Taarifa ya Zitto Kabwe kuhusu Gazeti la Taifa Imara

Taarifa ya Zitto Kabwe kuhusu Gazeti la Taifa Imara

Hivi katika mazingira ya kawaida unazani anaweza sema ni kweli?hata wale wezi wa tegeta escrow walijitetea kwa kukataa,,haijawahi na haitawahi tokea ktk historian hii mtuhumiwa kukunali
 
Mti wenye matunda ndo unaolengwa sana we endelea na mipango yako tu
 
Katika gazeti la Taifa Imara la tarehe 23 Machi 2015 kulikuwa na habari yenye kichwa cha maneno ' Zitto amchongea Mengi kwa JK?' Habari hiyo ilibeba maudhui ya 'post' iliyoandikwa katika mtandao wa ----------- online.
Habari hiyo inaonyesha kuwa Mimi nilikutana na Rais kwa msaada wa watu mbalimbali na katika kikao hicho inadaiwa nilisema kuwa Mengi ndiye aliyechochea wabunge kuishughikia Serikali ya Rais Kikwete ili ianguke.

Ni vema ifahamike kuwa gazeti la Taifa Imara linamilikiwa na Bwana James Rugemalira wa kashfa ya Escrow na kuendeshwa na Bwana Prince Bagenda aliye organise press conference ya mmoja wa mawaziri waliofukuzwa kazi kwa kashfa hiyo. Vile vile chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa ----------- online ambao unaendeshwa mmiliki wa Mawio gazeti ambalo kila wiki lina habari za kutunga dhidi yangu na chama cha ACT Wazalendo.

Habari hiyo ni ya kutunga yenye fitna zenye lengo la kuchonganisha watu. Naomba kufafanua ifuatavyo

1 Taarifa Maalumu ya Kamati ya PAC kuhusu ufisadi wa tshs 306 bilioni za Escrow hauhusiki na Bwana Reginald Mengi kwa namna yeyote ile. Mengi sio mbunge, sio mjumbe wa PAC na hakushawishi PAC kwa namna yeyote ile. Wezi wa Escrow wasitapetape kutafuta mchawi wakati mchawi ni wizi wao wenyewe. Porojo za kwamba Mengi alihonga wabunge ili kuishughulikia Serikali zinabaki porojo tu. Ila kama kuna mtu ana chembe ya ushahidi wa jambo hilo apeleke kwenye vyombo vya dola kwa hatua kuliko kurudia rudia porojo hizo kwenye vyombo vya habari.

2 Sihitaji kutumia watu ili kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwani ninaweza kukutana naye kwa taratibu za kawaida kabisa za kiserikali. Hadithi ya kwamba nimeomba watu wanikutanishe na Rais inaonyesha namna mwandishi alivyoshindwa kutunga uongo wake. Katika kukutana kwangu na Rais kikazi sijawahi hata mara moja kuzungumzia watu. Hivyo kusema nilikwenda Ikulu kumzungumzia Bwana Mengi ni kunidharau na kuidhalilisha Taasisi ya Urais.

3 Nimemwelekeza mwanasheria wangu achukue hatua za kisheria dhidi ya Gazeti la Taifa Imara na vilevile Gazeti la Mawio kwa mfululizo wa habari za kutunga uongo dhidi yangu kila kukicha. Nimeagiza tupeleke mashtaka kwenda Baraza la Habari Tanzania ili magazeti hayo yathibitishe habari zao.

Zitto Kabwe
Kiongozi wa ACT Wazalendo

Kwa nin serikali isilifungie hili gazeti mara moja
 
Kwa wepesi wa haya majibu ninaanza kuamini Taarifa ya gazeti la TAIFA IMARA

Yaaan hata ww leo kisa zitto tu mnaunga mkono gazeti la ruge fisadi wa escrow dah kweli zitto atawasumbua sana
 
Kubenea ameanza kuwa mwandishi wa hovyo katika siku za hivi karibuni kila mara na wakati ameendesha project chafu za kuwachafua watu hasa Zitto. Kumuandika Zitto kila wakati hakusaidii sana, ni vema CHADEMA waelekeze muda wao mwingi kuelezea itikadi na issues.
Ni kweli kuwa watanzania wanapenda siasa za matukio na fitna na sio issues lakini ni vema kukumbuka matukio ya kumchafua Zitto hayawasaidii wao sana bali yanawapotezea muda wa kujieleza kwa wananchi.
Na chama cha CDM kisipobadilika ni wazi kuna mgogoro mwingine utakuja ndani ya chama chao muda si mrefu.
 
Kunawatu niwachonganishi mpaka mnatia kinyaa, hiv mnafaidi nini kwa kutunga mambo ya uongo?? Zitto zitto zitto, kwani hakuna newz nyingine?? Kama siasa cdm zimewashinda rudini moshi mkalime...

Ki ukwel mnakera sana, njon basi walao na fact kidogo.. mnawasiwasi kama mna k..u.n .y..anje??

Hamchoki ooo msaliti, ooo kahongwa oooo kafanya hivi...
Asee mnalipwa sh ngapi bavicha??

Mm c mwanachama wa chama chochote ninakareka sana hao wanaosema usaliti, cjui hongo

Maccm huwa yanajificha kwa mgongo wa "sina chana". Wote Ni wake wale!!
 
ZZK populality went away with his expulsion from CDM, huyu ni bingwa wa kushitaki, kwa nini asiende mahakamani kushitaki waliotoa tuhuma?

Sisi tumemchoka, na inatuuma kuona kijana tuliyemwamini anatumiwa vibaya.

Zitto umetuangusha tuliokupugia debe hadi ukawa maarufu.
 
Kubenea ameanza kuwa mwandishi wa hovyo katika siku za hivi karibuni kila mara na wakati ameendesha project chafu za kuwachafua watu hasa Zitto. Kumuandika Zitto kila wakati hakusaidii sana, ni vema CHADEMA waelekeze muda wao mwingi kuelezea itikadi na issues.
Ni kweli kuwa watanzania wanapenda siasa za matukio na fitna na sio issues lakini ni vema kukumbuka matukio ya kumchafua Zitto hayawasaidii wao sana bali yanawapotezea muda wa kujieleza kwa wananchi.
Na chama cha CDM kisipobadilika ni wazi kuna mgogoro mwingine utakuja ndani ya chama chao muda si mrefu.

Kubenea ana mtimanyongo sana na ni limbukeni ndio maana mtandao wake umechuja shame on him
 
Hawezi kukubali kirahisi lazima akane si mjinga Wa kukubali kirahisi wengi wakana pesa za escrow si za umma hadi mkuu lakini mwisho wake aibu hata hii mwisho wake aibu
 
Zitto kishapoteza mwelekeo anajiingiza matatizoni always! Mara anagombana na CDM kufika tu ACT anaongea ovyo ovyo tu! Kajiingiza kwenye bifu na Dr. Mengi kajimaliza!!!
 
Siku zote hizo ulikuwa wapi kukanusha mpaka bwana Mengi alipojitokeza hadharani na kulia lia kama kawaida yake, ndio eti unakanusha?!
 
Kubenea ameanza kuwa mwandishi wa hovyo katika siku za hivi karibuni kila mara na wakati ameendesha project chafu za kuwachafua watu hasa Zitto. Kumuandika Zitto kila wakati hakusaidii sana, ni vema CHADEMA waelekeze muda wao mwingi kuelezea itikadi na issues.
Ni kweli kuwa watanzania wanapenda siasa za matukio na fitna na sio issues lakini ni vema kukumbuka matukio ya kumchafua Zitto hayawasaidii wao sana bali yanawapotezea muda wa kujieleza kwa wananchi.
Na chama cha CDM kisipobadilika ni wazi kuna mgogoro mwingine utakuja ndani ya chama chao muda si mrefu.

Kubenea sio chama. Inawezekana Ni mwanacdm lakini huwezi kumlink na Cdm moja kwa moja. Hana nafasi yoyote ya uongozi ndani ya chama.
 
peleka mahakani hawa akina kubenea na machizi wenzake
Yaani ungejua mi hii mijizi inavyoniboa nadhani ningekuwa Raisi ningebeba sheria mkononi kwani huwa kuna mijitu hata haifai ku ague nayo
 
Back
Top Bottom