Mtoboasiri
JF-Expert Member
- Aug 6, 2009
- 5,101
- 1,948
Msibeze "maendeleo" ya Tabora bana!
Tabora,
Tatizo lenu ni watu wa majungu, hamtaki kubadilika
Hizo barabara haziji kama mvua, ni mapambano ya kudai haki yenu ya msingi, kama mnauza tumbaku kodo inakwenda wapi?
Na hao wawakilishi wenu madiwani na wabunge wanawasaidiaje?
Kama mliowachagua mnaona hawana msaada, piga chini kwenye uchaguzi
Ni kweli nimekaa Tabora na nimejionea mwnywe kale ka mkoa ni kabaya kuanzia na barabara mpaka ujinga,ftina na majungu,hawa watu ni hatari sana kwa fitina na ubnafsi, na bado naamini ni miaka mingi itakayopita paspo Tabora kupata maendeleo
Unalosema ni kweli mwana JF, mimi nilienda mwezi Dec, 2011 kuna barabara ya kutoka Itigi to Tabora ni mbaya sana. Wanadai barabara ya rami wameanza lakini kinachofanyika hakionekani. Tunachoomba ni wabunge wa maeneo husika wasilale wafanye kazi ili mkoa wetu upate maendeleo kama mikoa mingine. Kama ilani ya CCM inavyosema kuwa barabara zote zinazounganisha mkoa kuwa na rami, inakuwaje mikoa mingine bado? Tafakari na chukua hatua!
Kutoka Nzega kwenda tabora mjini, ile barabara haieleweki kama ni barabara au nini kinjia. Nilipita 2 years ago, sijui kama walishabadilisha hata hizo changarawe. Tabora wanakalia majungu na kunywa togwa. Wazinduke wananchi!
Hivi, ni lini mtaacha kuwapa magamba kura zenu, ndio faida zake hizoJamani barabara za mkoa wetu wa Tabora zinatisha. Mpaka sasa hakuna barabara hata moja yenye rami ambayo inaingia mkoa wa Tabora. Chama changu cha Chadema mko wapi? Waamsheni wananchi wa Tabora kwani ni waelewa. Siku zote wanyamwezi na wasukuma ukiwaelimisha wakaelewa watakuunga mkono. Chadema nendeni Tabora kwani waanzilishi wa vyama hakina Fundikira, Mapalala na Kasela Bantu wote walikuwa ni wenyeji wa Tabora.
Wana JF muwe huru kuchangia kwenye thread ili mkoa wa Tabora uweze kuinuliwa. Kwasababu wanasiasa wenye maamuzi nao wanatembelea mtandao wetu wa JF. Nahisi kuna kitu kitafanyika.
pale amemchaguliwa mbunge wa Simba sio mbunge wa Tabora,kwa masuala ya maendeleo ya wanatabora hayamuhusu ndo maana kila siku kwenye tv akiangaikia mara kumpeleka contractor wa jengo lao mahakamani mara kakamata tani 1 ya jezi za Simba.Wacha tuipatepate wanatabora kwa kuendekeza magambaz.
Tabora ni ngome ya CCM. Hata mfanyeje haitahamia CDM. Mmeona Igunga. Mtapoteza nguvu nyingi na pesa ambazo mngetumia kwingine. Ngome zingine za CCM ni Lindi, Mtwara, Unguja na Pwani.
Msipende kujua ni kwa nini iko hivyo. Inatokana na nchanganyiko wa vitu vingi na haviko systematic. Hata Marekani kuna Red States na Blue States.
CDM iwekeze zaidi kwenye maeneo yasiyo ngome za CCM. eg Mwanza, Shinyanga, Musoma, Mbeya, Arusha etc
Jamani barabara za mkoa wetu wa Tabora zinatisha. Mpaka sasa hakuna barabara hata moja yenye rami ambayo inaingia mkoa wa Tabora. Chama changu cha Chadema mko wapi? Waamsheni wananchi wa Tabora kwani ni waelewa. Siku zote wanyamwezi na wasukuma ukiwaelimisha wakaelewa watakuunga mkono. Chadema nendeni Tabora kwani waanzilishi wa vyama hakina Fundikira, Mapalala na Kasela Bantu wote walikuwa ni wenyeji wa Tabora.
Wana JF muwe huru kuchangia kwenye thread ili mkoa wa Tabora uweze kuinuliwa. Kwasababu wanasiasa wenye maamuzi nao wanatembelea mtandao wetu wa JF. Nahisi kuna kitu kitafanyika.