa wasomi na wazawa wa Tabora ambao ni wengi sana wapo katika taasisi za elimu ya juu, waangalie ni namna gani wanaweza kusaidia kukuza uchumi wa mkoa wao wakisaidiana na sisi wazawa wengine tulioko huku, maana wengi kaka zangu wameloea huko pwani na kaskazini hawataki kurudi kabisa kusaidia mipango ya maendeleo katika sehemu walizotoka hasa katika sekta za kilimo, elimu na ufugaji ambazo ndizo pekee za kumkomboa mwananchi wa kipato cha chini kabisa
Tabora ni ngome ya CCM, na CCM lazima iwe na ngome mahala palipojaa wajinga ( Tabora ) na kama hiyo haitoshi hata Ubunge wamempa Msomali wakati Watanzania wenzao wapo. hii ni mijtu ya hovyo kweli kweli!!
kwa hiyo ulitaka ajenge kama wa taifa?,hebu tupe picha uwanja wa mpira wa karatu,bagamoyo,pemba na moshi mjiniView attachment 46152
Na huu ndio uwanja wa mpira wa mji ambao mbunge wake anadai mpira uko kwenye damu yake!.... Unafiki mkubwa.
Mkuu lakini mimi nadhani Tabora inakaribia kufunguka kwa kuwa kuna hiyo miradi ya kuwekea lami barabara za kuingia na kutoka mkoa wa tabora (angalia post ya FF). Pia Tabora itakuwa kiungo muhimu kati ya Mpanda (Mbuga ya Katavi) na mikoa mingine. Jitahidini tu mhakikishe barabara ya Tabora - Ipole - Mpanda inawekewa lami pamoja na ile ya Tabora - Ipole- Rungwa - Mbeya.
Kuhusu asali nasikia wazungu siku hizi hawaipendi sana asali ya Tabora na Mpanda kwa kuwa inakuwa na vimelea vya nicotine. Naambiwa hiyo inatokana na kwamba nyuki huwa wanachavusha maua ya tumbaku na kwenda kutengenezea asali. Tumbaku ina nicotine hivyo asali itokanayo na na maua ya Tumbaku huwa ina nicotine. Ni afadhali Tabora ikaachana na kilimo cha tumbaku ili ijiimarishe kwenye asali kwa kuwa huenda sigara (tumbaku) ikapigwa marufuku kama bangi!
Kila la kheri Tabora.
Mkuu nashukuru. Nilikuwa nimeenda kufanya uwindaji wa kitalii huko kwenye hifadhi ya Rungwa nikapita pale Sikonge nikapata hiyo chakula!Asante mkuu karibu ujipatie MATOBOLWA NA NSANSA ZA NTWILI
Thanks FF najua umecopy na kupaste kwenye site fulani ama wewe unafanya wizara ya magufuri, ukweli ni kwamba kuna kambi zimejengwa njia ya kwenda urambo nadhani mpaka sasa ni takribani zaidi ya mwaka mmoja lakini sijaona kitu cha maana kilichofanyika pale zaidi ya idadi kubwa ya NYOKA na MIJUSI kupungua kutokana na idadi kubwa ya wachina waliopo kambini, Ninasubiri tarehe ya kukamilisha ujenzi huo..................................
View attachment 46152
Na huu ndio uwanja wa mpira wa mji ambao mbunge wake anadai mpira uko kwenye damu yake!.... Unafiki mkubwa.
Jamani barabara za mkoa wetu wa Tabora zinatisha. Mpaka sasa hakuna barabara hata moja yenye rami ambayo inaingia mkoa wa Tabora. Chama changu cha Chadema mko wapi? Waamsheni wananchi wa Tabora kwani ni waelewa. Siku zote wanyamwezi na wasukuma ukiwaelimisha wakaelewa watakuunga mkono. Chadema nendeni Tabora kwani waanzilishi wa vyama hakina Fundikira, Mapalala na Kasela Bantu wote walikuwa ni wenyeji wa Tabora.
Wana JF muwe huru kuchangia kwenye thread ili mkoa wa Tabora uweze kuinuliwa. Kwasababu wanasiasa wenye maamuzi nao wanatembelea mtandao wetu wa JF. Nahisi kuna kitu kitafanyika.
Jamani mimi ni wa huko lakini mjadala huu hauna vigezo wala viashilia kuonyesha Tabora imedidimia mbali na kutoa hisia zetu. Faiza amejaribu kuonesha facts na wengine tuoneshe facts. kama ni barabara tulinganishe na mikoa mingine, kama ni regional GDP tulinganishe na mikoa mingine, kama ni mchango wake kwenye national GDP tulinganishe na mikoa mingine, n.k. Kwa kifupi tuwe na variables na indicators ambazo zitaonyesha kuwa kabla ulikuwa juu na sasa huko chini pia in comparison with other regions with similar comparative advantages!!! Otherwise na sisi tutakuwa tunajadili kama tuko pale kwa fundi viatu Manzese darajani!!!!!!
Kwa msaada soma kwanza Tabora region: socio-economic profile 2005 available at NBS library.
Kutwa nzima wanakunywa kahawa,kucheza bao,draft.wataendelea saa ngapi?hawa hawapishani na wazaramo!
Umejuaje? Kinachonifurahisha kwa hawa wanyamwezi wa Tabora ni kuwa na jambo moja only ambalo ni unform kwao si kwa watoto, vijana, wazee, au hata wale unaowaona machoni kwako kuwa ni vikongwe lakini ni balaa, jambo hilo wao ni jadi na lipo ndani ya damu bila kujali umri, wapi, lakini zaidi zaidi inapoingia giza Tabora ya mchana huwa si ile ya kagiza kanapoingia, utaona kama kumbi kumbi vile from no where wametapakaa kila kona ushindwe weye, Tabora ni mji wa kipato kidogo hivyo wewe Maggid kama kamchezo kale unakapenda sijui kama utarudi salama, kuanzia buku mpaka msimbazi tosha kabisa, si mtoto si mama si kikongwe ni balaa wote wanashindana nani kafungasha zigo kubwa na hapo ni wewe tu kwa raha zako, ukitaka kuthibitisha usiku nenda pale Orion Hotel au kwa sie tusio na uwezo wa kufika Tabora basi angalia tabia hizo toka kwa viongozi wanaotoka Tabora (maisha ya ndani) eg Kapuya mzee wa Ngwasuma au Mr 6 wote hao ni "formula one" kama walioko Tabora
kwa hiyo ulitaka ajenge kama wa taifa?,hebu tupe picha uwanja wa mpira wa karatu,bagamoyo,pemba na moshi mjini
Hii topic sasa imeamua kututukana,hivyo vimichezo ni vya kila mahara,sehemu gani hakuna?Umejuaje? Kinachonifurahisha kwa hawa wanyamwezi wa Tabora ni kuwa na jambo moja only ambalo ni unform kwao si kwa watoto, vijana, wazee, au hata wale unaowaona machoni kwako kuwa ni vikongwe lakini ni balaa, jambo hilo wao ni jadi na lipo ndani ya damu bila kujali umri, wapi, lakini zaidi zaidi inapoingia giza Tabora ya mchana huwa si ile ya kagiza kanapoingia, utaona kama kumbi kumbi vile from no where wametapakaa kila kona ushindwe weye, Tabora ni mji wa kipato kidogo hivyo wewe Maggid kama kamchezo kale unakapenda sijui kama utarudi salama, kuanzia buku mpaka msimbazi tosha kabisa, si mtoto si mama si kikongwe ni balaa wote wanashindana nani kafungasha zigo kubwa na hapo ni wewe tu kwa raha zako, ukitaka kuthibitisha usiku nenda pale Orion Hotel au kwa sie tusio na uwezo wa kufika Tabora basi angalia tabia hizo toka kwa viongozi wanaotoka Tabora (maisha ya ndani) eg Kapuya mzee wa Ngwasuma au Mr 6 wote hao ni "formula one" kama walioko Tabora
mhanya kaunga na figher , kwapela igembe kwenuko?sasa mukova kusuve hangi? ila mwenugu nago muhayo wakutega hivanza leki kugeme! !!! guys pale mto wala way to sikonge hapafai kuanzisha shamba kubwa la kilimo cha mpunga kwa umwagiliaji just to set an example to others!!! basi tunaweza kuanza na hilo kwanza huku tukijadili hilo la kilimo cha maembe ya miaka mitano maana ardhi Tabora ni ya kumwaga.Wapanga du, ni dada yako lkn! I am glad umeamua kitu cha maana; there is a lot to do in Tabora. Wasomi wengi wameukimbia mji, waliobaki ni waswahili tu unategemea nini?
mhanya kaunga na figher , kwapela igembe kwenuko?sasa mukova kusuve hangi? ila mwenugu nago muhayo wakutega hivanza leki kugeme! !!! guys pale mto wala way to sikonge hapafai kuanzisha shamba kubwa la kilimo cha mpunga kwa umwagiliaji just to set an example to others!!! basi tunaweza kuanza na hilo kwanza huku tukijadili hilo la kilimo cha maembe ya miaka mitano maana ardhi Tabora ni ya kumwaga.
Tabora for change --2015.