Kesi ya Chipukizi CCM kutajwa kwa mara ya kwanza Jumanne 13, 2024

Precious Diamond

JF-Expert Member
Jun 9, 2023
397
993
images (51).jpeg

Mwanaharakati na Mtetezi wa Haki za Watoto Kumbusho Dawson amewasilisha Ombi la Kikatiba katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar, kesi hiyo ya namba 2212 ya mwaka 2024 itatajwa kwa mara ya kwanza tarehe 13.02.2024 majira ya saa tatu asubuhi mbele ya Jaji Angelo Rumisha.

Mwanaharakati huyo na mtetezi wa haki za watoto anaitaka Mahakama ieleze usahihi wa CCM kutumia watoto chini ya miaka 18 wajulikanao kama Chipukizi katika shughuli zake za kisiasa za kila siku, ikiwa ni pamoja na kuwaalika kushiriki katika vyombo vya maamuzi, kwamba kuendelea kuwatumia watoto inakuika Katiba ya Tanzania; Sheria ya Mtoto na Mikataba mingine ya Kimataifa ya Haki za Mtoto ikiwa ni pamoja na Mkataba wa Afrika juu ya Haki za Watoto na Mkataba wa Haki za Mtoto.
 
Chama dola kongwe kina kiukwa katiba ktk kila nyanja na sekta, ni wakati wanasheria na wanaharakati kujitokeza kuifungulia kesi nyingi za kikatiba CCM
 
Wamevimbiwa

Uzalendo ni pamoja na kurudisha Shirika la Elimu Kibaha

TPRI Tropical Research Institute...domeni ya Ukweli Duniani ..hapo nyumba ya mwewe kiota cha Utafiti nini shida

Mbogamboga ilaaniwe...
 
Back
Top Bottom