Tabia ya kutopokea namba ngeni/namba mpya

CHIBA One

JF-Expert Member
Nov 16, 2018
560
2,087
Kwenye maisha kila mtu kajiwekea principles zake na utaratibu wa Maisha.. Ni sahihi sana lakini Kuna vingine vinahitaji Utashi wa kibinadamu kung'amua Hasara na Faida zake.

Kuna watu wamejiwekea utaratibu kwamba Hata iweje, Basi Namba ngeni itapiga sana na kamwe hatopokea.. Sijui ni madeni au basi tu hataki lakini ndo alivyoniwekea.. Hii iko pande zote kwa Baadhi ya wanaume na Wanawake.. Wanawake wengi wanasema wao huepuka Usumbufu kwani mara nyingi huwa ni wanaume wakware wanaotaka penzi lao.

Dhana hii kwa upande mmoja ni sahihi.. Lakini Je, huoni haja ya kumsikia anayekupigia ni nani kabla huja ignore? Na unakuta wewe ni mfanyabishara, mfanyakazi na pengine Mtafutaji wa kazi ume apply huko na huko.. Sasa umepigiwa simu ya interview na hupokei unataka uje kumlaum nani?

Juzi Mtu wangu wa karibu Kapigiwa sana simu Kwa namba mpya na hakuipokea maksudi kabisa zaidi ya mara nne.. Huku akibetua mdomo "Wanaume bana huyu nae anataka kunisumbua tu" Lakini baadae kupitia Namba hyo hiyo akatumiwa Msg Kwamba Kaka yake kafariki kwa Ajali.. Ndo akaanza kutoa vilio kama punda mwenye Njaa

Wakati mwingine tuangalie misimamo yetu kama ina tija kwenye Maisha.
 
Mm mmoja wapo namba ngeni shida sana kuipokea... Vimeo vipo ila kwngu sio shida changamoto yangu mimi ni ndugu..... dah! Wanazingua hawa raia simu zao mda mwingi ni majungu kutaka tu kujua nowadays unaendelea na nini apate cha kusimulia ila wakati unaongea nae km MTU vile
 
Back
Top Bottom