ELNIN0
JF-Expert Member
- Nov 26, 2009
- 4,161
- 1,460
Sikonge umeona comments za Jamaa yetu Mjegwa? baada ya kutembelea kwetu, cha kushangaza hajasifia uoto wa asili hii ni pamoja na kimvuli vya miembe katika barabara kuu zote hasa ile inayoenda station, ngome kuu zamani, ofisi za mkoa hadi kitete hospital.
Ni kweli wananchi wa Tabora hawana utamaduni wa kupanda daladala sababu vitongoji vyake vipo jirani sana, kwa hiyo huhitaji kupanda gari kwa mfano toka Mjini kwenda kitete, kanyenye, ng'ambo, Tambukareli huhitaji daladala -- hata mie nikenda likizo natembea tu sababu kwanza hakuna joto kama hapa kwenu Dar. Hoja ya Umaskini na udhaifu wa kubuni miradi ya maendeleo isihusihwe na hili na kutembea kwa miguu na matumizi ya baskeli - huu ni utamaduni tu wa mkoa wetu kama ilivyo Tanga.
Ni kweli hali ya uchumi inazidi kudidimia hasa baada ya Reli ya kati kufa kifo kibaya, wengi tulisikitika kwani ndiyo ilirahisisha kukuza uchumi ukizingatia Tabora ilikuwa kiungo cha usafiri wa Reli toka Kigoma, Mwanza hadi Dar.
Pia kumbukani Tabora haijaunganishwa na mikoa mingine ambayo imepakana nayo kwa njia ya barabara, hii pia inachangia mkoa ukose nguvu ya kiuchumi na biashara kwa wakazi wa Tabora kuwa ndoto ya mchana. Kwa mfano Tabora ingeweza kuunganishwa na Mbeya, Kigoma via Mpanda (Kwa waziri Mkuu wetu), Nzega (Wilaya ambayo ina nguvu ya uchumi sababu ya madini na pia barabara kuu ya Dar Mwanza inapitia hapo), Siginda via Itigi na ile ya Tabara Kahama, Geita hadi mwanza, kama mnavyojua Kahama ni mji wenye madini na kilimo hasa cha mpunga na mahindi.
Mbali na kilimo cha zao la Tumbaku na Uvunaji wa mbao aina na Mninga kwa wingi zaidi Tanzania, Ikumbukwe pia Mkoa wa Tabora ni mkoa pekee unaotoa zao na Asali na Nta ambayo ina soko kubwa sana nchi ya arabuni na ulaya, kama kweli serikali ingelifufua kiwanda cha nyuki ili kuwafanya wananchi wa mkoa huu ambao 80% ni wakulima wadogo wadogo na wale wavunaji wa asali basi ingesaidia sana kukuza uchumi wa mkoa huu.
Mwandishi kapita Tabara mjini tu, lakini ningemshauri kama angekuwa na nafasi angesafiri katika wilaya ndani ya mkoa huu kuona fursa nyingi tu ambazo kama kweli tungezitilia mkazo kama Taifa basi zingeweza kuongeza pato la taifa na pia kuwafanya wenyeji wa Tabora kunyenyuka ki-uchumi.
Kwa kuanza ningeomba sana mwandishi tuwasiliane ili tuanze kulifanyika kazi hili la Zao la Asali - nina uhakika ni Tabora pekee inatoa Mamillion ya lita ila zinaishia mikononi kwa kina MO na wengine wenye mitaji wanaowalalia wananchi wa mkoa huu.
Pia viwanda vingi vinatakiwa kufufuliwa -- nakumbuka vichache tu ambavyo vimekufa kifo cha mende kama kiwanda cha nyuzi na SIDO ambapo vijana waliweza kupata ajira miaka hiyo. Pia kufufua vyuo ambavyo vimekufa au kama vipo basi ni mahututi kama chuo cha Nyuki; chuo cha ardhi; Reli na hata kile chuo cha kihistoria cha Uhazil.
Mwisho natoa wito kwa wasomi na wazawa wa Tabora ambao ni wengi sana wapo katika taasisi za elimu ya juu, waangalie ni namna gani wanaweza kusaidia kukuza uchumi wa mkoa wao wakisaidiana na sisi wazawa wengine tulioko huku, maana wengi kaka zangu wameloea huko pwani na kaskazini hawataki kurudi kabisa kusaidia mipango ya maendeleo katika sehemu walizotoka hasa katika sekta za kilimo, elimu na ufugaji ambazo ndizo pekee za kumkomboa mwananchi wa kipato cha chini kabisa