Tabia ya kutopokea namba ngeni/namba mpya

Tabia ya kutopokea namba ngeni/namba mpya

Nimepokea simu nyingi tu za kuniita kwenye interview. Nyingine unapigiwa kama leo hivi interview ni kesho yake asubuhi. Nyingine za kunijulisha kuwa nimepewa kazi baada ya interview. Nyingi tu. Sasa ningejifanya kuwa sipokei namba nisiyoijua?
Kama wewe ni muuza machungwa, pengine you have nothing to lose.
Mimi bana baada ya kugraduate kuna siku nilipigiwa simu na namba ngeni kama mara mbili nkapotezea.. baada ya hapo nikatumiwa message inayosema "This is UDSM calling.."

kila nkipiga ile namba haipokelewi kila nikipiga waapiii.. dah tumbo lilichafuka ghafla mana nilishaona nimebugi.
sasa sijui walikua wanataka waniajiri au wamenitaftia muajiri. siwezi kusahau ile siku.
 
Sidaiwi na mtu
Ila pia huwa sipendi kupokea namba ngeni

Sanasana...ntaflash auto reply kuwa anitumie msg tafadhali
 
Endeleeni kutopokea Simu kisa namba ngeni mtapishana na magari ya mishahara.

Kwani MTU ukishapokea Simu yake akianza mazinguzi si unakata kwani lazim umsikilize kila mtu???

Na kama je ni tatizo ambalo unahitajika wewe kulisolve???

Mimi naona ni ushamba,kujiona,dharau,kiburii,,acheni viburiii ipo siku mtarudi udongoni mkawe msosi wa finye finye!!
Inastajabisha mkuu
 
Mimi bana baada ya kugraduate kuna siku nilipigiwa simu na namba ngeni kama mara mbili nkapotezea.. baada ya hapo nikatumiwa message inayosema "This is UDSM calling.."

kila nkipiga ile namba haipokelewi kila nikipiga waapiii.. dah tumbo lilichafuka ghafla mana nilishaona nimebugi.
sasa sijui walikua wanataka waniajiri au wamenitaftia muajiri. siwezi kusahau ile siku.
Unaona sasa mpaka leo Hujajua walikuwa wanataka kukwambia nini?
 
Siku utapigiwa simu ya uteuzi uta igniore
Nadhani utafika muda nitaanza kupokea ila kwa sasa hapana kwa kweli.
Simu nyingi ni usumbufu tu,mtu anakosea namba unamuuliza nani naye anakuuliza wewe nani,
Mwingine kila siku ana namba mpya,
Wengine basi tu usumbufu na huwa sipendi kuongea na simu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusema kweli ata Mimi sio mpenzi wa namba ngeni madeni plus michango isiyo na kichwa Wala mguu.

Me napenda kukata na kumwambia mhusika anitumie mesage.
Mimi huwa sikati.
Naamini mtu Kama ana Shida kweli atanitafuta kwa message baada ya kuona simu haipokelewi.
Asiponitafuta kwa msg ndo imetoka hiyo.

Sina madeni,Sina ishu za kuombwa michango,Sina wapenzi.
Ni vile tu sipendi usumbufu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unapokea tu,namba ngeni,"wewe ndo fulani?,jumatatu uripoti kituoni".
"Kituo gani?"
"Kituo cha UDA kilicho karibu yako".

Piga ua huwa sipokei namba nje ya contact zangu.
 
Technology zipo why mtu uhangaike?
Caller id app inasaidia kujua Nani anakupigia..
Utajua Tu hii nipokee au hii sipokei
Aisee 90%ya app kwenye google store ni magumashi,,zingine haziapply huku Tanganyika,labda uwe europe
 
Siogopi kupokea simu yangu hata upige kwa namba ya nchi gani.

Nakumbuka mwaka 2014 niliomba kazi Tumbaku Morogoro, nikaambiwa nitapigiwa simu kwa ajili ya interview. Kila sehemu nilikuwa naenda na simu mpaka wakati wa kuoga.

Siku nikasahau kwenda nayo bafuni, na nilipokuwa nakaa ni uswahilini hasa Mazimbu Dark City wapangaji wanafungulia sabufa mpaka bati zinapiga kelele. Kuingia ndani nakuta missed call ya namba ya simu ya mezani kila nikipiga hakuna mafanikio. Ikabidi nimcheki jamaa niliyeomba naye ndio akaniambia wamepiga simu za interview.
 
Mimi hii ndio principle yangu namba ngeni huwa sipokei kabisa.
Huu utaratibu naupenda na siuachi kamwe.

Najiambiaga kama una la muhimu sana kuniambia utanitumia message.
Na kama hujatuma message najua huyu hakuwa na jambo la msingi ndio maana hajanitumia message.

Ila kwa ujumla kabisa sipendi kupokea simu kabisa, kuna siku ntapokea na tutaongea vizuri ila kuna siku sipendi kupokea kabisa hata kama naijua namba yako.

Cha ajabu ukituma texts tutachati kabisa na nitaanza kutunga sababu za kukwambia kwanini sikupokea simu yako.

Japo ni tabia ya ajabu kabisa yaani unaona kabisa simu inaita na jina unaliona lakini badala ya kupokea unaanza kutunga uongo wa kudanganya kwanini hukupokea.
Na ikinilazimu sana nitakupigia huku nikiomba kimoyomoyo usipokeee yaani ikiita tu mara 2 nakata, kuweka ushahidi kuwa hata mimi nilikupigia.

Ila kuna watu wanaudhi sana wanaweza kukupigia simu saa 12 asubuhi alafu hawana hata cha maana kukwambia.
Mimi naanza kupokea simu kuanzia saa tatu asubuhi (9:00AM) kwa siku za kazi na saa tano(11:00AM)siku za WeekEnd na Public Holiday.

Sio dharau wala kiburi ila ndio Principle yangu tu japo najua kuna wakati nakosea sana kufanya hivi, ila kwenye maisha lazima uwe na Principle zako na uweze kuzisimamia.
 
Back
Top Bottom