Tabora iliyodidimia inahitaji kuinuliwa...

Mkuu Malila,

Nilishapiga simu mara kibao na jibu huwa "ahhh mie sijui....." Mtu pekee ambaye alikuwa anijulishe ni binamu yangu ambaye ni ajabu kuwa ni kipindi sasa hapokei simu au huwa simpati. Si kuwa nimesahau hapana, nakumbuka sana. Vipi Dr. Yongolo ulifanikiwa kumuona? Vipi yule Mkuu mwingine nilikujulisha?

Hiyo misitu, mainly inaota miti ya Miyombo. Kuotesha miti Tabora ni rahisi sana ila inabidi kuwa na miti inayokuwa taratibu. Ukileta ya Ulaya au sehemu kavu, basi itakufa kwa mvua au kukua haraka sana ila quality ya mbao itakuwa mbaya kama miti ya Mikaratusi ya Tabora, myepesii...
KWA MITI: Jaribu kuwaona Chuo Cha Kilimo Tumbi wanaweza kukupa msaada mkubwa zaidi. Sijui kama kuna chuo cha misitu na ufugaji nyuki Tabora, hawa pia wanaweza kuwa msaada.

Nikifanukiwa tu basi ntakurushia ujumbe:
Ktk ardhi hiyo ni miti aina gani inamea?,hasa ya kigeni (exortic trees), niliwahi kuomba msaada wa kujua kiwanda walau kidogo cha kusindika asali huko kwenu Tabora,mkaahidi kuni-PM mpaka leo kimyaaa.
 
Angalia hizi anwani kama bado zinafanya kazi, Tumbi wanaweza kuwa msaada mkubwa sana.



1. ZONAL DIRECTOR FOR RESEARCH AND DEVELOPMENT (WZ)
TUMBI AGRICULTURAL RESEARCH INSTITUTE
P.O.BOX 306,
TABORA – TANZANIA.
TEL. 0787 604142
EMAIL: zdrdwz@yahoo.com
bbsilanga@yahoo.com


2. Gerson Nyadzi
Tumbi Agricultural reserch and Development Institute
P.O. BOX 306 Tabora Tanzania
Fax: +255 26 260 4907
Email: bnyadzi@hotmail.com


3. Raphael Luhende
Tabora Miombo Woodland reserch centre
P.O Box 1960 Tabora, Tanzania
Email: rluhende2003@yahoo.co.uk
Tel. +255 26 4540 Fax: +255 26 4906


Watu wa Tumbi wanaweza kuwa msaada mkubwa sana kwako zaidi yetu sisi maana wao ni Wataalamu.
 
Mkuu Malila,

Nilishapiga simu mara kibao na jibu huwa "ahhh mie sijui....." Mtu pekee ambaye alikuwa anijulishe ni binamu yangu ambaye ni ajabu kuwa ni kipindi sasa hapokei simu au huwa simpati. Si kuwa nimesahau hapana, nakumbuka sana. Vipi Dr. Yongolo ulifanikiwa kumuona? Vipi yule Mkuu mwingine nilikujulisha?

Hiyo misitu, mainly inaota miti ya Miyombo. Kuotesha miti Tabora ni rahisi sana ila inabidi kuwa na miti inayokuwa taratibu. Ukileta ya Ulaya au sehemu kavu, basi itakufa kwa mvua au kukua haraka sana ila quality ya mbao itakuwa mbaya kama miti ya Mikaratusi ya Tabora, myepesii...
KWA MITI: Jaribu kuwaona Chuo Cha Kilimo Tumbi wanaweza kukupa msaada mkubwa zaidi. Sijui kama kuna chuo cha misitu na ufugaji nyuki Tabora, hawa pia wanaweza kuwa msaada.

Nikifanukiwa tu basi ntakurushia ujumbe:

Kwa Dr Yongolo sikwenda,nilibanwa vibaya mpaka leo,huenda week ijayo nikapata nafasi ya kutosha. Yule mkuu mwingine aliniahidi kunijulisha ndo namsubiri.

Hawa watalaam nitawatafuta ili wanisaidie kujua miti stahili ktk ardhi ya Tabora,lakini nina hakika Mitiki itafanya vizuri. Ngoja niwaone kwanza.

Nakushukuru sana mkuu.
 
Most of the folks in Tabora are lazy!
All you cherish is umwinyi, and pretending you are Arabs while the reality is you are not, and will never be. You worship witchcraft. You send your kids to Madrasat schools instead of formal education.
 
Most of the folks in Tabora are lazy!
All you cherish is umwinyi, and pretending you are Arabs while the reality is you are not, and will never be. You worship witchcraft. You send your kids to Madrasat schools instead of formal education.

Dude, you seem to be a racist, judging pending on your posts, you'll soon be banned, if you can, change your attitude. Take it or leave it!
 
Most of the folks in Tabora are lazy!
All you cherish is umwinyi, and pretending you are Arabs while the reality is you are not, and will never be. You worship witchcraft. You send your kids to Madrasat schools instead of formal education.

whats so special about being an arab? we muhindi wa wapi?
 
Angalia hizi anwani kama bado zinafanya kazi, Tumbi wanaweza kuwa msaada mkubwa sana.



1. ZONAL DIRECTOR FOR RESEARCH AND DEVELOPMENT (WZ)
TUMBI AGRICULTURAL RESEARCH INSTITUTE
P.O.BOX 306,
TABORA – TANZANIA.
TEL. 0787 604142
EMAIL: zdrdwz@yahoo.com
bbsilanga@yahoo.com


2. Gerson Nyadzi
Tumbi Agricultural reserch and Development Institute
P.O. BOX 306 Tabora Tanzania
Fax: +255 26 260 4907
Email: bnyadzi@hotmail.com


3. Raphael Luhende
Tabora Miombo Woodland reserch centre
P.O Box 1960 Tabora, Tanzania
Email: rluhende2003@yahoo.co.uk
Tel. +255 26 4540 Fax: +255 26 4906


Watu wa Tumbi wanaweza kuwa msaada mkubwa sana kwako zaidi yetu sisi maana wao ni Wataalamu.

Inaonekana hizo mail address mbili(highlighted) haziko hai,ila nyingine za juu ziko hai. Ngoja tuone majibu yake.
 
Yeah Wachangiaji.

Wee Hosftede, mie siyo Mkonongo bana. Wala Magando ni Wakonongo wanaotoka Kitunda.

Watu wa kitunda ni kati ya Mnyamwezi na Mfipa / Mnyakyusa. Wanavyoongea kwa mfano neno Hivyo hivyo, Wanyamwezi wa Sikonge tunasema "Vyenivyo", Wasukuma wanasema "Shenisho" na Wakonongo kwa kukaa karibu na Wanyakyusa wanasema "Fyenifyo.....".

Magando, hahahaa kwa wasiofahamu ni kuwa kuna mti unaitwa Mgando na huwa kuna hawa Catapiller wanapenda sana kula majani yake na Wakonongo (baadhi ya Wanyamwezi pia) huwa wanaenda na kuukata mti (Hapa wanafanya makosa) au huwa wanapanda na kutikisa matawi na wale Caterpiller huwa wanaanguka na wanawachukua na kuwakaanga. Kama sikosei watakuwa na radha kama Senene au Kumbikumbi...

Niliporudi kutoka mjini (niliishi nikiwa mtoto) niliambiwa kuwa watu wanakula. Bahati nzuri kwetu tulikuwa hatuli maana ingelikuwa kasheshe kunilazimisha kula. Ila nilisoma na kusikia makala moja kwenye CCN juu ya kisa kwamba Wazungu wanaagiza kwa wingi sana haya Magando. Wengine wameyapenda na wengine wameyachukia. Ila yana soko sana.

Caterpillar12.jpg


Nina mpango wa kuja kuwa napita vijijini Sikonge nzima na kuwaambia kuwa siku kama wameshuka kumbikumbi, basi wawakamate wengi na wanipigie simu na mie siku hiyohiyo ninaingia na kuwabeba. Ntawakaanga na kuwatunza vizuri na baadaye kuja JF, Tanzanet, Michuzi Blog nk nk na kuwauza. Wahaya na Waganda wanaoishi nje, watanunua hata kwa dola 200 kilo, hihihiiiii ..... Elnino, Kichuguu na Keil msinicopy.
Kwa Wanyamwezi ntawatumia (Matini) mchwa wa kwenye Kichuguu. Pia ntakuuzieni ule uyoga wa Bunsolele, teteteteeeeee :)
Na kwa makabila yoote, ntauza pia kumbikumbi. Mnaonaje hii biashara? Kila kitu kitakuwa kwenye EBAY, hahahahaaaaa na malipo kwa PAYPAL na Mkuu wangu Mwakalinga atakusanya pesa yangu na kunitumia........

Jamani, makala yangu bado naandika.

Hahahaha, umenukumbusha uyoga hivi bunsolele si ndiyo ule mdogodogo sana, kuna uhima huu unaota kwenye vichuguu, umpalala. Halafu kuna matunda pori kama mantonga, ndati, ntalali, mbuguswa, nsalasi, kuna yale matunda flani machachu sana walikuwa wanayaita magogonti, zambarau, nkuni.

Halafu nasikia chuo cha ufugaji nyuki kilihamishiwa Arusha, sijui nani aliyetoa maamuzi ya ajabu namna hiyo, nyuki wafugwe Tabora kwa wingi chuo kiwe arusha, haya ndiyo mambo yanayoli-cost Taifa watu wanafanya maamuzi kisiasa zaidi badala ya kuangalia masilahi ya Taifa. Kuna viongozi wapo tayari hata migodi yote ihamishiwe kwenye mikoa yao ya asili kama hilo lingewezekana.

Sikonge na wanaoijua Tabora kuna mboga fulani inaitwa mswalu mnaifahamu?
 
Mkubwa, ule uwanja wa Ali hassan mwinyi kweli hakuna mwananchi wa Tabora ambaye hakushiriki - nakumbuka hadi Vijijini michango ilipita mwenye kuku, bata, mbuzi ili mradi uwanja uishe. Wenzetu waliokuwa Tabora mjini wasioweza kutoa pesa basi wajijitolea kufanya kazi ya ujenzi - kufyatua matofali, kubeba mchanga, kuchanganya simenti n.k

Kinachosikitisha uwanja sasa hvi ni pango la wezi, umekatika vipande vipande -usimamizi mbovu nguvu ya wananchi imepotea bure.

Ile timu yetu iliyokuwa inawika ya Mashujaa wa Unyanyembe yaani Milambo, inasuasua - nakumbuka enzi hizo kuna kijana alikuwa anaitwa Quresh Ufunguo na yule number Tano ( Wanyawezi wanapenda kuita Dala ) Yule alikuwa Bubu Jina la uchezaji alipachikwa "Kwasakwasa" Ilikuwa moto wa kuotea mbali.

Wakuu sasa nakumbuka home sana...

Mkuu ile timu naikumbuka ilibaki kidogo ichukue ubingwa wachezaji ninaowakumbuka ni Feruzi Teru, Wastara baribari, Bubu, Quresh ufunguo, Hamisi Macho(huyu nina uhakika ni marhumu sasa)
 
Cha msingi hapa ni kuanzisha research groups ambazo zitadeal na mikoa moja kwa moja kubainisha fursa zilizopo kila mkoa na kuanzisha mikakati mahususi. Angalia pale manyara/babati wana viwanda vya kusindika mafuta ya alizeti, nadhani walibaini mapema wakaamua kuwekeza zinawasaidia wakazi wa pale. Tabora na mikoa mingine inabidi ifanyike hivyo hivyo itasaidia watu kutokimbilia mjini wakijua wanafuata maisha bora kumbe ni ubakaji tu.
 
tabora mbona imeoa watu wengi tu wapo hapo mjini? na wengine ndio wamejiishia tu? sema wengi hawakutumia nafasi zao kuuendeleza mji wa tabora kutokana na tatizo la usafiri
zaidi ya majina yaliyo tajwa kama el-mamry, wapo akina kapya, mfalila, mdachi, inza?, mwanukuzi, na wengineo wengi tu inabidi muanzishe kama development coordinating commitee, wengine wapo tra, bot, jeshi, polisi nk, tatizo la watu wa tabora ni kukosa mashirikiano kati yao wenyewe, na kudharauliana na jingine katika suala binafsi ni watu kukosa mwamko wa maendeleo-umwinyi, kama ilivyo bagamoyo, kigoma, lindi, tanga-. kinacho saidia tanga ni uwepo wa bandari na barabaram na kinacho saidia kigoma ni biashara na nchi jirani zaire, na burundi.
hizo barabara kwenda mbeya, kigoma, mpanda, nzega ndio ufunuo wa mkoa wa tabora na mashrikiano kati ya watu katika vitu vya maendeleo
 
Jamani barabara za mkoa wetu wa Tabora zinatisha. Mpaka sasa hakuna barabara hata moja yenye rami ambayo inaingia mkoa wa Tabora.

Chama changu cha Chadema mko wapi? Waamsheni wananchi wa Tabora kwani ni waelewa. Siku zote wanyamwezi na wasukuma ukiwaelimisha wakaelewa watakuunga mkono. Chadema nendeni Tabora kwani waanzilishi wa vyama hakina Fundikira, Mapalala na Kasela Bantu wote walikuwa ni wenyeji wa Tabora.

Wana JF muwe huru kuchangia kwenye thread ili mkoa wa Tabora uweze kuinuliwa. Kwasababu wanasiasa wenye maamuzi nao wanatembelea mtandao wetu wa JF. Nahisi kuna kitu kitafanyika.
 
Unalosema ni kweli mwana JF, mimi nilienda mwezi Dec, 2011 kuna barabara ya kutoka Itigi to Tabora ni mbaya sana. Wanadai barabara ya rami wameanza lakini kinachofanyika hakionekani. Tunachoomba ni wabunge wa maeneo husika wasilale wafanye kazi ili mkoa wetu upate maendeleo kama mikoa mingine. Kama ilani ya CCM inavyosema kuwa barabara zote zinazounganisha mkoa kuwa na rami, inakuwaje mikoa mingine bado? Tafakari na chukua hatua!
 
Mikoa yote maskini na walio nyuma kimaendeleo ni ngome ya magamba.fikra zao zimetawaliwa na magamba ndio maana hata wabunge wao hawajali
 
pale amemchaguliwa mbunge wa Simba sio mbunge wa Tabora,kwa masuala ya maendeleo ya wanatabora hayamuhusu ndo maana kila siku kwenye tv akiangaikia mara kumpeleka contractor wa jengo lao mahakamani mara kakamata tani 1 ya jezi za Simba.Wacha tuipatepate wanatabora kwa kuendekeza magambaz.
 
wabunge wao wanafanya nini??????????je kuna madiwani?????????ni wa chama gani??????????wananchi hawalioni hilo??????????
 
Tabora imeshindwa kuendelea kutokana na siasa za majungu,fitina na usanii,ongeza ujinga na umasikini,Tabora imebakia ngome imara ya magamba!
 
Ni kweli nimekaa Tabora na nimejionea mwnywe kale ka mkoa ni kabaya kuanzia na barabara mpaka ujinga,ftina na majungu,hawa watu ni hatari sana kwa fitina na ubnafsi, na bado naamini ni miaka mingi itakayopita paspo Tabora kupata maendeleo
 
Back
Top Bottom