Tabia ya kutopokea namba ngeni/namba mpya

Nimecheka sana.!
Afu mtu huna mawasiliano yake,unapokea ila anapata ujasiri wa kukuuliza wewe nani wakati kapiga yeye.Huwa nakata twa!
Mimi mtu akinipigia simu akiniuliza mimi ni nani, huwa namjibu kuwa hii sio simu ya mezani, hii ni simu ya mkononi na mimi nitambue kama mmiliki wa simu hii.
 
Kwenye maisha kila mtu kajiwekea principles zake na utaratibu wa Maisha.. Ni sahihi sana lakini Kuna vingine vinahitaji Utashi wa kibinadamu kung'amua Hasara na Faida zake.

Kuna watu wamejiwekea utaratibu kwamba Hata iweje, Basi Namba ngeni itapiga sana na kamwe hatopokea.. Sijui ni madeni au basi tu hataki lakini ndo alivyoniwekea.. Hii iko pande zote kwa Baadhi ya wanaume na Wanawake.. Wanawake wengi wanasema wao huepuka Usumbufu kwani mara nyingi huwa ni wanaume wakware wanaotaka penzi lao.

Dhana hii kwa upande mmoja ni sahihi.. Lakini Je, huoni haja ya kumsikia anayekupigia ni nani kabla huja ignore? Na unakuta wewe ni mfanyabishara, mfanyakazi na pengine Mtafutaji wa kazi ume apply huko na huko.. Sasa umepigiwa simu ya interview na hupokei unataka uje kumlaum nani?

Juzi Mtu wangu wa karibu Kapigiwa sana simu Kwa namba mpya na hakuipokea maksudi kabisa zaidi ya mara nne.. Huku akibetua mdomo "Wanaume bana huyu nae anataka kunisumbua tu" Lakini baadae kupitia Namba hyo hiyo akatumiwa Msg Kwamba Kaka yake kafariki kwa Ajali.. Ndo akaanza kutoa vilio kama punda mwenye Njaa

Wakati mwingine tuangalie misimamo yetu kama ina tija kwenye Maisha.
Hili ni tatizo kubwa sana aisee, hili nimeliona kwa watu wa sampuli mbili.

1. Watu wenye hela mara nyingi wana tabia hizi, yaani kwa ufupi wale ambao wanajihisi hawana shida wala kuhitajia jambo kwa mtu mwingine.

2. Watu wenye kudaiwa madeni, hawa huwa hawapokei kwa ajili ya usalama wao binafsi yaani kukimbia fedheha.

Hili nyongeza, nimeshwahi kuambiwa hivi "Ili kujiwekea heshima kwa watu, hakikisha usiwe unapatikana kila unapotafutwa kwa njia simu"

Kwangu mimi namba ngeni huwa nazifurahia sana, sababu huwa nahisi mchongo. Ila huwa nakereka sana napo pokea namba ngeni halafu mty ananiuliza "Wewe nani.....?? " huwa nakata simu au kumwambia "Waulize Tigo, au Airtel au Voda".
 
  • Thanks
Reactions: SMU
Hili ni tatizo kubwa sana aisee, hili nimeliona kwa watu wa sampuli mbili.

1. Watu wenye hela mara nyingi wana tabia hizi, yaani kwa ufupi wale ambao wanajihisi hawana shida wala kuhitajia jambo kwa mtu mwingine.

2. Watu wenye kudaiwa madeni, hawa huea hawapokei kwa ajili ya usalama wao binafsi yaani kukimbia fedheha.

Hili nyongeza, nimeshwahi kuambiwa hivi "Ili kujiwekea heshima kwa watu, hakikisha usiwe unapatikana kila unapotafutwa kwa njia simu"

Kwangu mimi namba ngeni huwa nazifurahia sana, sababu huwa nahisi mchongo. Ila huwa nakereka sana napo pokea namba ngeni halafu inaniuliza "Wewe nani.....?? " huwa nakata simu au kumwambia "Waulize Tigo, au Airtel au Voda".
Hiyo namba 1 ongeza na kukwepa mizinga! Inachosha hatari. Watu hawana aibu kabisa.

Wengine unakuta namba mpya halafu missed calls 10! Huwa natukana kimoyomoyo na hata sipigi. Ukishampigia mtu mara moja (au max mara 2) hajapokea, mtumie text tu ujitamhulishe au useme shida/taarifa yako.

Jamaa wa Dawasa kila mwezi wanakupigia na namba mpya kukumbushia bili ya maji!
 
Sahihi kabisa.
 
Nachukia sana nikimpigia simu mwanamke mzuri asipokee

Inaumiza kwaaakweri..!!!
 
Mimi niwaambie ukweli chanzo cha kuanza kutopokea simu mpaka leo
1.mizinga kwa ndugu
2.mke wa mtu
3.kumlinda boss wangu ambae mtu yeyote hawezi kumpata bila mimi..
Hivo mwenye shida na mimi lazma contact isome jina kinyume na hapo lawama au matusi huwa havinikasirishi ukiyaanzsha.
4.mimi bado nina umri mdogo hivo vishawishi lazma niviepuke kwa njia hizo
 
Simi nyingine ni za kikazi, interview na vitu kama hivyo kwanini usipokee?
Basi tuache iwe hasara ya mpokeaji ambaye hajataja kupokea..... Labda huyo Hajaomba kazi yoyote sasa kwa nn afikiri interview wkt kajiajiri😀😀
 
hizo ni prinsipo za kijinga kabisa unaweza poteza fursa bila kutarajia alafu badae unaanza kujuta
 
Basi tuache iwe hasara ya mpokeaji ambaye hajataja kupokea..... Labda huyo Hajaomba kazi yoyote sasa kwa nn afikiri interview wkt kajiajiri
Labda useme tayari ana kazi, ukiwa umejiajiri si ndio kabisa connection muhimu? Au hiyo ajira yako inakuwa haina wateja au clients
 
Back
Top Bottom