Taarifa ya Zitto Kabwe kuhusu Gazeti la Taifa Imara

Taarifa ya Zitto Kabwe kuhusu Gazeti la Taifa Imara

Zitto upo tayari nilete ushahidi wa wewe kukutana na rais na kumwambia ya Mengi?
Unatambua kuwa kila anapokaa au kusimama rais pana Special surveillance camera?
 
Ndio umemaliza kupost au ...! This is one of mentally castrated posts! Jus think if it is worth being posted here
Mkuu mshana jr, hadhi yako sio hata ya kubishana na mjinga kama huyu, hata hiyo karma unayoizungumzia na ile post hajaisoma. Hajui kwanza ataipata kwenye jukwaa gani humu JF, maana lile jukwaa ni la watu advanced. Mpotezee huyo kapurwa
 
ulikua wapi kusema mwanzo mambo hayo?? mpaka leo mwenyewe mengi kasema wasisi wake eti na wewe ndo unajitetea...
 
Gazeti la Ruge limeandika hiyo kitu tar 23 Machi, Zitto amekaa kimya mpaka Mengi alivyolalamika jana tar 17 April ndio Zitto akaona eheeee ngoja a-react. Mhhh?
 
Zitto unajidharirisha mkuu maana umekuwa mtu wa kutumwatumwa na kutumiwa kama ile mipira ya kiume dah!hivi kwa nn usiijari shule yako mkuu?
 
Cdm inahusika vipi hapo!!? Tumia akili Mkuu. Cdm ndio tunajiandaa kwenda ikulu. Waliopo sasa ndio wanatakiwa kujibu!!

Kubenea ni mwanachama wenu mtiifu ana tumika kuchafua watu na chadema wana mkono kwenye hili.
 
Katika gazeti la Taifa Imara la tarehe 23 Machi 2015 kulikuwa na habari yenye kichwa cha maneno ' Zitto amchongea Mengi kwa JK?' Habari hiyo ilibeba maudhui ya 'post' iliyoandikwa katika mtandao wa ----------- online.

Habari hiyo inaonyesha kuwa Mimi nilikutana na Rais kwa msaada wa watu mbalimbali na katika kikao hicho inadaiwa nilisema kuwa Mengi ndiye aliyechochea wabunge kuishughikia Serikali ya Rais Kikwete ili ianguke.

Ni vema ifahamike kuwa gazeti la Taifa Imara linamilikiwa na Bwana James Rugemalira wa kashfa ya Escrow na kuendeshwa na Bwana Prince Bagenda aliye organise press conference ya mmoja wa mawaziri waliofukuzwa kazi kwa kashfa hiyo. Vile vile chanzo cha habari hiyo ni mtandao wa ----------- online ambao unaendeshwa mmiliki wa Mawio gazeti ambalo kila wiki lina habari za kutunga dhidi yangu na chama cha ACT Wazalendo.

Habari hiyo ni ya kutunga yenye fitna zenye lengo la kuchonganisha watu. Naomba kufafanua ifuatavyo
1 Taarifa Maalumu ya Kamati ya PAC kuhusu ufisadi wa tshs 306 bilioni za Escrow hauhusiki na Bwana Reginald Mengi kwa namna yeyote ile.

Mengi sio mbunge, sio mjumbe wa PAC na hakushawishi PAC kwa namna yeyote ile. Wezi wa Escrow wasitapetape kutafuta mchawi wakati mchawi ni wizi wao wenyewe.

Porojo za kwamba Mengi alihonga wabunge ili kuishughulikia Serikali zinabaki porojo tu. Ila kama kuna mtu ana chembe ya ushahidi wa jambo hilo apeleke kwenye vyombo vya dola kwa hatua kuliko kurudia rudia porojo hizo kwenye vyombo vya habari.

2 Sihitaji kutumia watu ili kukutana na Rais Jakaya Kikwete kwani ninaweza kukutana naye kwa taratibu za kawaida kabisa za kiserikali. Hadithi ya kwamba nimeomba watu wanikutanishe na Rais inaonyesha namna mwandishi alivyoshindwa kutunga uongo wake. Katika kukutana kwangu na Rais kikazi sijawahi hata mara moja kuzungumzia watu. Hivyo kusema nilikwenda Ikulu kumzungumzia Bwana Mengi ni kunidharau na kuidhalilisha Taasisi ya Urais.

3 Nimemwelekeza mwanasheria wangu achukue hatua za kisheria dhidi ya Gazeti la Taifa Imara na vilevile Gazeti la Mawio kwa mfululizo wa habari za kutunga uongo dhidi yangu kila kukicha. Nimeagiza tupeleke mashtaka kwenda Baraza la Habari Tanzania ili magazeti hayo yathibitishe habari zao.
Zitto Kabwe

Kiongozi wa ACT Wazalendo



Kwani wewe ndiye Zitto !!? Au Ni msemaji wake. Aje akanushe mwenyewe!!
 
Last edited by a moderator:
Mods kwanini mnamuacha huyu jamaa mmoja kuanzisha threads za kufanana zaidi ya mbili?,,
 
Hakika Chadema na mchekeshaji wao wanaendelea kupata aibu.
 
kikwete anaongoza wananchi wasio na uwelewa,ila laiti kama angalipewa kaunt ya mombasa pekee kuongoza basi angaliresign within aday
 
Hajakana kukutana na raisi kikwete kama ilivyoripotiwa, Zitto haaminiki hata kidogo
 
Kila mmoja yuko obsessed na mwenzake....ndiyo utamu wa siasa za kibongobongo
 
Back
Top Bottom