Mkuu PJ kama tulivyoongea kwenye simu jana, tuliondoka eneo la makaburi kama saa nane kaso robo hivi mara tu baada ya mazishi, kwani hatukuweza kubaki zaidi kwa sababu ilikuwa turudi tuliko toka kwa ajili ya majukumu siku ya Jumatatu na kuzingatia tulikuwa na safari ndefu mbele yetu ya zaidi ya 500km!
Tunashukuru Mungu kwamba safari ya kurudi ilikuwa salama kabisa na wote tuliosafiri (wana JF wanne) kwa shughuli ile tulifika salama kabisa makwetu, ingawa wakati tunakwenda tulipata breakdown kidogo njiani (tairi la mbele kuburst) lakini tulikuwa safe hakukuwa na madhara yeyote kwenye miili yetu na tukafanikiwa kufika Njombe saa kumi na moja na nusu asubuhi!
Mungu ni waajabu sana, mimi binafsi baada ya kufika kijijini kule ambako pia mjomba aangu yupo hapo, nikajikuta ule msiba wa ndugu yetu FT unanihusu kama ndugu, kwani Uncle yangu kumbe ameoa kwao kina FT.....amazing sana! mimi niliamua kwenda kwa kuguswa kama mwana JF lakini kumbe ilikuwa ni zaidi ya JF......! Nawashukuru wanaJF wote tulioenda nao kwa moyo wenu wote wa support ya hali na mali katika kuhakikisha safari ile inafanikiwa!
Asante sana mzee PJ kwa mawasiliano mazuri uliyofanya kwenye tukio hili, ulitoa taarifa nzuri sana zilizotusaidia sana kufanya maamuzi mengi wakati wa maandalizi ya safari yetu, Mungu akubariki sana!
Kwako Freetown, kama tulivoongea juzi na jana Mungu aendelee kukutia nguvu sana katika kipindi hiki kigumu sana katika maisha yako na daima kumbuka maneno mazito na yenye hekima ya Mchungaji aliyoyatoa jana wakati wa ibada ya marehemu pale nyumbani kwako ''Msihuzunike sana, msisikitike sana na wala msilie sana kwani kufa ni wajibu,leo ameondoka huyu, kesho itakuwa kwangu, keshokutwa kwako'' maneno haya binafsi yalinigusa sana kwa kweli! Pia nikaguswa sana na jinsi binti yako mkubwa alivokuwa anamlilia mamaake wakati anamuaga kwa mara ya mwisho, it was too emotional, very touching event.......!
Mungu ailaze roho ya marehemu mama FT mahala pema peponi! Amen.