Taarifa: waandamana kupinga ujio waBUSH

Chuma

Bendera ni ishara ya taifa na tumeweka viwango ambavyo binadamu wanaweza kubishana bila kupigana. Unapofika kuweka dhihaka kwenye bendera, ngao na nyimbo za mataifa mbali mbali basi wewe unakuwa punguani. Kuna standards ambazo tumejiwekea ambazo kama huzifuati basi wewe unakuwa na kasoro.

Hili lipo hata kwenye elimu standards zinawekwa na baadaye zinafuatwa, kama huwezi kulielewa hili ni sawa na kurudi katika karne za nyuma na kuanza kuvaa nyasi au magamba ya miti.

USTAARABU NI KITU CHA BURE LAKINI GHARAMA YAKE NI KUBWA.
 
Msomi mzima huna upeo kiasi hiki? ni nini udini? basi na mafuta tusinunue toka Middle East. kina Mtikila walikuwa wanaandamana jee wametoka mashariki?

kiongozi wa TLP leo rwekamwa alikanganya bendera ya Taifa letu hadharani ametoka middle East?

kumbe ndio maana umekuwa ukimtuhumu Professor Kighoma Malima humu bila ushahidi. yaani ndugu yetu hata maiti unamchukia?

kama wewe mkweli juu ya Marehemu malima na uadilifu wake kwa nchi tupatie ripoti ya M.V BUKOBA?

mbona Mkapa aliitia kapuni? Malima kwa uadilifu wake alipinga ununuzi wa ile meli kuwa ni bomu aliyeleta tenda ile ni sir Kahama suala lile kwenda kwa Mwalimu Nyerere akamuunga Mkono Kahama halafu Malima akaamua kujiuzulu, na kwenda zake kufundisha Marekani.

Matokeo ya Malima tumeyaona wote kifupi ni majuto mjukuu.

mzee acha roho mbaya ya udini sote ni binadamu na nchi ya wote.ni bora mtuambie kuwa mko kwenye CRUSADE inawezekana ni wewe uliyepinga OIC bila kuzingatia maslahi makubwa kwa nchi mwenzetu museveni kawakubali OIC anakula kwa mrija sie tufe na udini wetu.

kama nchi za middle East hazifai vipi chuo kikuu cha Dodoma wanakifadhili? tukatae pesa zao.mpelekeni Bush atumalizie chuo kama ni mkweli.

Umekuwa sensitive na udini sana bila sababu yoyote ya msingi. Kupinga sera za Bush ni jambo la kawaida. Hupingwa karibu kila nchi anakokwenda. Mara ya mwisho alipokuwa marekani ya kusini huko alipingwa vikali sana. Alipokwenda Australia pia alipingwa sana. Alipokuwa Ujerumani na Uingereza kote huko amekuwa anapingwa na kuzomewa. Hilo ni jambo la kawaida.


Swala la kuchoma bendera ya Marekani na kusema Death to Amerika ni swala lilioanzia Mashariki ya Kati na limekuwa linafanywa na militants wenye ideology fulani dhidi ya siasa za Marekani. Unafanya kosa sana unapodhani kuwa ideology ya hao militants ndio uislamu wenyewe. Ingawa ni kweli kuwa wale militants ni waislamu, siyo kweli kuwa ideology yao ndiyo uislamu. Hata mimi ninatoka familia ya kiislamu na ninayajua vizuri sana mafundisho ya kiislamu; hayako hivyo.

Hayo mambo mengine kuhusu professor Malima na Mkapa nadhani unaongewa bila kujua uongealo mradi tu unawaangalia kwa dini zao.

  1. Kumbuka kuwa Professor Malima alifukuzwa uwaziri na Rais Mwinyi kutokana na ufisadi aliofanya akiwa Waziri wa Fedha. Sidhani kama Rais Mwinyi alimfukuza Professor Malima kwa msingi wa dini, na sidhani kuwa baada ya yeye kufariki hatuwezi tena kuongelea rekodi yake. Ikiwa ni hivyo, basi hatutakuwa na haja ya kujua historia. Sijawahi kumsema Malima kama mwislamu bali Malima kama Malima, na siku zote nimekuwa nasema kuwa alikuwa msomi aliyebobea lakini alipopewa madaraka akaangusha nchi badala ya kutukomboa kiuchumi.
  2. Mkapa aliiba/alitumia madaraka yake vibaya na ndiyo maana mpaka leo tunapiga kelele kuwa asimamishwe kizimbani. Sijawahi kumtetea Mkapa kwa sababu ya dini yake. Katika wote, mtu ambaye mpaka sasa nahitaji sana kichwa chake mbele ya kizimba ni Mkapa.
  3. Hayo mengine za Middle East na Dodoma University naona ni pumba zisizokuwa na maana yoyote. Tanzania tangu imepata Uhuru imekuwa inapokea misaada kutoka sehemu mbalimbali za dunia na kwa sasa hivi Marekani inatoa fedha nyingi sana. Bill gates wa Merkani naye alitoa fedha nyingi za kujenga Dodoma University. Majengo kadhaa ya University of Dar es Salaam na Kilimanjaro Hotel yalijengwa na waisrael. Kitivo cha Uhandisi UDSM kilijengwa na Wajerumani. Sijui misaada ya namna hiyo wewe unaiweka upande gani katika mtazamo wako wa kidini.

    Kudai ripoti ya MV Bukoba kama uthibitisho wa uadilifu wa Malima ni pumba nyingine hizo.
 
Mbona wao huchoma Kuran na kuingia misikitini wakiwa na viatu ama sheria hizi zipo ku protect Marekani na Wakristu tu?...
 
Chuma

Bendera ni ishara ya taifa na tumeweka viwango ambavyo binadamu wanaweza kubishana bila kupigana. Unapofika kuweka dhihaka kwenye bendera, ngao na nyimbo za mataifa mbali mbali basi wewe unakuwa punguani. Kuna standards ambazo tumejiwekea ambazo kama huzifuati basi wewe unakuwa na kasoro.

Hili lipo hata kwenye elimu standards zinawekwa na baadaye zinafuatwa, kama huwezi kulielewa hili ni sawa na kurudi katika karne za nyuma na kuanza kuvaa nyasi au magamba ya miti.

USTAARABU NI KITU CHA BURE LAKINI GHARAMA YAKE NI KUBWA.
Actually kuchoma bendera kwa nchi kama Marekani si kosa la jinai hata US Supreme Court iliruhusu uchomaji wa bendera kwa amani kama ishara ya political speech.
 
Kama kawaida ya Wadanganyika siku zote huongea hoja kwa rangi zao....na ajabu ni pale watu wengine wanajaribu kutunga sababu na uzito wa maandamano kutokana na imani zao..

Kwanza wananbodi wote inabidi tujirudi na kumkufuru shetani kwani Tanzania ni nchi yenye uhuru mkubwa wa dini.. na tofauti kati yetu kidini haina maana wale wengine hawana sheria kwa sababu tu haikuhusu wewe.

Navyofahamu mimi Waislaam siku zote wamekuwa wakidai kutokana na kauli yake mwenyewe Bush kuwa yupo ktk crusade kuuondoa Uislaam na imani zao za kishetani. Hii statement ni nzito sana kwa kiongozi kama yeye kuweza kuitoa mbele ya hadhara ktk mkutano.
Kama kiongozi na rais mwenye nguvu kubwa duniani alifikia hata kuwaita majina mazito yenye kuutukana Uislaam. Na kwa matusi yake (kama Kiongozi wa Taifa kubwa) aliwavuta baadhi ya wakristu na kibao wanaendeleza kutumia matusi kama yale wakidai ni uhuru wao wa kusema chochote wanachotaka hata kama wamedai kuuondoa Uislaam na sheria zake ambazo hazikubaliki ktk dunia ya Kikristu. Hapo hapo wanasema wanaamini haki ya mtu kuabudu kile anachokitaka....
Lakini ajabu ni kwamba kila mhusika toka upande wa pili ambao ni waislaam akitumia matusi hayo hayo na ahadi hizo hizo huonekana kuwa ni gaidi (Terrorist). Tena basi wapo radhi kusema kuwa ahadi za Bush na mauaji anayoyafanya huko Iraq yana tofauti kubwa na mauaji yanayofanywa na Waislaam hata kama majeshi ya Marekani yameua watu wengi zaidi ya hesabu ya Saadam Hussein.
Na kinachozidi kushangaza ni kwamba wapo watu pamoja na hao wanasiasa wa Marekani wanaopinga vita hii kwa sababu:- Marekani inapoteza baadhi ya vijana wake vitani lakini hawatazami hesabu ya Wa Iraq wanaokufa kuwa iwe sababu ya kusimamisha vita hivi.

Sasa mnapodai kuwa kwa nini waislaam wasiandamane kwa sababu ya MV Bukoba, BoT na sijui Richmond Je wewe umesha andamana?... Inakuwaje swala la kuandamana ambalo ni haki ya kila Mtazania pale anapoona hakuna haki iwe ni jukumu la Muislaam ati kwa sababu tu kaandamana kupinga ujio wa Bush ambaye dunia nzima watu huandamana kila anapokwenda bila kujali dini zao, iweje Tanzania iwe ni issue ya Waislaam na kuwaona wao wajinga.. Hivi kweli nyie wakristu wa Tanzania mna akili kuliko wakristu wengine wote waliowahi kuandamana nchi tofauti na sidhani kama kuna nchi hata moja ambayo Bush amewahi kuweka mguu na ikawa hakuna maandamano..

Duh, ama kweli Tanzania ni nchi ya AMANI na UTULIVU = UJINGA!
 
Wabongo wa ajabu kweli,jamaa wanahamasishana kuandamana eti kumwonyesha kichaka wanavyomchukia,lakini utashangaa asubuhi ya jumatatu wako ktk foleni pale ubalozi wa amerika kuomba vikaratasi ili waende nyumbani kwa kichaka. Waacheni waandamane kutii kiu yao hatuna ubavu wa kumzuia kuja kuangalia misheni zake huku bongo,siku nne kukaa bongo sio mchezo.Subirini Africom basi.
 
Invisible and the forces that be, nimetaka kuweka picha hapa. Siku hizi ni mpaka m-approve au?
 
Malila,
Sasa wewe nambie imekuwaje watu waliandamana kuhusu BoT lakini bado fedha ya Taifa iko huko?..Umelalamika kuhusu Richmond na usiku wawasha taa zako?... come on fikiria kwanza kabkla hujaandika kitu.
Kuandamana kumpinga JK haina maana kesho hutakwenda Ofisi yoyote ya serikali...
 
Invisible and the forces that be, nimetaka kuweka picha hapa. Siku hizi ni mpaka m-approve au?

aaaa12rj4.jpg


Wachomaji Bendera.

Hakuna anayezuia picha labda ni mashine yako tu.
 
hii thread nzima mie nitai-summarize ktk neno moja, nalo ni MADNESS!!!.

achaneni na mambo ya udini, mnajitia aibu za bure, mnaji-expose kwa undani zaidi na mwisho wa siku hakuna cha maana mtakachopata zaidi ya kuchora mistari ya utengano!!

nakumbuka kabla ya 9/11 hata hapa USA kuchoma bendera ya marekani haikuwa kinyume cha sheria!! watu kuandamana hapa hapa USA juu ya ujio wa bush kwenye mji wao ni kitu cha kawaida......mfano mji ninaoishi bush ni "sumu" na yeye analijua hilo kiasi haji!!!

sasa hili yengele hapa litawapeleka wapi nyinyi ma-extremist(wote waslam na kristo). tena bush mwenyewe atasema kwamba "nimeenda tanzania, nimekuta democrasia ya hali ya juu!! kwani watu wanahaki ya kuandamana juu ya lolote provided hawavunji sheria."

kuna watu both sides, wana/mna tamani sana kutokee mfarakano wa kidini nchini TZ. mie hata siwaelewi ni chepi mtakachofaidika nacho........inshallah, naomba mungu nia zenu mbaya zishindwe na mlegee!!!
 
hii thread nzima mie nitai-summarize ktk neno moja, nalo ni MADNESS!!!.

achaneni na mambo ya udini, mnajitia aibu za bure, mnaji-expose kwa undani zaidi na mwisho wa siku hakuna cha maana mtakachopata zaidi ya kuchora mistari ya utengano!!

nakumbuka kabla ya 9/11 hata hapa USA kuchoma bendera ya marekani haikuwa kinyume cha sheria!! watu kuandamana hapa hapa USA juu ya ujio wa bush kwenye mji wao ni kitu cha kawaida......mfano mji ninaoishi bush ni "sumu" na yeye analijua hilo kiasi haji!!!

sasa hili yengele hapa litawapeleka wapi nyinyi ma-extremist(wote waslam na kristo). tena bush mwenyewe atasema kwamba "nimeenda tanzania, nimekuta democrasia ya hali ya juu!! kwani watu wanahaki ya kuandamana juu ya lolote provided hawavunji sheria."

kuna watu both sides, wana/mna tamani sana kutokee mfarakano wa kidini nchini TZ. mie hata siwaelewi ni chepi mtakachofaidika nacho........inshallah, naomba mungu nia zenu mbaya zishindwe na mlegee!!!

watu waandamane kumpinga BUSHI sera zake na sio kukimbilia eti ana isakama dini fulani.
Bushi ni mafia hana cha uislamu ama mkristo wote wakikaa mbele yake anawamafia vilevile
Haya mambo ya vita yameanza siku nyingi wanapigania maslahi Bushi ni mwendelezo tu wa hayo maslahi ,ni kitu cha ajabu sana kusema anapigana na uislamu jamani Bush IRAQ na ILAN anatafuta MAFUTA.Bongo anakuja kutafuta mahala pakuweka base yake ili akombe hayo mafuta ya Angola vijidhahabu vyetu,vya kongo na huko ghana,
 
Mushi Jambo gani la kitaifa linalomfanya Bush atembelee TZ?...
KWANZA NI KUMWAMBIA KUWA WAO WANA VITA VYAO VYA UGAIDI NA SISI TUNA VYETU VYA UFISADI!NDIVYO TUNAVYOTAKA VIPEWE KIPAUMBELE..KWANI HUJUI WATU WANAOKUFA KWA MAGONJWA NA NJAA NI WENGI KULIKO WALE WALIOKUFA KWENYE MABOMU YA UBALOZI 98?UPO?
Hiyo moja..japokuwa sikumaanisha kuwa kuja kwa Bush ndio suala la kitaifa bado nandhani nimekujibu ipasavyo hapo juu.
Lingine ni kuwa TULITAKIWA TUYAPE KIPAUMBELE YALE YANAYOTUATHIRI MOJA KWA MOJA KAMA VILE UFISADI AMBAO UNACHANGIA VIFO VYA WAZALENDO..HUO NDIO UTAIFA NILIOKUWA NIKIUNZUNGUMZIA..KWAMBA TUANDAMANE SIO TU KWA AJILI YA ISSUE ZA WATU WENGINE BALI ISSUE ZETU SISI WENYEWE AMBAZO HAZIUSISHI TOFAUTI ZA KIDINI AMA KIKABILA!LABDA KAMA HAO MASHEICK WANGEWAOMBA VIONGOZI WA DINI ZOTE WAUNGANE NAO KWENYE HAYO MAANDAMANO..THEN HILO TUNGELIANGALIA KWA NAMNA YA TOFAUTI!ILA TUSISAHAHU KWAMBA HATA SISI TUNA VITA VYETU DHIDI YA UFISADI..KAMA VILE BUSH NA MAREKANI KWENYE VYAO WANAVYOSEMA NI DHIDI YA UGAIDI!
 
PhD ya Physics au Maths haimzuii mtu kuishi kwa chuki.

Hii tabia ya kuchoma bendera ya marekani (na kudai kuwa Death to America) ni tabia ya militants iliyoaniza mashariki ya kati na kusambaa. Inaelekea kuwa sasa hivi imeanza kuingia Tanzania; kwa hiyo Tanzania tujihadghali kwa vile hii ni dalili kuonyesha kuwa na sisi tumeanza kuwa na hao militants.


Eti na huyu naye anataka atambulike kama mwanahabari huru na anaita watu kuwahoji na wengine kusikiliza kiredio chake cha uvunguni!

Mtalii kwanini usiwashauri kina njozi wapigie kelele ripoti ya MV Bukoba?

Sasa unakwenda kuhojiana naye nini?

Utamwita mtu, uhemkwe mawazo yako, kisha uje kutuambia ulichohojiana nae ambacho kinakidhi matashi yako!
 
watu waandamane kumpinga BUSHI sera zake na sio kukimbilia eti ana isakama dini fulani.
Bushi ni mafia hana cha uislamu ama mkristo wote wakikaa mbele yake anawamafia vilevile
Haya mambo ya vita yameanza siku nyingi wanapigania maslahi Bushi ni mwendelezo tu wa hayo maslahi ,ni kitu cha ajabu sana kusema anapigana na uislamu jamani Bush IRAQ na ILAN anatafuta MAFUTA.Bongo anakuja kutafuta mahala pakuweka base yake ili akombe hayo mafuta ya Angola vijidhahabu vyetu,vya kongo na huko ghana,

Ulichoongea ni sawa.Bush hana shida na dini ya kiislam.Yeye shida yake ni raslimali,ambao kwa wenzetu Waarabu ni Mafuta. Kwa kuwa ili aendelee kuwa super power mwenye uchumi imara lazima ajihakikishie mafuta yanapatikana bila matatizo, na hii ilitokana na lesson aliyojifunza miaka 1970s baada ya bei ya mafuta kupanda na kusababisha uchumi wa Marekani uliyumba sana. Sasa kutokana na Mgogoro wa Israel na Palestina, USA imeoneonekana inaisapoti Israel Waarabu waliamua kutumia Mafuta yao kama fimbo ili kumwadhibu Mmarekani. Baada ya hapo aliamua kuhakikisha anatumia uwezo wake kuhakiikisha anakuwa na mafuta muda wote.Katika kutumia uwezo wake akajikuta anavaana uso kwa uso na Waarabu ambao pia ni Waislamu. Na wao kwa kutotumia akili wakaona njia pekee ya kuwaunganisha na kupata support ni kutumia propaganda ya dini. Sasa unapotumia dini kama silaha yako yeye, hata bagua ila ni jukumu lako wewe ambaye uliamua kuiunganisha dini na vita hiyo kuamua.

Wengi humu tunaochangia naamini hatuma ubaguzi wa kidini,mimi binafsi 80% ya rafiki zangu ni waislamu.Lakini % hiyo hainifanyi nisiwaambie ukweli.Wenzetu hawa waislamu wanaubinafsi sana wa udini kuliko Utaifa wao. Wako tayari kushupalia issue inayogusa waislamu 10 kuliko issue inayogusa maisha ya Watanzania 30milioni na wao wakiwemo.Wako tayari kukashupalia kaishu kalikoanzishwa huko Uarabuni kuliko issue hot hapa nyumbani.
Sitaki kuwapangia issue ipi muishupalie au hapana ila busara na uzalendo ni kitu kizuri sana.
Nchi zenye waarabu wajanja (Dubai,Qatar,Kuwait,UAE,nk)wako kimya na ziko mbali kimaendeleo kuliko hao wanaojiita wao ni siasa kali.
 
Mkamap,

Mkuu wangu nadhani hutazami mapana ya issue nzima na nani muathirika.. Ni sawa na kusema Hata South Africa Kaburu alikuwa akitafuta Almasi , dhahabu na utajiri mwingine sio mtu mweusi kama kuuana basi waliuana toka enzi za Shaka Zulu...
Ebu niwe mzungu kidogo hapa..
Kwa nini Tanzania na nchi za kiafrika tuliandamana na pengine kwenda pigana vita huko South hali Ubaguzi upo kila kona duniani... kwa nini tusiende kila nchi yenye Ubaguzi na hasa Israel kama sisi tulikuwa tunatafuta haki?..

Ndugu zangu nitakuacheni na Hekima za Mzee Jumbe...by Mkandara.

Mzee Jumbe aliibiwa Generator ya Umeme akaamua kwenda Polisi toa taarifa. Alipofika pale alikutana na mkuu wa Kituo na kuomba afungue file kama taarifa ya kuibiwa..
Baada ya kusikiliza mashtaka hayo huyo mkuu wa kituo alisema - Mzee Jumbe umekuja hapa shtaki kuibiwa generator kwa nini usitumie nafasi na muda huu kumshtaki Lowassa ambaye alitunyima nchi nzima Umeme? (Richmond) nadhani utakuwa umefanya la maana sana kwani hiyo generator yako sidhani kama itapatikana wala haitakusaidia kitu kufungua mashtaka...

Kwa hekima na Busara mzee Jumbe alisema:- 'Afande, maneno yako kweli tupu na hakika swala la Lowassa ni zito zaidi. Sasa unaonaje maadam nipo hapa wewe kama afande nakuomba fungua mashtaka na mimi hapa nipo kama shahidi wako!'
 
TWO QSNS:

Can some body give me plausible reasons kwa nini Tanzania hatutaki kuruhusu majeshi ya USA (AFRICOM) kuweka base Tanzania? Apart from these normal songs of militarization of Africa continent ambazo tunazisikia kila siku. Mfano tukiyaruhusu, tutaathirika kivipi? na vice versa....

Swali lingine, hivi ugaidi tunaoushuhudia leo sehemu mbali mbali duniani eg Pakistan, Afghanistan, Iran etc, kama usingekuwa unatumia mwavuli wa dini ya kiislamu, ungefanikiwa?, I mean could they convince people like militants and fanatics to do what they do like blowing up buildings, themselves? Could they? WITHOUT USING THE NAME OF ISLAM? In otherwords kwa nini in most Islamic countries when people want to achieve their agendas, they tend to use the religion mask? Like when you kill infidels..you will be rewarded in heaven..? Kifupi hawa the so called maghaidi wanaweza kufanikisha agenda zao bila kutumia platform ya UISLAM?

Waungwana mi napenda kuuliza hivi na naomba Muislamu/Mkristu/Mpagani yeyote aliyemo humu jamvini anieleweshe. Kwa sababu nashindwa kuelewa kwa nini dini ya waumini millions and millions iwe LINKED na mambo mabaya? AS WE SEE EVERYDAY... na bado tunaambiwa ISLAM is the religion of Peace. I honestly find it puzzling for someone to kill another and justify his/her actions through the holy books. Perhaps we could get the answer kwa nini watu wanaandamana dhidi ya Bush kama adui wa Uislamu na Bush anatembeza bakora dhidi ya maghaidi... (ambao most of them they happen to be Islamist...)

What am I missing in this whole issue?

I will appreciate anybody`s response!
 
Mkamap,

Mkuu wangu nadhani hutazami mapana ya issue nzima na nani muathirika.. Ni sawa na kusema Hata South Africa Kaburu alikuwa akitafuta Almasi , dhahabu na utajiri mwingine sio mtu mweusi kama kuuana waliuana toka enzi za Shaka Zulu...
Na kwa nini tuliandamana na pengine kwenda pigana cita huko South hali Ubaguzi upo kila kona duniani... kwa nini tusiende kila nchi yenye Ubaguzi na hasa Israel kama sisi tulikuwa tunatafuta haki?..

Ndugu zangu nitakuacheni na Hekima za Mzee Jumbe...by Mkandara.

Mzee Jumbe aliibiwa Genetrator ya Umeme akaamua kwenda Polisi yoa habari. Alipofika pale alikutana na mkuu wa Kituo na kuomba afungue mashtaka..
Baada ya kusikiliza mashtaka hayo huyo mkuu wa kituo alisema - Mzee Jumbe umekuja hapa shtaki kuibiwa generator kwa nini usutumie nafasi na muda huu kumshtaki Lowassa ambaye alitunyima nchi nzima Umeme? nadhani utakuwa umefanya la maana sana kwani hiyo generator yako sidhani kama itapatikana wala haitakusaidia kitu kufungua mashtaka...

Kwa hekima na Busara mzee Jumbe alisema:- 'Afande, maneno yako kweli tupu na hakika swala la Lowassa ni zito zaidi. Sasa unaonaje maadam nipo hapa wewe kama afande nakuomba fungua mashtaka na mimi hapa nipo kama shahidi wako!'

Tungo tata Mkandara sijaokota kitu rudi mkuu unisaidie kuelewa .
 
Masanja,
Swali lingine, hivi ugaidi tunaoushuhudia leo sehemu mbali mbali duniani eg Pakistan, Afghanistan, Iran etc, kama usingekuwa unatumia mwavuli wa dini ya kiislamu, ungefanikiwa?, I mean could they convince people like militants and fanatics to do what they do like blowing up buildings, themselves? Could they? WITHOUT USING THE NAME OF ISLAM?
Nitakujibu swali la Pili...
Kwanza unalitazama swala hili kwa zangi na huyaoni mengi kwa sababu hayakuhusu... So let me touch you pale panapo kuhusu.
Umeuliza matumizi ya dini ktk nchi hizo kufanya Ugaidi, sasa nakuuliza wewe ilikuwaje sisi waafrika tulitumia weusi wetu (rangi) ktk ukombozi wa Afrika?...na tuliunda magaidi kutokana na rangi zetu, whites walikuwa na fikra kama zako na walishindwa kabisa kuelewa.
Pili, Umezitaja nchi ka ma Pakistan, Afghanstan... Je, sisi Afrika tungekuwa na machungu na Mzungu kama sii yeye kuwa kwetu Africa kututawala na badala ya kututendea haki wakatuburuza!.. Same with hao waislaam mkuu ni sisi tuliokwenda kwao na sasa hawataki kuburuzwa...
 
Masanja,

Nitakujibu swali la Pili...
Kwanza unalitazama swala hili kwa zangi na huyaoni mengi kwa sababu hayakuhusu... So let me touch you pale panapo kuhusu.
Umeuliza matumizi ya dini ktk nchi hizo kufanya Ugaidi, sasa nakuuliza wewe ilikuwaje sisi waafrika tulitumia weusi wetu (rangi) ktk ukombozi wa Afrika?...na tuliunda magaidi kutokana na rangi zetu, whites walikuwa na fikra kama zako na walishindwa kabisa kuelewa.
.

Hapa hata mie sijakuelewa.Kwa nini basi na wao wasipigane kwa kutumia Uarabu wao tu. au Uhindi or whatever na sio kutumia DINI?
 
Back
Top Bottom