Jeneza lawekwa juu ya gari la DC Siha

Jeneza lawekwa juu ya gari la DC Siha

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,923
Reaction score
6,570
Kilichopaswa kuwa siku ya mwisho ya kumuaga dereva bodaboda Emmanuel Mwanry kiligeuka kuwa tukio la taharuki na sintofahamu katika Kijiji cha Ngirinyi, Kata ya Levishi, Wilaya ya Siha mkoani Kilimanjaro.

Mamia ya waombolezaji waliokuwa wamekusanyika tangu mchana kwa ajili ya mazishi ya marehemu walijikuta wakisubiri kwa saa nyingi huku shughuli nzima ikikwama kutokana na msimamo mkali wa kundi la vijana waliokuwa wakishinikiza kuachiwa kwa wenzao 10 wanaoshikiliwa na Jeshi la Polisi.

Kadiri muda ulivyokuwa ukisonga, hali ya huzuni ilianza kuchanganyika na hasira.

Vijana hao walichukua hatua isiyo ya kawaida kwa kulichukua jeneza lenye mwili wa marehemu na kuliweka juu ya gari la Mkuu wa Wilaya ya Siha, Dk. Christopher Timbuka, kama ishara ya kupinga kile walichodai ni kutotendewa haki.

Tukio hilo lilisababisha taharuki miongoni mwa waombolezaji na wananchi waliokuwa eneo la mazishi, huku shughuli zote za maziko zikisimama kusubiri suluhu ya mgogoro huo.

Baadhi ya waombolezaji, waliokuwa wamekaa eneo hilo kwa zaidi ya saa sita wakisubiri mazishi kuendelea, walianza kutawanyika baada ya kutokuwepo kwa mwafaka kuhusu hatima ya mazishi hayo.

Mmoja wa vijana hao, Nickson Nkya, alisema hawakuwa tayari kuruhusu maziko yaendelee hadi wenzao waliokamatwa waachiwe huru.

“Hatuwezi kumzika mwenzetu mpaka wenzetu waliokamatwa waachiwe.

Pia tunataka pikipiki ya marehemu irejeshwe, tunaamini haki bado haijatendeka na hatuwezi kukubali kuendelea kuonewa,” amesema Nkya.

Msimamo huo uliendelea kushikiliwa na vijana hao huku familia ya marehemu, viongozi wa eneo hilo na waombolezaji wakisubiri kuona kama kungepatikana suluhisho ambalo lingewezesha mazishi kuendelea.

Hadi wakati wa tukio hilo, mazingira yalibaki ya sintofahamu, huku mwili wa marehemu ukiwa bado haujazikwa na jamii ikisubiri hatua zitakazochukuliwa ili kumaliza mvutano huo na kumpumzisha marehemu katika safari yake ya mwisho
Screenshot_20260617_074815_Lite.jpg
 
Huyo DC matako kweli unakuaje na DC wa aina hio? Sasa huyo DC Timbuka alisemaje baada ya kuhojiwa ndugu mwandishi tuambie au wewe haukumuhoji huyo DC baada ya jeneza kuwekwa kwenye gari yake ishara ya uchuro alijibu nini?
 
Ni vile tu maisha .....

Boda boda sio kazi !!! Risk kubwa, kipato kidogo , bado wanadharaulika huko barabaradi na wanaodtumia vyombo vingine vya moto mfano gari nk ! Mtu ana gari yake anakuletea huko huko, pia madareva wenyewe wameifanya hii kazi idharaulike..... wachafu, walevi, wengine wezi n.k

Apumzike kwa amani kijana mpambanaji
 
Ni vile tu maisha .....

Boda boda sio kazi !!! Risk kubwa, kipato kidogo , bado wanadharaulika huko barabaradi na wanaodtumia vyombo vingine vya moto mfano gari nk ! Mtu ana gari yake anakuletea huko huko, pia madareva wenyewe wameifanya hii kazi idharaulike..... wachafu, walevi, wengine wezi n.k

Apumzike kwa amani kijana mpambanaji
Wanadhaurika sana! Kuna mmoja tulikuta lori limemtupa huko Halafu likapita hivi! Yani ikabidi tumsadie ana magunia ya hoho mawili juu yake anavuja damu tu! Duhh hakuna mtu anayependa hiyo kazi ni maisha tu, tupunguze kuwalaumu sana jamani!
 
Si dalili nzuri wananch wa sasa s wale wa kidumu chama kimoja

Waache wajisahaulishe hasa viongoz wa bara ambao wanadhan ZANZIBAR inacheka na kima wakishtuka Tanganyika litakuwa koloni la zanzibar
 
Back
Top Bottom