MamaSamia2025
JF-Expert Member
- Mar 29, 2012
- 10,090
- 22,368
Kwa siku kadhaa nimeshangazwa na wafuasi wa chama cha Mbowe kushambulia idara ya chipukizi iliyo chini ya UVCCM kana kwamba ni jambo la ajabu sana kuwahi kufanyika. Wanaoshangazwa na uwepo wa chipukizi wanatakiwa kujikumbusha kuwa chipukizi CCM haijaanza leo. Ni idara ambayo ipo kwa miaka mingi kwenye awamu zote. CCM imara inajengwa kwa mambo mengi sana kuliko wafuasi wa Mbowe wanavyodhani.
Taasisi zote za siasa, dini na zingine zote za kijamii zinazohusisha watoto huwa zinakuwa na programs maalum za kuwafundisha watoto itikadi zao na maono ya hizo taasisi. Kwa mfano kanisa la kisabato wana idara za PF na Adventures kwa ajili ya kuwanoa watoto. RC, KKKT, na madhehebu mengine nao wana programs zao kwa ajili ya watoto. Wenzetu waislamu wao wako makini kabisa kwa kuwa na madrasa. Watoto ndo Future ya taasisi hivyo ni muhimu kuwakuza wakielewa mwelekeo wa taasisi. Vyama vya siasa navyo pia hufanya hivyo.
Badala ya kuiongelea Chipukizi CCM ninawashauri CHADEMA wajitafakari na kuangalia namna gani wanaweza kuandaa viongozi wa baadae. Inachosha kila siku tunasikia Mbowe, Lema, Lissu, Sugu, Heche, Msigwa, Mnyika na John Mrema. Ni ngumu kusikia jina jipya limechomoza. Hao BAVICHA hawana makali mbele ya hao mafaza. Yaani hao mafaza ndo BAVICHA pia. Uimara wa chama ni wanachama wake na sio vinginevyo.
Mwisho ninawashauri CHADEMA impe kazi komredi Lucas mwashambwa kuwapa semina BAVICHA ili kuzidi kujiimarisha kisiasa. Mwashambwa ni kijana mzalendo mpenda nchi yake kwahiyo sidhani kama atakataa kuwanoa BAVICHA.