Kiparamoto
Senior Member
- Oct 1, 2015
- 100
- 100
Wakuu,
Kwa kuanza, mimi ni kijana wa makamu, umri 35+, mfupi, kibonge, mweusi tiiiiiiii!
Nimeajiriwa kwenye NGO moja ya wazungu, alhamdulilah familia inaenda chooni. Nimebahatika kuwa na watoto wa3 kila mmoja na mama yake na nashukuru wanangu wanaishi vizuri lakini sikubahatika kuoa wazazi wenza kwa sababu ya tabia zao za midomo midomo na uswahili mwingi.
Nilikuwa nikiishi single na muda mwingi niliutumia nikiwa na jamaa zangu Jeffu na Bakari ambao tulikuwa tukifanya kazi pamoja.
Basi siku moja rafiki zangu Jeffu na BeKa wakanishauri ninyoe upara kwa madai eti utanipendeza kutokana na kujaaliwa na udevu kama brush la kupakia chachandu kwenye mihogo.
Kweli bwana nikaamua kuwasikiliza swahiba zangu Beka na Jeffu nikafunga safari mpaka kwa kinyozi wangu kevii aliyezoea kuninyoa mnyoo wangu wa pank la kiaskari, siku hii alishangaa sana kusikia nataka kunyoa upara, hakuwa na budi kwakuwa mteja ni mfalme.
Nilipata tabu sana wakati wa mwanzo, sikuzoea kabisa kuwa na kipara. Basi ni kipindi hiki ndio nilikutana na wife wangu wa sasa, huyu alikuwa bestie yake na mke wa swahiba yangu bakari (beka) weekend moja nilimtembelea Beka kwake na nilimkuta peke yake huku akidai mkewe kaenda kicoba, basi baada ya muda shemeji alirudi akiwa na huyo rafiki yake (wife wangu wa sasa)
Baada ya siku kadhaa nilitafutwa na namba ngeni ambapo baada ya kujitambulisha niligundua ni yule rafiki wa shemeji basi tukaanza ukaribu na kuwa marafiki, huyu dada alipenda sana kunisifia upara wangu, na kunifanya nijute kwanini nilichelewa kunyoa dongo.
Muda ukapita, siku, wiki, miezi ukaribu ukazidi na akawa mtu wangu rasmi (beka na mkewe wote walijua) ukiacha upara wangu, huyu bibie alikuwa akiniheshimu na kunishukuru sana nilipokuwa namuokoa na pesa za marejesho na vicoba kwani alikuwa na michezo zaidi ya 15 sijui alikuwa anapeleka wapi hizi pesa.
Penzi likakolea na bibie wote tukakubaliana kufunga ndoa na tafrija fupi iliyokutanisha watu wachache tu, wazazi, marafiki zetu wakina beka na Jeffu pamoja na wana kikundi wenzake wa kikoba.
Hii siku ya ndoa hakika nilipendeza sanaa, nilimwambia kinyozi wangu kevii ahakikishe anakwangua haswaa upara wangu ili nimfurahishe mke wangu kwenye harusi yetu. Harusi ilifana sana, watu walikula na kunywa.
Maisha ya ndoa yakaanza...............:.!
Itaendelea.....