jamani sijui wenzangu kama mmepata kung'amua kitu hiki mkoa wa Tabora ni kama vile umekufa kwa jinsi nionavyo mimi licha ya wakazi wake kuwa na chakula pengine cha kutosha lakini miaka nenda rudi nikipita hapo sioni mabadiliko utafikiri vile hakuna wazawa waliokwenda shule mpaka leo mbavu za mbwa ziko katika mji tatizo liko wapi?
-kwa wazawa wenyewe?
-serikali?
kwa kuwa kama ni viongozi waliosoma na kuwepo katika sytem hii ya serikali wapo tangu kitambo mbona kunadorola yaani huwa napata maswali mengi kichwani?
hebu nisaidiane hasa ninyi wazawa wa tabora na wenye kuufahamu vizuri unastahili kuwa kama ilivyo? ukizingatia kuwa ni mkoa wa kihistoria katika harakati za uhuru wa nchi hii.
Kwanza nikupe HONGERA kwa Mada nzuri uliyotuwekea Mezani...
HONGERA SANA,,ila nasikitishwa na hawa wenzangu na mimi ambao bila kutaja jina la mtu au mbunge flani au chama flani ... Mada hiyo kwao haijakuwa ya Kisiasa..
Tabora ni mkoa kama mikoa mingine tu katika Tanzania yetu masikini(najua wengi hamtaki hili neno ingawa ndo ukweli wa mambo)...
Maendeleo ya Taifa/sehemu yoyote utegemea mambo mbalimbali ikiwemo WATU WA JAMII USIKA..
Umezungumzia matatizo kadha wa kadha ya Tabora... Hakika yapo yanayoweza kutatuliwa na Serikali na mengine ni watu wa Eneo husika....
Wewe umesikia wapi katika miaka 10 iliyopita, nchi imewajengea wananchi makazi bora bila ya kuwa na tatizo la msingi kama ilivyotokea KENYA kwa wakazi wa KIBELA...
Ni ngumu sana ndugu yangu kumlazimisha mtu kulala ndani ya chandarua kabla ya kujua umuhimu wake,, mim nasema swala la makazi boro,,yani nyumba nzuri katika miji ya mikoa mingine ni Juhudi tu za wananchi wa Eneo husika na si vinginevyo..!!
Hakuna mkoa ambao wananch wake waliwai pewa ruzuku ya kujengea...
Hvyo ELIMU ya umuhimu wa makazi bora ni lazima itolewe kwa wanaTABORA na watu wajue umuhimu wake..
Naskia mtu anasema "sasa hyo si kazi ya Serikali"
Ndiyo lakini yapo mashirika Mengi yanayojitolea kutoa Elimu kama hzi katikati ya Jamii,,mkisubiri Serikali mpaka Itengee bajeti swala hilo,, mtasubiri sana na mpaka hzo nyumba zitawabomokea...!!
Wito wangu ni kwamba wananchi wa Tabora amkeni na mkatae kukaa kwenye vijumba vibovu kwa kujenga nyumba za Kisasa...!
Swala la Barabara nadhani niwaachie wenzangu waendelee..