Taarifa ya Msiba...!

Japo kuwa wote tulimpenda lakini muumba alimpenda zaidi. Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi Amina.
 
Wakuu,

Nimetaarifiwa sasa hivi kwamba mke wa member mwenzetu Freetown ameaga dunia mchana huu saa7.30 kwenye hospitali ya KCMC-Moshi.

Freetown ni member 'legend' hapa majukwaani, na kwa wale waliofika Arusha mwaka jana (27/12/2010) tulipoenda safari ya Tarangire wanapata hisia zaidi juu ya kuondokewa na mkewe kwa huyu member mwenzetu, maana tulikuwa pamoja nae bega kwa bega, na alisafiri na wanae, mabinti wawili.

Mipango ya Mazishi bado haijawekwa wazi, na zaidi inasubiri kuwasili kwa Freetown mwenyewe toka Ughaibuni anakomtumikia mkoloni, na kwa taarifa nilizopewa ni kwamba anatarajiwa kuondoka huko leo usiku, na atawasili kesho alasiri, Mungu akipenda.

Tutajuzana zaidi kinachoendelea, kwa sasa tunachoweza kusema ni kwamba Mungu ailaze pema roho ya Marehemu mke wa Freetown.
Amen.
Heroes never die because their ideas will live for ever - R.I.P
 
pole sana bro
Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi
 
Pole sana Freetown kwa msiba mkubwa uliokufika. Mwenyezi Mungu awape nguvu na faraja katika kipindi hiki kigumu kwenu na ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi~AMEN
 
pole sana freetown na familia nzima,mungu awatie nguvu na kuwapa faraja.
 
RIP Marehemu

Pole Freetown, binti zako na familia nzima

Bwana alitoa na Bwana ametwaa, Jina lake lihimidiwe. Amen

PakaJjmmy tunaomba uwakilishi wako kwa niaba yetu tulio mbali na asante kwa taarifa
 
UPDATE 1:
Confirmed Freetown ataondoka leo huko ughaibuni mwendo wa saa 6 usiku ambapo itakuwa ni saa 10.za alfajiri kwa huko anakoishi, na anatarajiwa kuwasili JNIA mwendo wa saa 7.00mchana kwa ndege ya shirika la QATAR AIRWAYS.
 
Pole sana, Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi na amtie nguvu mwenzetu na familia yake. Amen
 
Innalillah.........rajiuun.
Kuna jamaa zangu kule A-town ntawashauri japo wahudhurie.
member wetu Mungu ampe subira zaidi.
Kila kitu kitaonja kifo.
 
Asee nimeshtuka kusikia habari hi ya kusikitisha! Nampa pole sana Mwenzetu Freetown, Familia yake ndugu na jamaa wote. PJ tupo pamoja na fikisha pole yangu!
Bwana ametoa na bwana ametwa jina la bwana libarikiwe!Amen
 
Pole sana mkuu Freetown na Mungu akupe nguvu wakati huu mgumu.


Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.
 
Back
Top Bottom