Wadau, ni kwamba katika muda huu(0840pm), msafara mzima ndo unaingia Mjini Morogoro...Watapata chakula hapo, na bahati nzuri wameshakutana na convoy iliyotoka Dar na ya hapohapo Morogoro(ambao pia wana usafiri wao binafsi), kwahiyo wataanza kuondoka baada ya muda mfupi, huenda saa 3kamili...
Mungu awatangulie wenzetu hawa.
MwanajamiiOne,PJ ninamlaani sana mkoloni wangu kwa kuninyonya muda wangu wa mwisho wa wiki.........sasa hivi ndio ninapata pumzi na kuingia JF na kukutana na habari hii.....nakosa hata cha kusema.
Freetown.......................nitasema yale ambayo hunifariji kila nisikiapo taarifa ya kuondokewa na mpendwa au ndugu yeyote wa mpendwa wangu.
Duniani sis si wapitaji.... sisi ni maua mazuri tulopandwa Bustanini kwa MUNGU. Tumepandwa tuipendezeshe dunia na wale wote walio karibu nasi. Sisi ni maua ambayo ni mali ya Mwenye Bustani (MUNGU). Pamoja na kuwa na harufu nzuri na rangi nzuri tuliyo nayo kwa wale wote watupendao, pamoja na kupendwa na wale watupendao. sisi ni mali ya Mwenye Bustani. Na siku yoyote akiamua kutuchuma na kwenda kutupamba popote apendapo basi wale watupendao hawana budi kukubaliana naye.
Na kila mara anapoamua kutuchuma huamua mwenyewe akatupambe wapi. Kama ilivyo jadi mwenye bustani achumapo maua huamua ayapambe wapi kutokana na mapenzi yake. Yapo yanayopambwa sebuleni, jikoni, bafuni na mengine chumbani. Ni imani yetu kuwa MUNGU amemchuma mama yetu, dada yetu, wifi yetu na kipenzi chetu kwa kuwa tu imempendeza akampambe chumbani kwake kule ambapo atakuwa wa kwanza kumwona kila aamkapo na wa mwisho kumwona kabla hajalala.
SISI TULIMPENDA LAKINI MUNGU AMEMPENDA ZAIDI. Tumshukuru MUNGU kwa kulichagua uwa hili kuwa pembeni mwa kitanda chake.
BWANA Ametoa na BWANA ametwaa, jina lake Libarikiwe.
At Arusha level, hilo jambo limeshafanyika leo tayari..PJ you are such a blessing.
Kuna namna yoyote mme-organize japo tutoe rambirambi zetu kwa FT??.
At Arusha level, hilo jambo limeshafanyika leo tayari..
Kwa level ya tofauti na hiyo, sidhani kama kuna namna ingine yoyote ya utaratibu...
kITU kama hiki unachosuggest kingekuwa success kama kingekuwa organized na Wakubwa/wAMILIKI wa JF...!
Baada tu ya mazishi baadhi ya marafiki na wanajf waliotoka dar na moro wameanza kurudi makwao, ambapo kati yao ni Kiongozi Teamo na Mkuu Next Level...wengineo wawili waliofika kijijini hapo tutawataja tu pale tutakapopata ruksa toka kwao.
Vinginevyo mbarikiwe sana kwa moyo wenu huo, na Mungu mwenyewe ndiye atakayewalipa
Amen.
Mkuu PJ kama tulivyoongea kwenye simu jana, tuliondoka eneo la makaburi kama saa nane kaso robo hivi mara tu baada ya mazishi, kwani hatukuweza kubaki zaidi kwa sababu ilikuwa turudi tuliko toka kwa ajili ya majukumu siku ya Jumatatu na kuzingatia tulikuwa na safari ndefu mbele yetu ya zaidi ya 500km!
Tunashukuru Mungu kwamba safari ya kurudi ilikuwa salama kabisa na wote tuliosafiri (wana JF wanne) kwa shughuli ile tulifika salama kabisa makwetu, ingawa wakati tunakwenda tulipata breakdown kidogo njiani (tairi la mbele kuburst) lakini tulikuwa safe hakukuwa na madhara yeyote kwenye miili yetu na tukafanikiwa kufika Njombe saa kumi na moja na nusu asubuhi!
Mungu ni waajabu sana, mimi binafsi baada ya kufika kijijini kule ambako pia mjomba aangu yupo hapo, nikajikuta ule msiba wa ndugu yetu FT unanihusu kama ndugu, kwani Uncle yangu kumbe ameoa kwao kina FT.....amazing sana! mimi niliamua kwenda kwa kuguswa kama mwana JF lakini kumbe ilikuwa ni zaidi ya JF......! Nawashukuru wanaJF wote tulioenda nao kwa moyo wenu wote wa support ya hali na mali katika kuhakikisha safari ile inafanikiwa!
Asante sana mzee PJ kwa mawasiliano mazuri uliyofanya kwenye tukio hili, ulitoa taarifa nzuri sana zilizotusaidia sana kufanya maamuzi mengi wakati wa maandalizi ya safari yetu, Mungu akubariki sana!
Kwako Freetown, kama tulivoongea juzi na jana Mungu aendelee kukutia nguvu sana katika kipindi hiki kigumu sana katika maisha yako na daima kumbuka maneno mazito na yenye hekima ya Mchungaji aliyoyatoa jana wakati wa ibada ya marehemu pale nyumbani kwako ''Msihuzunike sana, msisikitike sana na wala msilie sana kwani kufa ni wajibu,leo ameondoka huyu, kesho itakuwa kwangu, keshokutwa kwako'' maneno haya binafsi yalinigusa sana kwa kweli! Pia nikaguswa sana na jinsi binti yako mkubwa alivokuwa anamlilia mamaake wakati anamuaga kwa mara ya mwisho, it was too emotional, very touching event.......!
Mungu ailaze roho ya marehemu mama FT mahala pema peponi! Amen.