Taarifa ya Zitto Kabwe kuhusu Gazeti la Taifa Imara

Taarifa ya Zitto Kabwe kuhusu Gazeti la Taifa Imara

Mwl. Kaijage

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
216
Reaction score
214
Kutokana na taarifa zilizoandikwa na gazeti la 'TAIFA IMARA' linalomilikiwa na James Rugemalira, tuhuma dhidi ya Dr. Reginald Mengi alizozielekeza kwa Zitto Kabwe.

Mwami ZITTO KABWE atajibu kupitia mkutano wa Shinyanga utakaofanyika leo.

========
Tamko lake:
Katika gazeti la Taifa Imara la tarehe 23 Machi 2015 kulikuwa na habari yenye kichwa cha maneno ' Zitto amchongea Mengi kwa JK?' Habari hiyo ilibeba maudhui ya 'post' iliyoandikwa katika mtandao wa Mwana Halisi online.

Habari hiyo inaonyesha kuwa Mimi nilikutana na Rais kwa msaada wa watu mbalimbali na katika kikao hicho inadaiwa nilisema kuwa Mengi ndiye aliyechochea wabunge kuishughikia Serikali ya Rais Kikwete ili ianguke.

Ni vema ifahamike kuwa gazeti la Taifa Imara linamilikiwa na Bwana James Rugemalira wa kashfa ya Escrow na kuendeshwa na Bwana Prince Bagenda aliye organise press conference ya mmoja wa mawaziri waliofukuzwa kazi kwa kashfa hiyo. Vile vile chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa Mwana Halisi online ambao unaendeshwa mmiliki wa Mawio gazeti ambalo kila wiki lina habari za kutunga dhidi yangu na chama cha ACT Wazalendo.

Habari hiyo ni ya kutunga yenye fitna zenye lengo la kuchonganisha watu. Naomba kufafanua ifuatavyo

1. Taarifa Maalumu ya Kamati ya PAC kuhusu ufisadi wa tshs 306 bilioni za Escrow hauhusiki na Bwana Reginald Mengi kwa namna yeyote ile. Mengi sio mbunge, sio mjumbe wa PAC na hakushawishi PAC kwa namna yeyote ile. Wezi wa Escrow wasitapetape kutafuta mchawi wakati mchawi ni wizi wao wenyewe. Porojo za kwamba Mengi alihonga wabunge ili kuishughulikia Serikali zinabaki porojo tu. Ila kama kuna mtu ana chembe ya ushahidi wa jambo hilo apeleke kwenye vyombo vya dola kwa hatua kuliko kurudia rudia porojo hizo kwenye vyombo vya habari.

2. Sihitaji kutumia watu ili kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwani ninaweza kukutana naye kwa taratibu za kawaida kabisa za kiserikali. Hadithi ya kwamba nimeomba watu wanikutanishe na Rais inaonyesha namna mwandishi alivyoshindwa kutunga uongo wake. Katika kukutana kwangu na Rais kikazi sijawahi hata mara moja kuzungumzia watu. Hivyo kusema nilikwenda Ikulu kumzungumzia Bwana Mengi ni kunidharau na kuidhalilisha Taasisi ya Urais.

3. Nimemwelekeza mwanasheria wangu achukue hatua za kisheria dhidi ya Gazeti la Taifa Imara na vilevile Gazeti la Mawio kwa mfululizo wa habari za kutunga uongo dhidi yangu kila kukicha. Nimeagiza tupeleke mashtaka kwenda Baraza la Habari Tanzania ili magazeti hayo yathibitishe habari zao.

Zitto Kabwe
Kiongozi wa ACT Wazalendo
 
Huu ushirikiano Mpya kati ya Rugemarila (Mtuhumiwa wa Escrow)na Mmiliki wa Mwana Halisi Forum na Mwandishi wa gazeti la Mawio si Salama kwa Rasilimali za nchi.

Katika kuhangaika Mzee Mengi,amemtuhumu Zitto Kabwe kuwa ndiye kampelekea Rais Kikwete taarifa juu ya Mengi Kumshighulikia pindi atakapo staafu.Lengo la habari hii ni mwendelezo wa visasi na vita ya kuhakikisha Zitto anapotea hatimae kufifiza harakati za ACT-wazalendo.

Kwamujibu wa Mengi, Chanzo cha habari hizo ni Gazeti Jipya la 'Taifa Imara' lililoanzishwa Kimkakati.

Gazeti la Taifa Imara lenyewe mnajua linamilikiwa na nani?

Gazeti la Taifa Imara ni Mali ya Rugemalila ambae ni Miongoni mwa watuhumiwa wa Ufisadi wa Escrow waliowaponza Tibaijuka na Werema .

Sasa mtu huyu huyu alianikwa tena hivi karibuni kwenye ziara ya ACT-Wazalendo kuwa kapewa tenda ya Tril 54 kujenga Bandari ya Mwambani corridor kinyemela bila Zabuni hiyo kufuata taratibu za manunuzi.

Rugemalila na genge lake la mafisadi wanaofukarisha taifa hili kila kukicha wanaendelea kutafuta target ya kumsambaratisha Zitto ili waendelee kuliibia taifa bila kukemewa.

Halafu habari yenyewe,Chanzo chake eti ni Mwana Halisi forums.

Yaani Mwana Halisi inayomilikiwa na viongozi wa Chadema (Kubenea) wanaweza kuwa chanzo cha habari ya kuaminika na ikawa njema kwa Zitto?

Hizi ni tuhuma za kutunga,na ndio maana mara kadhaa tumetahadharisha kuwa huu ushirikiano kati ya baadhi ya viongozi wa Chadema na watu wachafu kama Rugemalila unapaswa kutiliwa mashaka hasa na wazalendo wa mchi hii.

Haya si mahusiano yenye Afya na kamwe hatuwezi kuendelea kuwachekea na kuwaunga mkono.

Vita dhidi ya Ufisadi imemfanya Zitto kupata maadui wengi, Sasa Rugemarila na Kubenea wanashirikiana kupambana na Zitto.

Gazeti la Mawio kila wakiamka hawana habari yoyote zaidi ya Zitto na ACT-Wazalendo.

Kubenea na Anthon Komu wameona nguvu ya kumdhibiti Zitto haitoshi,wameamua kufanya Collaboration na Rugemarila kupambana na Zitto.

Wametunga habari ili kutaka msaada wa Reginald Mengi kwenye hii vita.

Na Mengi bila kufuatilia mmiliki wa Gazeti na Chanzo cha habari (Source) ameamini kichoandikwa.

Tunachoweza kufanya wanyonge wa nchi hii ni kugomea kununua Magazeti yanayoshirikiana na Mafisadi kudhoofisha vita dhidi ya Ufisadi.

Tusinunue gazeti la Mawio,na Taifa imara kutokana na kusaliti Vita dhidi ya Wizi.

Wanyonge bado tunasafari ndefu na tusipoungana aki na Rugemarila watatumaliza na wataendelea kutukejeli kuwa Mil 25 ni pesa za Chai.
 
Kutokana na taarifa zilizoandikwa na gazeti la TAIFA IMARA linalomilikiwa na James Rugemalira,tuhuma dhidi ya Dr.Reginald Mengi alizozielekeza kwa Zitto Kabwe. Mwami ZITTO KABWE atajibu kupitia mkutano wa Shinyanga utakaofanyika leo.

Mimi nafikiri lile gazeti linapaswa kupigwa ban na wala Mengi haja mtuhumu Zitto bali amelalamika taarifa kuto kanushwa..ila mtu yeyote akiisoma hiyo taarifa anajua ni ya kutunga..hata hivyo uzushi hule wa kumchafua Rais ulianzia kwenye mitandao humu

Mwisho Mengi anapenda kulialia kama Bavicha yani habari kama hile ya kidaku inampa shida..
 
Mkuu Mbona BAVICHA wameiamini ile taarifa?
 
Mimi nafikiri lile gazeti linapaswa kupigwa ban na wala Mengi haja mtuhumu Zitto bali amelalamika taarifa kuto kanushwa..ila mtu yeyote akiisoma hiyo taarifa anajua ni ya kutunga..hata hivyo uzushi hule wa kumchafua Rais ulianzia kwenye mitandao humu

Mwisho Mengi anapenda kulialia kama Bavicha yani habari kama hile ya kidaku inampa shida..
Utamaduni wa kutopenda kukanusha habari mpaka ubanwe mbavu hasa ndio umetuharibu ndio maana unaona kawaida, Mengi ame-play part yake amekanusha, kurugenzi ya habari nayo ikanushe na Zitto nae akanushe alafu na gazeti nalo lije na sehemu ya pili tena baada ya jamaa kukanusha na mwisho wa siku wananchi tunapata kitu kamili na gazeti kama limetunga liandike ukurusa wa mbele kwa maandishi makubwa yaliyo bolidiwa (bold) kuomba msamaha
 
watu mumekariri kukanusha eti kwanini msifikiri upande mwingine wa kukubali
 
Habari kama hile ni ya kijinga kiasi kwamba watu kupoteza muda kuikanusha ni upotevu wa rasilimali..habari imejaa uongo mtupu kinacho takiwa ni lile gazeti kupigwa ban tuu..
 
Habari kama hile ni ya kijinga kiasi kwamba watu kupoteza muda kuikanusha ni upotevu wa rasilimali..habari imejaa uongo mtupu kinacho takiwa ni lile gazeti kupigwa ban tuu..
Hapo umenena mkuu maana hii ndio inasababisha kutungwa sheria ya mitandao kali na kuwanyima wengine uhuru wa kuchangia hoja
 
Mengi amekurupuka.....
Mwisho Mengi anapenda kulialia kama Bavicha yani habari kama hile ya kidaku inampa shida..
Nyie ni vilaza kweli, yaani mlitaka Mengi akae kimya wakati habari inamuumiza katika mambo yake? Hebu angalieni hapa chini, Kitila na ZZK waliwahi kuitaka CHADEMA itoe tamko kuhusu waraka uliokuwepo mitandaoni hapo nyuma, kwani walijua impact ya uongozi kukaa kimya:
Mgogoro ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), umeingia katika sura mpya baada ya viongozi wake wawili waandamizi, Naibu Katibu Mkuu, Zitto Kabwe na Mjumbe wa Kamati Kuu, Dk Kitila Mkumbo kuuandikia uongozi wa chama hicho wakitaka uikane taarifa inayowachafua mitandaoni.

Katika taarifa yake kwa vyombo vya habari jana, Zitto alisema amemwandikia barua Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willbrod Slaa kumwomba athibitishe ‘Taarifa ya Siri ya Chadema' kama ni ya kweli au chama hicho kiikanushe ili aweze kuchukua hatua za kisheria dhidi ya waandishi wa kile alichokiita ‘hekaya.'
 
Mimi nafikiri lile gazeti linapaswa kupigwa ban na wala Mengi haja mtuhumu Zitto bali amelalamika taarifa kuto kanushwa..ila mtu yeyote akiisoma hiyo taarifa anajua ni ya kutunga..hata hivyo uzushi hule wa kumchafua Rais ulianzia kwenye mitandao humu

Mwisho Mengi anapenda kulialia kama Bavicha yani habari kama hile ya kidaku inampa shida..

Umeanza vizuri lkn umemaliza vibaya.Mengi kasema kwanini Ikulu hawakanushi? Hayo ya Bavicha yameharibu jibu lako.Usidharau taasisi ya Urais bwana.Hata kama ni gazeti la udaku sidhani kama linastahili kuandika udaku unaomhusu Rais na Ikulu wakakaa kimya.Huoni Rais anadharirishwa wewe?
 
RUGEMARILA wa Escrow na CHADEMA Wame-Team Up na CHADEMA Kumshambulia Zitto kupitia Gazeti la TAIFA KWANZA(La RUGEMARILA), Mwana Halisi Online, Mawio na Tanzania Daima.

Why? "They now SHARE the SAME Enemy" - Zitto.
Tatizo sio ZZK wala nani, Tatizo kwanini Ikulu imekaa kimya?
 
watu mumekariri kukanusha eti kwanini msifikiri upande mwingine wa kukubali
Sio kukariri bali kitu chochote ambacho si cha kawaida au kinyume na utaratibu kinapotolewa kwa kumhusisha mtu bila yeye kukiongelea huwa tunaita tuhuma na mara nyingi ushahidi huwa ni wa kumulika na tochi hivyo lugha sahihi ni kuja kukanusha kwa misingi kwamba kwa mwanadamu wa kawaida hatutarajii kukifanya. Na ndio maana mahakamani pamoja na kwamba mtu ameonekana ameua lakini ataitwa aende akajitetee na si kuitwa kwenda kukubali. Anpokuja yeye sasa ndio anakiri ni kweli tena wengine husema wazi hapa sina cha kukanusha hiyo issue ni kweli kabisa
 
Back
Top Bottom