Tabora iliyodidimia inahitaji kuinuliwa... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tabora iliyodidimia inahitaji kuinuliwa...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by mapambazuko, Oct 6, 2010.

 1. m

  mapambazuko Member

  #1
  Oct 6, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 23
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani sijui wenzangu kama mmepata kung'amua kitu hiki mkoa wa Tabora ni kama vile umekufa.

  Kwa jinsi nionavyo mimi licha ya wakazi wake kuwa na chakula pengine cha kutosha lakini miaka nenda rudi nikipita hapo sioni mabadiliko utafikiri vile hakuna wazawa waliokwenda shule mpaka leo mbavu za mbwa ziko katika mji tatizo liko wapi?

  -kwa wazawa wenyewe?
  -serikali?

  Kwa kuwa kama ni viongozi waliosoma na kuwepo katika sytem hii ya serikali wapo tangu kitambo mbona kunadorola yaani huwa napata maswali mengi kichwani?

  Hebu nisaidieni hasa ninyi wazawa wa Tabora na wenye kuufahamu vizuri unastahili kuwa kama ilivyo? [Ukizingatia kuwa ni mkoa wa kihistoria katika harakati za uhuru wa nchi hii]
   
 2. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #2
  Oct 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Ehhhh weeeeee,

  Msula eve hihihiiiiiiiiiii
   
 3. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #3
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Kweli mkoa huu una utajiri wa historia kama kuna wabunifu na watafiti wazuri ungekuwa upo mbali katika kiwanda cha utalii.
   
 4. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #4
  Oct 6, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Tabora utatalii nini? Matoborwa?

  Dhahabu yenyewe wanauza akina Junius kwa kuipeleka Uarabuni.

  Na kesho wanadai hawataki Muungano.......

  Ngoja tubaki tu tunajilia ugali wa Nsansa na kuichagua CCM yetu. Kesho tunaamkia Kihembe ........
   
 5. Junius

  Junius JF-Expert Member

  #5
  Oct 6, 2010
  Joined: Mar 11, 2009
  Messages: 3,183
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 133
  Sikonge,
  Wewe jifanye kama mwehu tu...utakuwa mwehu kweli shauri yako!!!
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2010
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0

  Hahaha Sikonge umenikumbusha mbali sana enzi nipo Tabora Boys. Tulikuwa na rafiki yetu mmoja yeye alikuwa anakuwa anatukaribisha kwao maeneo ya Kanyenye au Ng'ambo kama sijasahau, nakumbuka tulikuwa tunapikiwa nsansa za karanga aisee unsahau ule ugali wa dona la maharage ya Alexander Ndeki (Nasikia huyu ni marhum kwa sasa).

  Nilichokiona pale Tabora ni kimoja, mzunguuko wa pesa ulikuwa mdogo sana, kingine kama nilivyokuwa wakati huo vibanda vya kahawa vilikuwa vingi ikiingia jioni. Mazungumzo makuu sehemu hizi yalikuwa ni kujadili watu wenye mafanikio na jinsi walivyofanikiwa na hata kusema yule mtoto amezaliwa tunamuona.

  Kuna jamaa aliwahi kuniambia siku za karibuni kuwa miji yote iliyokaliwa na waarabu kwa muda mrefu wakazi wake wanakuwa hawana wasiwasi na maendeleo. Ila kwa mji wa Tabora kikubwa kinacho changia ni land locked region inayotegemea zaidi reli ya kati zaidi ya barabara kama Kigoma. Elimu katika mikoa hii ukiangalia wanaosoma zaidi ni wageni zaidi ya wakazi ambao haipi kipaumbele sana. wanaojenga kwa wingi Tabora ni watu wa kuja kama wachaga n.k ambao ni wafanya biashara maarufu hapo Tabora. Wahindi wao wapo ila wanaishi kwenye nyumba za Msajili.

  Tabora ina neema nyingi sana kama asali, tumbaku, karanga na mazao mengi ya chakula, tabu kubwa ni soko kwani wengi wa wakulima wanajikuta wanadhulumiwa na wafanyabiashara wajanja ambao hununua kwa bei za kutupa kutokana na ufahamu mdogo na soko kuwa gumu. Majority ya nyumba za katikati mji ni za biscuit kwani ndiyo hasa wanazokaa wana-Tabora asilia ambao ndiyo kuna vibanda vingi vya kahawa na mihogo ya makopa na karanga + Kashata.

  Kuna wakati kulikuwa na dhana ya kwamba vijana wazawa wanaofanikiwa na kuwasaidia wazazi wao basi huwa wanashughulikiwa kisayansi ya Sheikh Yahya na kupoteza maisha hivyo wengi kujikuta wanaogopa kuendeleza miji yao kwa hofu ya kushughulikuwa kienyeji.

  Tatizo lingine nililoliona pale Tabora ni watu kuridhika na maisha hasa kama ana uhakika wa asubuhi kunywa chai na makopa, mchana ugali na mlenda/kihembe/nsansa/kauzu/ngege/kisamvu/mchunga/ et al. Kwa ujumla uswahili ni mwingi sana Tabora hakuna tofauti na Tanga/ Kigoma/ Bagamoyo/ Plus mikoa yote yenye influence ya mwarabu.

  Kuna hitajika sana elimu katika mikoa hii ili kushindana na hali halisi ya mentali za wakazi wake ambao kila kitu hukimbilia kujifariji kuwa KAZI YA MUNGU.
   
 7. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #7
  Oct 7, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,947
  Likes Received: 2,093
  Trophy Points: 280
  Hayo ni matunda ya uhuru na mafanikio ya CCM!
   
 8. Yegomasika

  Yegomasika JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2010
  Joined: Mar 21, 2009
  Messages: 7,149
  Likes Received: 23,840
  Trophy Points: 280
  Hivi Tabora na Shinyanga nani mwenye unafuu. Kwani Shinyanga nayo du haibadiriki hata kidogo!.
   
 9. Utingo

  Utingo JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 15, 2009
  Messages: 7,121
  Likes Received: 185
  Trophy Points: 160
  mkuu hebu nenda ilulunguru kwa akina lipumba ukaone. mkoa wa tabora unasikitisha sana. Miaka ya sabini na themanini tuliokulia vijijini na miji midogo katika mkoa huyo tunakumuka vijiji na miji hiyo ilikuwa alive, lakini sasa hivi ukipita katika miji na vijiji hivyo unaona mauti tu ya miji na vijiji. Kila mtu anakimbilia mjini na hili ni tatizo la nchi nzima.
  Bahati mbaya watawala (CCM) hawalioni hili kwani bongo zao zimeshagandamana.
   
 10. birungi

  birungi JF-Expert Member

  #10
  Oct 7, 2010
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 388
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  doh,
  naona tatizo ni viwanda vya uzalishaji hakuna,na vilivyokuwepo vimefungwa kama kiwanda cha nyuzi na hata kile cha tumbaku.
  enzi hizo hivi vilisaidia kuinua uchumi wa tabora sio kama sasa.kwa sasa hivi wanategemea tu kilimo hicho cha tumbaku na inauzwa mikoa jirani wakati hapo kiwanda kilikuwepo,na zinanunuliwa kwa bei ya chini.
  wengi wa wazawa wa tabora hawajapata elimu ya kutosha,japo mashule yapo mengi ya kutosha.wengi ni wageni wanasoma na kuondoka.anyway wafufue viwanda kwanza wataamka na kusimama taratibu.
  kitu kingine,ushauri kwa wawekezaji,tabora ina eneo la ardhi kuubwa sana ambayo ipo tupu na inahitaji kuendelezwa.mfano kule wangepeleka viwanda kama vitatu tu vingetosha sana,kama kiwanda cha vinywaji kama juis na maji,pia viwanda vya vyakula as long mpunga na mahindi ni zao linalolimwa mkoani hapo.
  si mbaya pia baadhi ya ofisi za serikali zikahamishia huko makao makuu.ni matumaini yangu wafanyakazi wake wengi watakaokua huko kufanya kazi watapaboresha zaidi.
   
 11. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #11
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Tabora tunatoa Asali wingi, Mbao bora za Mninga kwa wingi
  Tuna Hifadhi za taifa - Tabora ni miongini kwa mikoa ya kitalii
  Tuna ardhi yakutosha unutilized - leo hata nikitaka hekari 100 napata for free you cant believe.
  Tuna Kilimo cha Tumbaku kama zao kuu la biashara

  Tabora hasa wilaya ya Sikonge nafikiri ndiyo ipo kwenye hali mbaya sana kiuchumi siwezi kubisha. Nikifika nyumbani ugali kwa nsansa na swalu, majani ya muhongo na maboga kwa wingi..Tunawakaribisha.
   
 12. d

  dotto JF-Expert Member

  #12
  Oct 7, 2010
  Joined: Sep 29, 2010
  Messages: 1,720
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  ............umwinyi........
   
 13. StaffordKibona

  StaffordKibona JF-Expert Member

  #13
  Oct 7, 2010
  Joined: Apr 21, 2008
  Messages: 671
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nyie wenyewe si mliwasikia wagombeaji juzi kwenye Mcahakato kuna la maana pale?
   
 14. M

  Malila JF-Expert Member

  #14
  Oct 7, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,411
  Likes Received: 737
  Trophy Points: 280
  Sehemu gani Tabora ambapo naweza kujipatia eka 100 kwa ubwete? Hapo mahali panalimika?
   
 15. Kiroroma

  Kiroroma JF-Expert Member

  #15
  Oct 7, 2010
  Joined: Feb 6, 2009
  Messages: 368
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 45
  Hofstede kumbe wewe ni mwana TS ,Mambo yote ya umwamba na mbarara unayajua,Sasa umesahau kuwa Tabora ni mji wa kale sana hata mambo ya magoti yalikuwa kule Ngoma Sakasi
   
 16. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #16
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Na 'usula wakwe'; amesema kweli lakini!
   
 17. Mtoboasiri

  Mtoboasiri JF-Expert Member

  #17
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 6, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 94
  Trophy Points: 0
  Natofautiana na wewe kwa kusema wenyeji hawajali elimu - HAWANA UWEZO wa kusomesha. Kwa suala la wageni kujenga hilo si la Tabora peke yake (wazaramo wangapi wenye nyumba DSM, au Waluguru wangapi Morogoro mjini n.k n.k n.k??)

  Jamaa wa Kigoma hushangaa wakifika Tabora mjini, - what does this say on Kigoma??

  CCM imelemaza watu kifikra, tukiwatoa mabadiliko yakuja.
   
 18. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #18
  Oct 7, 2010
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Junius mtani wangu (kama Mzenji nina imani hiyo) pamoja na wachangiaji wengine,

  Nipeni muda kidogo na nitakuja na maoni yangu kwa ujumla juu ya Sikonge.

  Malila, Wilaya ya Sikonge ina ardhi nyingi na kubwa saaana. Angalia kwenye Google Earth maeneo kama Pangale, Kasisi, Tutuo kwenda hadi Mole, vuka Sikonge na nenda chini kama waenda Mbeya na fika eneo jingine walilo-ZOOM yaani waweza kuona kwa karibu hadi nyumba na utaona vijiji kama vilivyo kama km.40 kutoka Sikonge. Huko utaona maeneo mengi na makubwa saaana. Yaani hata ukitaka km.10 kwa 10 bado utazipata bila wasiwasi na hakuna wa kukuuliza.

  Tatizo la Sikonge na Tabora kwa ujumla ni USAFIRI na wakati wa Masika, maeneo hayo hadi kufika huko Itunda ambako Kikwete amekuwa Rais wa kwanza kufika, huwa hayafikiki. Hata Kikwete mwenyewe gari lilikwama na ikabidi watume Helcopiter imfikishe huko. Wakati wa Masika huwa ndiyo mabasi kama SHAKIRA linafika.

  Wasomi kama Balozi Chokara, ndiyo wanatoka maeneo hayo. Pia jamaa wengine wengi tu humu wanatoka maeneo hayo kwani hivyo vijiji vilivyoanzishwa wakati huo miaka ya 70, kama Usunga nk chini ya Uhamishaji watu wa Mzee Luswetula (asante Keil kwa kunikumbusha huyu Mzee) ulifanya mkusanyiko mkubwa sana wa watu na ushindani shuleni ukawa mkubwa. Kijiji hiki kilikuwa na sifa ya kupasisha wanafunzi wengi karibu kila mwaka na mara nyingi wakiizidi hata Sikonge yenyewe pamoja na kuwa na shule mbili za Msingi.

  Tatizo la Sikonge, ni tatizo common kwa Tabora nzima.

  MALILA: Angalia pia sehemu inaitwa Tumbi, ni kama unaenda Urambo na karibu sana na Tabora Mjini, na baada ya hapo nenda Kaskazini hadi utaiona kambi ya JKT ya Msange. Hii kambi peke yake kuna misitu mikubwa sana ambayo zamani yalikuwa mashamba ya katani ya Mzungu. Huyu Mzungu alishindwa kutamka Msange na akawa anasema Masange. Ndiyo maana zamani kambi pia ilikuwa ikiitwa Masange na baadaye ndiyo ikabadilishwa na kuitwa Msange (Mkute). Kutoka hapo unaenda hadi huko kijiji cha Mbola, ni msitu mkubwa sana. Hahaaaaa, kijiji cha Mbola kuna mama mmoja ambaye anaishi kwa kupewa Msaada na Mwanamziki Maarufu na Producer aitwaye John Legends. Ukiingia kwenye ukurasa wake, utaona picha zake akiwa Mbola na ukisikia katua Tz basi ujuwe kaenda kumtembelea mama yake wa Mbola. Vuka Msange nenda hadi maeneo lilipo bwawa la Igombe kama sikosei, na vuka Igombe, huko kote ni msitu mzito sana wa Miyombo na safi sana kwa kufuga asali..........

  Ntaandika zaidi baadaye kama nilivyoahidi na nafikiri KEIL na Mkuu Kichuguu watasaidia na wao maoni yao. Nitajadili zaidi sababu ambazo naona zimesababisha hali iwe hivi na nini kinaweza kufanyika maana si kulaumu tu ila pia kujaribu kutoa maelezo nini kifanyike.
   
 19. Guma Mlugaluga

  Guma Mlugaluga Member

  #19
  Oct 7, 2010
  Joined: Aug 20, 2008
  Messages: 98
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13

  Teheteheteheteheteheteheteh, kwiswe kumanyile icho wamuwila!, duh!
   
 20. ELNIN0

  ELNIN0 JF-Expert Member

  #20
  Oct 7, 2010
  Joined: Nov 26, 2009
  Messages: 3,771
  Likes Received: 221
  Trophy Points: 160
  Mlila nifuate Dec twende wote nikakupe Eneo. panalimika inategemea unatumia nyezo gani na kilimo kipi.
   
Loading...