Taarifa ya Msiba...!

Taarifa ya Msiba...!

R.I.P, sisi wana JF hatuwezi kukupa faraja ya kuondokewa na mpenzi mkeo, ni maombi yangu Mungu mwenyewe aliyempenda zaidi akupe faraja yake, kwamaana Biblia inasema yy ni mfariji wa kweli.

Twakupenda sana!!
 
R.I.P, sisi wana JF hatuwezi kukupa faraja ya kuondokewa na mpenzi mkeo, ni maombi yangu Mungu mwenyewe aliyempenda zaidi akupe faraja yake, kwamaana Biblia inasema yy ni mfariji wa kweli.

Twakupenda sana!!
Suzy, maneno yako yanaweza kabisa kumtoa nyoka pangoni!
Lakini zaidi sana yanafariji na kutia moyo, kiasi mtu anaweza kusahau kwa muda matatzo yanayomkabili !
God bless you too!
 
May her R.I.P.Tunawaombea faraja Mume wa Marehemu na familia katika wakati huu mgumu
 
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi, amen. Pole sana FT Mungu akufariji. My condolense.
 
wakuu, ndo tumerudi maofcn sasa bada ya kuuaga rasmi mwili wa mrs FT huko eneo la UsaRiver,
Na msafara umeondoka saa 5.20 kuelekea Iringa, Njombe, maeneo ya Iguachanya, Ihanja.
 
ukiacha mfiwa, Jf ilikuwa imewakilishwa na memberz 8 ambao ni:
derimto,
lilyflower
crashwise
mzee wa rula
preta
pakajimmy
msindima na
saharavoice.
 
ukiacha mfiwa, Jf ilikuwa imewakilishwa na memeberz 8 ambao ni:
derimto,
lilyflower
crashwise
mzee wa rula
preta
pakajimmy
msindima na
saharavoice.

Poleni sana wanafamilia na marafiki wote walioguswa na msiba huu! Mungu awatie nguvu na kuwafariji katika kipindi hiki kigumu. Na Mungu awalinde katika safari na kufika salama huko Iringa ili muweze kuupumzisha mwili wa marehemu. Asante kwa wana-JF waliotuwakilisha. Bless you all.
 
12022011.jpg
 
aksante crashwise.
Ni bahati mbaya kwamba tuliowakilisha tulikosa kubeba camera, lakini tulitumia mchina zetu japo kupata image mbili tatu.
 
PJ tufikishie pole hizi kwa wafiwa na pia tunashukuru kupata taarifa za kuondokewa na ubavu wa mwanajamii mwenzetu, mungu amtie nguvu kwa wote twaelekea huko tofauti ni tarehe tu na ndilo fumbo la imani. Pole nyingi kwa wafiwa.
 
nataarifiwa NA saharavoice kuwa kwa muda huu msafara ndio unaingia MOMBO.
Msafara huu utapiga breki ya kwanza mkoani Morogoro, ambapo ndiyo watapumzika kwa dakika kadha na kupata dinner kabla ya kuendelea na safari ya usiku kuisaka Iringa iliko.
 
RIP and may God give the family comfort and peace, tuko pamoja wakati huu.Mungu azidi kuwaonekania
 
Nataarifiwa kwamba kuna kundi lingine la memberz linalotokea Dar, na lingine Morogoro, lakini wote wanaungana pamoja pale Morogoro kuungoja msafara wa kutokea Arusha, ili hatimaye waungane kuelekea eneo la tukio.
 
Mungu awatie nguvu wafiwa na awape faraja yake iliyo kuu. tuko pamoja kwenye kipindi hiki kigumu cha majonz. thanx PJ kwa taarifa mhimu pia
 
Ni vigumu sana kusema
Ndugu yangu FT Mungu akupe moyo wa kuvumilia hasa wakati huu mgumu.
Ni kwa mapenzi yake Rabana kukupa mke huyu naye ndiye ameamua kumchukua kwake.
Tulifundishwa kushukuru kwa kila jambo.
Jipe matumaini ili sasa ujipange upya na uweze kusonga mbele.
Daima tutakuwa nawe kukuombea wewe na familia iliyobaki na zaidi tumwombee kwa Mungu ili marehemu apate rehema za Mungu.
Bwana alitoa na bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe milele AMINA
 
.....pole sana FreeTown, Bwana ametoa na Bwana ametwaa,jina la Bwana lihimidiwe. R.I.P mrs FreeTown.
 
Wadau, ni kwamba katika muda huu(0840pm), msafara mzima ndo unaingia Mjini Morogoro...Watapata chakula hapo, na bahati nzuri wameshakutana na convoy iliyotoka Dar na ya hapohapo Morogoro(ambao pia wana usafiri wao binafsi), kwahiyo wataanza kuondoka baada ya muda mfupi, huenda saa 3kamili...
Mungu awatangulie wenzetu hawa.
 
Back
Top Bottom