Mimi hii ndio principle yangu namba ngeni huwa sipokei kabisa.
Huu utaratibu naupenda na siuachi kamwe.
Najiambiaga kama una la muhimu sana kuniambia utanitumia message.
Na kama hujatuma message najua huyu hakuwa na jambo la msingi ndio maana hajanitumia message.
Ila kwa ujumla kabisa sipendi kupokea simu kabisa, kuna siku ntapokea na tutaongea vizuri ila kuna siku sipendi kupokea kabisa hata kama naijua namba yako.
Cha ajabu ukituma texts tutachati kabisa na nitaanza kutunga sababu za kukwambia kwanini sikupokea simu yako.
Japo ni tabia ya ajabu kabisa yaani unaona kabisa simu inaita na jina unaliona lakini badala ya kupokea unaanza kutunga uongo wa kudanganya kwanini hukupokea.
Na ikinilazimu sana nitakupigia huku nikiomba kimoyomoyo usipokeee yaani ikiita tu mara 2 nakata, kuweka ushahidi kuwa hata mimi nilikupigia[emoji23][emoji23][emoji23][emoji1787][emoji1].
Ila kuna watu wanaudhi sana wanaweza kukupigia simu saa 12 asubuhi alafu hawana hata cha maana kukwambia.
Mimi naanza kupokea simu kuanzia saa tatu asubuhi (9:00AM) kwa siku za kazi na saa tano(11:00AM)siku za WeekEnd na Public Holiday.
Sio dharau wala kiburi ila ndio Principle yangu tu japo najua kuna wakati nakosea sana kufanya hivi, ila kwenye maisha lazima uwe na Principle zako na uweze kuzisimamia.