wakuu,
nimetaarifiwa sasa hivi kwamba mke wa member mwenzetu freetown ameaga dunia mchana huu saa7.30 kwenye hospitali ya kcmc-moshi.
freetown ni member 'legend' hapa majukwaani, na kwa wale waliofika arusha mwaka jana (27/12/2010) tulipoenda safari ya tarangire wanapata hisia zaidi juu ya kuondokewa na mkewe kwa huyu member mwenzetu, maana tulikuwa pamoja nae bega kwa bega, na alisafiri na wanae, mabinti wawili.
mipango ya mazishi bado haijawekwa wazi, na zaidi inasubiri kuwasili kwa freetown mwenyewe toka ughaibuni anakomtumikia mkoloni, na kwa taarifa nilizopewa ni kwamba anatarajiwa kuondoka huko leo usiku, na atawasili kesho alasiri, mungu akipenda.
tutajuzana zaidi kinachoendelea, kwa sasa tunachoweza kusema ni kwamba mungu ailaze pema roho ya marehemu mke wa freetown.
amen.
update 1:
freetown ameondoka usiku wa saa 7.30 mahala anapoishi kuelekea doha-qatar,ambako likuwa aondoke saa 10.00usiku waleo(11/2/2011), lakini bahati mbaya flight aliyoondoka nayo anakoishi imechelewa kwa masaa mawili, hivyo hakuweza kuunganisha connection ya qatar-airways usiku wa leo, na hivyo atalazimika kulala hapo qatar na leo usiku ndipo atasafiri kwa shirika hilohilo na atafika dar-jnia kesho(ijumaa) saa 7.mchana, na atakuwepo uwanjani hadi saa 12.00jioni, ambapo ndio atapanda precision air kuja kia.
update 2:
mulioko dar mna nafasi kubwa ya kuonana na ft hapo jnia kesho, maana atakuwepo hapo kwa more than 4 hrs kabla ya kuja arusha, hivyo kwa watakaopenda kumtafuta tutawapa contact yake mumpate kirahisi.
update 3:
marehemu mrs ft atasafirishwa siku kati ya jmosi au j'pili kutoka arusha kuelekea njombe iringa, ambako ndiko domicile place ya couple hii...