Mkuu watu wa Tabora sijui wanapatwa na nini
Huwezi amini,huduma ya maji kwa sehemu kubwa,kubwa kabisa ya mji ule inapatikana kwa shida sana.Ukipita mitaani,Ng'ambo,Isevya,Kaloleni,Mwanza Road,Bachu,Mwinyi utasikitika sana watu wamepanga foleni kwenye kibomba kinachururiza maji
Na majanga zaidi ukisogea kilomita kadhaa kutoka manispaa kwenye vijiji kama Manoleo,maji hakuna completely watu wanategemea vijichemchem na maji yenyewe ni meupe kama maziwa
Ndugu zangu wa Tabora,mjini hususani,Rage kashashindwa kuwasaidia..hata kama mtawabakiza CCM,basi wekeni mtu mwingine aisee,ni majanga haya