Tabora iliyodidimia inahitaji kuinuliwa...

Tabora iliyodidimia inahitaji kuinuliwa...

Mkuu Maggid, ya Tabora nakukubalia 100%, nakushauri fika LINDI, unaweza kuukimbia mji ndani ya dakika chache baada ya kuwasili
 
mapori bei rahisi sana balaaa, kwanza bure tu,najipanga

Wageni kibao wanavamia na kutajirika. Waha sasa hivi wamejazana kuliko hata wachaga. I was home the other month, si groceries, maduka ya dawa hadi mabucha ya nyama ni ya kinaWACHU tu.

Ruzoka katuanzishia chuo, nawashauri hata kama mliacha mapagara, mkarenovate nyumba sasa bei imeanza kuwa juu!

Tukijapanga wenyewe twaweza kuanza kuprocess hata maembe na matunda mengine. Wanzuki yaweza kuboreshwa tukiamua kuibrew kisasa!

There are lots to be done, twahitaji kudare tu.
 
Ni kwa nini miji waliyojaa kina MS ni ya hovyo sana lakini wao wanaishi comfortably?
 
Mkuu Maggid, ya Tabora nakukubalia 100%, nakushauri fika LINDI, unaweza kuukimbia mji ndani ya dakika chache baada ya kuwasili
Siyo Lindi tu,mikoa ya kusini yote na vitongoji vyake(ukiiondoa Ruvuma) kulikobaki kote kumeoza na wao ndiyo mtaji mkubwa sana
wa CCM
 
Wageni kibao wanavamia na kutajirika. Waha sasa hivi wamejazana kuliko hata wachaga. I was home the other month, si groceries, maduka ya dawa hadi mabucha ya nyama ni ya kinaWACHU tu.

Ruzoka katuanzishia chuo, nawashauri hata kama mliacha mapagara, mkarenovate nyumba sasa bei imeanza kuwa juu!

Tukijapanga wenyewe twaweza kuanza kuprocess hata maembe na matunda mengine. Wanzuki yaweza kuboreshwa tukiamua kuibrew kisasa!

There are lots to be done, twahitaji kudare tu.

poa kaka ila tukianza wachaga ,waha na sisi dar watatukimbiza,hakuna anayepanga kuzaliwa alivyo,muha,muhindi etc yote ni mipango ya sir GOD mwenyewe,ila twendeni tukainyanyue 2015
 
WatakaoiendelezaTabora ni Wanatabora wenyewe. Wasitgemee kuwa kuna mtu eti atatoka nje ya Tabora kuja kuiendeleza. Hilo wasahau.
 
WanaJanmvi,
Tatizo sio mbunge mmoja, Tabora imekuwa na wabunge tangu tupate uhuru. Itakuwa si kumtendea haki mbunge mmoja kwa udhaifu uliodumu miongo mingi.

Kwa historia tu Tabora ni mji uliotakiwa uwe makao makuu kutokana na harakati nyingi za kisiasa na kuwa kiungo muhimu cha usafiri kati ya kanda ya magharibi, ziwa na kati.

Tabora ina ardhi nzuri na uoto mzuri wa asili.
Watu wa development programs wana njia mbali mbali za kuhamasiha maendeleo. Mfano, kuna ile ambayo miundo mbinu na huduma hupelekwa mahali na watu huifuata.

Njia ya pili ni ile ya eneo kulazimisha uwepo wa huduma mbali mbali na ukuaji wa miundo mbinu kutokana na mahitaji. Mfano, Serikali ililazimika kuingilia kati ujenzi wa daraja la bara bara ya Segera Chalinze lilipovunjika kwasababu mikoa ya kanda ya kaskazini ni sehemu muhimu sana ya uchumi wa nchi . Hata kama hili litawaudhi baadhi ya watu lakini ndio ukweli.

Maendeleo ya Tabora yataletwa na watabora kwanza na mambo mengine yatatokana na mahitaji na umuhimu wa shughuli. Haiwezekani kujenga bara bara kisa kuna uoto wa asili!! bara bara itajengwa kwasababu kuna mahitaji fulani na huduma.
Fursa zilizopo zitumiwe na wana Tabora na si kusubiri taifa izitumie fursa hizo. Taifa itazitumia pale wana Tabora watakapokuwa wamezitumia kwanza. Kwanini mtu atoke nje ya Tabora na afanikiwe ili hali wana Tabora wapo pale ?

Ikifika hapo ndipo nina hitimisho moja. Tatizo si rasilimali wala ujenzi wa miundo mbinu. Tatizo ni kuwa wana Tabora hawajaelewa fursa walizo nazo na jinsi ya kuzitumia ili zilazimishe taifa kuangalia eneo hilo kwa ukaribu zaidi.
Suluhisho si kujenga miundo mbinu ni kuinua kiwango cha elimu, kuhamasisha wana Tabora wajitambue na fursa zinazowazunguka.

Hakuna kontena la maendeleo kutoka Dar kwenda mikoani, maendeleo yanaletwa na msisimko wa jamii pale ilipo, msisimko utakaolazimisha huduma.
 
OYAAAA, Mnyamwezi nimefika kwa sasa.

Kwanza wewe wa Mpwapwa, MSULA EVE. Unatuita sisi Mbwa?

Nimekaa Dodoma sana tu na nilikuwa naona vijana wakija mwaka wa Kwanza pale Mazengo, wakiwa wananuka harufu fulani ambayo unaisikia kabisa ni ya mbuzi. Wembambaa na wamekondeana na wakila kila kinachokatiza.

Wagogo ni kabila pekee wanakula ugali wa pumba. Utawasikia asubuhi wakiulizana "Chikulya Chi?" Na jibu utasikia "Wa mhumba." Sasa binadamu utakulaje ugali wa Pumba jamani? Umekuwa Nguruwe wewe? Nyie endeleeni sana kubeba mizega mizega ya Mikaa huku mnakula miwa yenu. Usiku ukifika, imbeni sana "Myujiyuji, mti wa lulenga, si wakukata zengo."

Nikija kwa ELNINO na Majjid, ntajibu baadaye maana inabidi kukaa na kutulia na siyo kukurupuka.

Kwa aliyeuliza kwa nini USA wanaita Unyamwezini, nafikiri ni kutokana na lile tusi la Mother F...... ambalo ni Wanyamwezi pekee kama sikosei, tuna tusi kama hilo. Kama unafahamu Kinyamwezi, kuna wimbo unaimbwa "Nguluve ikulyaga twingi vayaya........ nani wamleta 'Mt***** Nina/n*oko' tumlye masumule........ Nafikiri Elnino atakuwa anaufahamu zaidi.

Kuhusu Rage, kwa kweli ni makosa ya CCM kumpitisha mtu kama huyu na baadaye wanaweka U-Chama mbele ili ashinde tu CCM na Wanyamwezi acha wazike wafu wenzao.

Makala yangu itafuata jamani........
 
Acha na ntonya mpwapwa sema mkuu tunaitajika mimi,wewe na wengine kuujenga mji wetu aisee!!
 
Nimekulia Tabora pia na kusoma form 1 mpk 4 kule..ni kweli kuwa watu hawajishughulishi kbc kias kwamba inawaathiri mpk watoto wao..mfano mzuri ni rafiki zangu niliosoma nao ambao ni wanyamwezi...mmoja nilisoma nae mkoa mwngne then chuo akaenda UDOM kasoma education policy planning...bht nzuri mm mchakato wa kazi nilianza kutafta mapema so nimeanza kufanya kazi nipo mwaka wa kwanza chuo...huyu jamaa baada ya kumaliza chuo cku moja nilimuuliza huko Tabora unafanya dili gani lolote? Dah jibu lake nilichoka aise akajibu NIPO TU NAIMBA KWAYA KANISANI...
Sasa hapo utategemea Mboka itaendelea kweli km huyu ni mmoja wa wwasomi wetu
Duh...Mboka Tabora...sio siri Tabora inahitaji mwamko...WANYA MOON ..acheni kulala..Nimesoma Tabora Boys ninaujua vzuri...pipo za Tabora ni kama wapwani..kutwa taarabu kazi hawataki ...
 
Hatuwezi kuanzia kwenye tufanye nini. Kwanza lazima tulielewe tatizo letu na ndiyo tuje kwenye kujadili tufanye nini.

Matatizo ya Tabora wengine wameshaanza kujadili watu na wengi wanasema ukweli. Kuna yale yanaonekana na yale yasiyoonekana kwa haraka ambayo yataka mzawa uwe kwenye kilima fulani hivi ndiyo uyaone au mgeni anayekuja na kuishi na wenyeji kwa muda mrefu.

Hawa wanaosema nilisoma Tabora Boys sijui au niliishi Tabora mjini hawa hawawezi kuyaeleza matatizo ya pale Tabora kwa ufasaha.
Acha na ntonya mpwapwa sema mkuu tunaitajika mimi,wewe na wengine kuujenga mji wetu aisee!!
 
sehemu yoyote yenye majungu na bifu zisizokuwa za msingi huwa inamatatizo sana, watu wa tbr ni wavivu hawapendi kujituma pia hata viongozi wenyewe kwa wenyewe wanagombana i.e mps. tufanye kazi tuwe tunawivu wa maendeleo maendeleo yatakuja tu.
 
Watu wenu akina 6 badala ya kuwasaidieni wao wanazungumzia tu Urais kila siku,stupid!
 
Wageni kibao wanavamia na kutajirika. Waha sasa hivi wamejazana kuliko hata wachaga. I was home the other month, si groceries, maduka ya dawa hadi mabucha ya nyama ni ya kinaWACHU tu.

Ruzoka katuanzishia chuo, nawashauri hata kama mliacha mapagara, mkarenovate nyumba sasa bei imeanza kuwa juu!

Tukijapanga wenyewe twaweza kuanza kuprocess hata maembe na matunda mengine. Wanzuki yaweza kuboreshwa tukiamua kuibrew kisasa!

There are lots to be done, twahitaji kudare tu.

Mkuu Kaunga,

Sioni kama kuna ubaya watu wa kutoka nje ya mkoa kujihusisha na biashara za aina yoyote ile, nadhani hao wageni wanaweza kuwa ni chachu ya kuleta maendeleo kwa wazawa. Wazawa wataona kwamba inawezekana kabisa kufanya shughuli kama hizo na hivyo nao wanaweza kuanza kujishughulisha nazo.

Mapagala [lol] ... tatizo ni kwamba nimeangalia picha nyingi ambazo zimepigwa na Maggid Mjengwa ni nyumba za miaka 1970s [zama hizo wakiezeka na madebe na zilikuwa ni za miti]. Ma-Mwinyi anaowaongelea ndio wenye hizo nyumba na hawana mshiko [fedha] za kubomoa nyumba ili nyumba nzuri na za kisasa ziweze kujengwa. Ukiangalia nyumba za maeneo ya Ng'ambu, Kiloleni, Kanyenye, Isevya [vitongoji vya asili] nyingi zimechoka. Nyumba hizo ziko tofauti sana na zile ambazo zimejengwa miaka ya 1990 na 2000 maeneo ya Bachu, Cheyo na Ipuli. Kwa hiyo kuwa na sura mpya ya nyumba za hapo ni lazima wenyeji wawe tayari kukubali kuachia nyumba hizo ili wenye fedha waweze kujenga. Bahati mbaya wanyamwezi huwa ni masikini jeuri, anaweza kuona kuachia pagala lake la miti lililoezekwa na madebe kwamba anajidhalilisha, lakini haelewi kwamba kukaa kwenye nyumba kama hiyo ambayo inaweza kudondoka siku yoyote ni kudhalilika zaidi.

Swala la ku-process matunda ni gumu kwa kiasi kikubwa kwa kuwa miundo mbinu ya Tabora [barabara] ni mibovu sana na pia within Tabora hakuna soko la kutosha. Muwekezaji yeyote atakaye taka kuweka kiwanda kama hicho akifanya feasibility study hawezi kuwa tayari kuwekeza mtaji wake kwa sababu ya usafiri. Maembe yanatoka vijijini na kwa ujumla Tabora hakuna feeder roads ambazo zinaweza kupitika mwaka mzima.

Ili kujikomboa, inabidi tukubali kwamba miundo mbinu iboreshwe [barabara]. Kuna mazao mengi sana yasilyo rasmi ambayo yanaharibikia kijijini. Ukienda sehemu kama Igalula kuna asali na nta kibao, lakini kama reli ya kati haifanyi kazi ndugu zangu wa Igalula, Igoweko, Nyahua na kwingineko wanaishia kulia tu. Hakuna barabara ya uhakika ya kuwaunganisha watu wa hayo maeneo na Tabora mjini.

Ukija kwa ndugu zangu wa Sikonge, ndio usiseme kabisa pamoja na kwamba asilimia kubwa ya tumbaku na asali inatoka huko, barabara ni mbaya sana na tangu mfumo wa ununuzi wa tumbaku uwe wa soko holela, makampuni ya wanunuzi wa tumbaku yamekuwa yakiwanyonya ipasavyo kwa kuwauzia mbolea kwa bei kubwa na kisingizio ni gharama za usafiri na wakija kununua tumbaku pia wananunua kwa bei ndogo bado watasema kwamba usafiri gharama.

Biashara ya mbao ndio ilishakwenda na maji, sijui hata kama bado kuna "ma-digala", maana mininga yote ilishaisha. Kwa hiyo option pekee inayobakia ni kujikita kwenye kilimo na asali. Miaka ya zamani kulikuwa na Chama cha Wafuganyuki Tabora na ninadhani pia kuna Chuo cha Nyuki, soko la asali na nta lipo kama usafiri utakuwepo. Pia wasomi wa sayansi wanaweza kutoa ushauri wa kuboresha wanzuki [lol]. Wanzuki ikiboreshwa na watani zetu wahehe nao wataboresha ulanzi [ulasi] wao!

Mkoa unasikitisha na kukatisha tamaa.
 
Hatuwezi kuanzia kwenye tufanye nini. Kwanza lazima tulielewe tatizo letu na ndiyo tuje kwenye kujadili tufanye nini.

Matatizo ya Tabora wengine wameshaanza kujadili watu na wengi wanasema ukweli. Kuna yale yanaonekana na yale yasiyoonekana kwa haraka ambayo yataka mzawa uwe kwenye kilima fulani hivi ndiyo uyaone au mgeni anayekuja na kuishi na wenyeji kwa muda mrefu.

Hawa wanaosema nilisoma Tabora Boys sijui au niliishi Tabora mjini hawa hawawezi kuyaeleza matatizo ya pale Tabora kwa ufasaha.

Mhanya,

Nimependa maelezo yako. Nadhani ili kuweza kujikwamua kutoka hapo, lazima tujue nini kilisababisha tukakwama na bahati mbaya viongozi wetu [wabunge] sidhani kama wanaumiza vichwa ili kujua kwanini mkoa umedidimia kiasi hicho au kwanini mkoa hauendelei. Hii inahitaji kiongozi ambaye ameishi hapo kwa muda mrefu sana na awe ni mwendaji wa mara kwa mara kuona kinachoendelea na kujionea hali halisi.

Tatizo kubwa ninaloliona ni kwamba hakuna juhudi za pamoja za wabunge wa mkoa mzima wa Tabora za kusaidia kuendeleza mkoa. Wabunge wa mkoa wengi wao wanakimbilia ku-lobby vitu vidogo vidogo kwa ajili ya majimbo yao, lakini yale ambayo ni ya muhimu kama miundo mbinu hawayagusi.

Wengi wa hao wabunge huwa hawana muda wa kuchunguza matatizo na pia hawaoni ubaya kwa kuwa hawaishi huko, maana makazi yao ya kudumu yako Dar. Saa ngapi ataona aibu ya nyumba zilizochoka au barabara ambazo hazipitiki kirahisi au kuona ugumu wa maisha ili hali 80% ya maisha yake yuko Dar na Dodoma ambako hakuna ugumu kama ulioko Tabora?
 
Back
Top Bottom