Taarifa: waandamana kupinga ujio waBUSH

mtalii

JF-Expert Member
Dec 14, 2006
286
0
iri ri shehe zomba naro rinatowagaga mapointi. watakuchiaga,
Mwanakjj.

Dalili za kushindwa hoja. Mkandara,Zomba,Chuma na wote muacheni huyu bwana ana frastuesheni. hana makaratasi ndio maana ana muabudu Bush.mtu ambaye hawezi kutoka marekani ameshindwa hata kuoa ndoa za magirini.

sehemu yake ya kujiliwaza ni JF, bongoradio.na Tanzania Daima.
rudi nyumbani ukafanye kampeni kama kweli wewe Mwanaume.
mwenzenu hapa ni nyumba kwake kila dakika yuko JF hata bila hoja. akitoka marekani hawezi kurudi. kifupi tunasema hana miguu(green card).
 
Chuma

JF-Expert Member
Dec 25, 2006
1,329
0
Ndugu zangu nadhani hii imetosha turudi kwenye Mafisadi maanake tukisahau hilo tumekwisha hakuna cha muislaam wala mkristu hapa.. Maslahi ya Umma mbele..

Mafisadi jamani mafisadi!....wakiwemo waislaam na wakristu kibao sijui tutaitwa kina nani baada ya Wapinzani!

Mkandara sawa sawa...tupambane na Mafisadi nyumbani kwetu...Hili umelijadili vya kutosha...wale wasioelewa basi...
 
Lizy

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
412
500
uswahili mwingine mbaya, sasa kama wao hawataki Bush aje kwanini wanachoma bendera ya Marekani? Kama wanaamini katika huo uhuru wa kuandamana na maoni si wachome bendera ya Tanzania maana ni Tanzania ndiyo iliyomwalika Bush. Kama wanataka asije waandamane kumpinga Rais Kikwete na kuchoma bendera ya Tanzania!!

Hapana Mkuu, sikubaliani na wewe kwamba wangechoma Bendera ya Tanzania, labda kama ungesema wangechoma Bendera ya Kikwete kama walikuwa wanampinga Kikwete. Lakini vile walikuwa wanampinga Bush kwa sababu wanazojua wao nafikiri wana haki ya kuchoma Bendera ya Marekani vile Bush anakuja kama Rais wa marekani na sio kama yeye Bush kama Bush Na kitendo cha kuchoma Bendera, ni hali ya kawaida kwa binadamu (wengi wetu) ukiwa na hasira basi waweza fanya kitu chochote kilicho ndani ya uwezo wako kufikisha ujumbe sehemu husika. Isitosha, Tanzania sio nchi ya kwanza, utakubaliana na mimi kwamba hata nchi zingine kupinga jambo linalofanywa/linalotegemewa kufanywa na nchi flani (hasa katika maandamano), hupelekea kuchoma Bendera, Kuchora katuni na kuandika mabango yenye jumbe tofauti kupingana na kitu husika kilichopelekea maandamano.

Siungani na wala sipingani na waliondnamana kwani sina sababu za kupinga wala kukubali Ujio wa Bush.
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
Mwafrika wa Kike,

Only if,... kama dunia inge wa indentify kama Wakristu..lakini yalichukuliwa majina mengine kama vile Sandinist ambayo sielewi maana yake..Hivyo basi tunaweza jiuliza why Sandinista.. ama hata hao wa Iraq kuitwa Insurgents kwa nini wasiitwe waarabu?.. kesho wakija kubali kuwa wao ni Insurgents mtaanza kusema wanajibagua.
Kumbuka mkuu wangu tuliitwa Mandingo, Nigger, Negro na kila mara tulipojaribu kuyakubali maneno hayo kwa kuyatapa sifa na ushujaa walikuja na jingine hadi majuzi tu, watu weusi wenyewe walipochagua kwa kauli moja kuitwa African -American. It's the first time mtu mweusi kapata pumzi ya kuchagua jina analotaka awe identified..otherwise ni mwenye nguvu tu mwenye haki ya kupachika watu majina.

Exactly,

Hapa sasa ndipo unakuja zaidi kwenye point yangu kuwa sio suala la udini pekee linaloweza kuangaliwa katika issue ya vita vya marekani.

Kama suala la vita ya centra na south amerika ambako wengi ni wakristo haikusemwa kuwa marekani inapiga wakristo, kwa nini hii ya iraq isemwe kuwa marekani inapiga waislam?

Wewe mwenyewe mkuu ume-advocate hapa msimamo wa kutogeneralize wote kwa sababu ya vitendo vya wachache kwa hiyo nadhani hii issue lazima iwe kubwa zaidi kuliko misimamo ya kidini!
 
Lunyungu

JF-Expert Member
Aug 7, 2006
8,875
2,000
Hapana Mkuu, sikubaliani na wewe kwamba wangechoma Bendera ya Tanzania, labda kama ungesema wangechoma Bendera ya Kikwete kama walikuwa wanampinga Kikwete. Lakini vile walikuwa wanampinga Bush kwa sababu wanazojua wao nafikiri wana haki ya kuchoma Bendera ya Marekani vile Bush anakuja kama Rais wa marekani na sio kama yeye Bush kama Bush Na kitendo cha kuchoma Bendera, ni hali ya kawaida kwa binadamu (wengi wetu) ukiwa na hasira basi waweza fanya kitu chochote kilicho ndani ya uwezo wako kufikisha ujumbe sehemu husika. Isitosha, Tanzania sio nchi ya kwanza, utakubaliana na mimi kwamba hata nchi zingine kupinga jambo linalofanywa/linalotegemewa kufanywa na nchi flani (hasa katika maandamano), hupelekea kuchoma Bendera, Kuchora katuni na kuandika mabango yenye jumbe tofauti kupingana na kitu husika kilichopelekea maandamano.

Siungani na wala sipingani na waliondnamana kwani sina sababu za kupinga wala kukubali Ujio wa Bush.

Umejikaanga .Lizy baada ya kuchoma wamepata nini? Madai yao yamefika wapi ? yamesikilizwa ?
 
Lizy

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
412
500
Umejikaanga .Lizy baada ya kuchoma wamepata nini? Madai yao yamefika wapi ? yamesikilizwa ?

Walifikisha ujumbe wao kwamba hawakupenda Ujio wa Bush, na kwamba walitumia uhuru wao kuandamana period!

Unajua fika wasingeweza kuzuia kuja kwake, na hata wao walilijua hilo kwamba wasingeweza kumzuia kuja. Ila ujumbe wao ulifika kama walivyoukusuadia.

Sijui kama nimekujibu swali lako ama this time nimejipika mwenyewe?
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Mwafrika wa Kike,
Mamaa vipi tena bado tu hujanielewa?.

Ukitangaza leo kuwa aliyekushambulia ni Musilaam ama niseme Black yule mhusika atajitambulisha vipi?... wewe hapa unajiita Mwafrika wa kike hivi unataka mimi nitumie jina gani?.. Uke wako ama kile unachokiweka hadharani.

Kama unakumbuka hata mlipuko wa Oklahoma, waamerika walianza tangaza kuwa ni waislaam na dunia ikaanza kuamini kuwa ni waislaam, sasa ni nani akanushe kna kwa jina gani kama sio waislaam kusema sio sisi..Mbona alipopatikana mzungu hawakumpa rangi ama dini yake bali jina lake...
Nimesema inategemea na mwenye nguvu atakavyo address hiyo issue na Wamerekani wametumia neno Waislaam kuwa ndio magaidi so wao wajiite nini kama sio kupitia jina hilo..Hata South tulisema waafrika why not kabila ama Wabantu maanake waafrika wote sio weusi.
Hizi ni tungo mnazotaka kuzitumia wakati sisi tunazo karata lakini kesho likilipuka bomu jingine utasikia Waislaam hawatasema wasomali ama waarabu.... that is my point.
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
Mwafrika wa Kike,
Mamaa vipi tena bado tu hujanielewa?.

Ukitangaza leo kuwa aliyekushambulia ni Musilaam ama niseme Black yule mhusika atajitambulisha vipi?... wewe hapa unajiita Mwafrika wa kike hivi unataka mimi nitumie jina gani?.. Uke wako ama kile unachokiweka hadharani.

Kama unakumbuka hata mlipuko wa Oklahoma, waamerika walianza tangaza kuwa ni waislaam na dunia ikaanza kuamini kuwa ni waislaam, sasa ni nani akanushe kna kwa jina gani kama sio waislaam kusema sio sisi..Mbona alipopatikana mzungu hawakumpa rangi ama dini yake bali jina lake...

Nimesema inategemea na mwenye nguvu atakavyo address hiyo issue na Wamerekani wametumia neno Waislaam kuwa ndio magaidi so wao wajiite nini kama sio kupitia jina hilo..Hata South tulisema waafrika why not kabila ama Wabantu maanake waafrika wote sio weusi.

Hizi ni tungo mnazotaka kuzitumia wakati sisi tunazo karata lakini kesho likilipuka bomu jingine utasikia Waislaam hawatasema wasomali ama waarabu....
that is my point.

Mkandara baada ya ufafanuzi huu nimekuelewa kuwa tatizo ni jina lipi linalotumiwa na mwenye nguvu na sio uhalisia wa mambo katika issue yenyewe.

Kama ni hivyo basi nadhani tunaojaribu kuweka ukweli hapa, tuseme kuwa kinachoendelea iraq ni vita dhidi ya binadamu wenzetu na wala sio vita dhidi ya waislam kama vile ambavyo vita dhidi ya grenada, panama, colombia, vietnam, nk haikuwa vita dhidi ya wakristo!

Otherwise, mkuu mimi ni moja kati ya watu wanaopinga hii vita ya Iraq kwa nguvu kubwa na kama ungejua nick yangu ninayotumia kwenye liberal blogs au forums ungejua kuwa ni vigumu kuwa liberal in America na at the same ukakubali kile Busha anafanya.

Katika hili ninaamini kuwa watu wengi hawaipendi hii vita na pia kuwa hao watu si lazima wawe waislam kupinga hii vita. Ndio maana ninasapoti kupinga hii vita zaidi kama binadamu kwanza na wala sio kama muislam pekee
 
Lizy

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
412
500
Hili ni kweli na mimi nakubaliana nalo..... lakini vipi kuhusu mabango na sentiment kuwa wanapiga suala la Bush kuwauwa waislam (na wala sio waarabu au wasomali au waburushi?).

MWK,
Hapa una ulimaanisha Waarabu, Wasomali na Waburushi wote ni Waisalam, kwamba hawana madhehebu mengine kama Ukristo ama ulikuwa na maana ingine? Coz if that what you meant, nasikitika kukujulisha kwamba you were complitely wrong.
Hivi mnajua baadhi ya walioandamana kupinga ujio wa Bush kesho yake ndiyo walikuwa wamejipanga na vibendera vya Marekani wakinyosha mikono ili wampungie?

Thibitisha.......
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,203
2,000
Mwanakjj login zako za mwafrika wa kike umeziuza au uliziweka ktk stock market?...people knows u...wale waliomtosa Lowassa ni wale wasiri wake...na wale uliowapa nyeti zako zikaleak kwa wengine...

nice try..! mbona mimi sijifichi anayetaka kunijua ananijua! Ila nawasikitia wanaojaribu kunibatiza majina mengi hapa. No, natumia jina moja tu wenye kazi ni ninyi wenye majina zaidi ya moja.. ila ukinihusisha na watu kama MwK naona fahari!!
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
MWK,
Hapa una ulimaanisha Waarabu, Wasomali na Waburushi wote ni Waisalam, kwamba hawana madhehebu mengine kama Ukristo ama ulikuwa na maana ingine? Coz if that what you meant, nasikitika kukujulisha kwamba you were complitely wrong.
...

Lizy,

Mimi kama liberals wengi hapa US tunapinga hii vita ya Kichaka kwa sababu tunawajali hao watu wengine kwa binadamu kwanza kabla ya kujali dini zao. Nikiona mtu Somalia anateseka basi mimi namuona kama Msomali na wala sio kama muislam. The same thing kwa watu wa Iraq na kadhalika.

Nadhani umesoma baadhi ya wadini hapa walivyojibu swali langu kuwa wanaokufa Iraq ni waarabu au ni waislam... wao wamejibu haraka kuwa ni waislam. Hiki ndio kitu Mkandara anajaribu kutoa hapa ili watu wachukuliane kama binadamu kwanza na sio kama watu wa dini moja.
 
Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,203
2,000
mwafrika said:
wa kike;144548]Hili ni kweli na mimi nakubaliana nalo..... lakini vipi kuhusu mabango na sentiment kuwa wanapiga suala la Bush kuwauwa waislam (na wala sio waarabu au wasomali au waburushi?).

MWK,
Hapa una ulimaanisha Waarabu, Wasomali na Waburushi wote ni Waisalam, kwamba hawana madhehebu mengine kama Ukristo ama ulikuwa na maana ingine? Coz if that what you meant, nasikitika kukujulisha kwamba you were complitely wrong.
Hivi mnajua baadhi ya walioandamana kupinga ujio wa Bush kesho yake ndiyo walikuwa wamejipanga na vibendera vya Marekani wakinyosha mikono ili wampungie?

Thibitisha.......

did I say Baadhi? thibitisha kwamba hawakuwamo!
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Mwafrika wa Kike,
Matumizi ya wale wanaoonewa Iraq ni swala la mwenye nguvu yaani siku Marekani wakisema kwa nguvu moja kuwa Wairaq badala ya kutumia dini tena sasa wameanza kusema Sunni, Shia Kurdish itakuwa vigumu sana kwa muislaam kuweza kutenganisha vitu hivyo. Maanake serikali inapoposema Mkerewe ama Msukuma wamefanya hivi basi ni kazi kubwa kwa mtu mdogo kama mimi kuibadilisha kesi iwe ya Mtanzania - hasa ukiwa huna nguvu.

Mwenye nguvu ataendelea kukuita hivyo hadi pale utakapoweza kumshinda kimsingi kama walivyoweza fanikiwa ndugu zetu weusi wa Marekani. Otherwise hii ni ndoto na nitazidi kusema kuwa hapahapa tunatumia neno waandamanaji kuwa ni Waislaam hali hao watu hawakubeba mhuri wa Uislaam usoni isipokuwa addressing, mabango, wao ni toka msikitini basi bila shaka hawa ni waislaam. Magazeti yote yakaandika Waislaam - which is true, kwa nini ifichwe? Lakini kulingana na matakwa yako haikutakiwa kusemwa hivyo. Mfano wa South America ni mzito sana kwani ndio nchi pekee duniani iliyokwisha adopt fully culture za Kigeni yaani wao ni Waspanish ama Portuguese. Wameihsa poteza kabisa identity yao huwezi kulinganisha na mgogoro utakao tokea Afrika, China ama India ambako rangi na dini bado ni ID ya wakazi..Mbona China inalaumiwa kwa kuwakandamiza wananchi wa Tibet hawatumiii neno Wachina isipokuwa dini yao - Budhism?.. how do we address that? wote Wachina hawa tofauti zao ni zinatokana na dini, na ajabu dunia nzima inaunga mkono haki ya watu hawa kuongozwa na dini, not muslims though...

Mwisho jamani hili halikuwa swala la waislaam kukataa ujio wa Bush, nitarudia kusema huwezi kumkataza Bush kuja nchini kwa maandamano hali mtu mwenyewe tayari yuko safarini... Sasa mabango ya nini ikiwa mtu huyo hatafika nchini kuweza kuyasoma?....
I Mean mbona Tanzania bado kabisa hatujafahamu maana ya maandamano?.. siku zote unaandamana kupinga kilichopo na kama hawakutaka aingie nchini nina hakika wangeenda uwanja wa ndege na kulala ktk runaway wakachukua virungu, ama wangechoma matairi ndege isipate kutua.
Hizi ni mbinu za magazeti yetu hasa yayayoongozwa na waandishi wenye nia chafu, sawa na baadhi magazeti ambayo ndio chombo chenye nguvu ya kutapakaza ujinga.

Waislaam waliandamana kupinga American Policy nchi za nje chini ya Utawala wa Bush!..victims ni waislaam nahata kam wangekuwa wanawake na wakristu tungesema ama kuandika hivyo.
 
Lizy

JF-Expert Member
Feb 11, 2008
412
500
Hivi mnajua baadhi ya walioandamana kupinga ujio wa Bush kesho yake ndiyo walikuwa wamejipanga na vibendera vya Marekani wakinyosha mikono ili wampungie?..

Hata Mimi (kama ulivyo wewe), siwezi kuthibitisha kama walikuwepoa ama hawakuwepo. Ila ingependeza zaidi kama ungesema "INAWEZEKANA" kuliko "HIVI MNAJUA"
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
Mwafrika wa Kike,
Matumizi ya wale wanaoonewa Iraq ni swala la mwenye nguvu yaani siku Marekani wakisema kwa nguvu moja kuwa Wairaq badala ya kutumia dini tena sasa wameanza kusema Sunni, Shia Kurdish itakuwa vigumu sana kwa muislaam kuweza kutenganisha vitu hivyo. Maanake serikali inapoposema Mkerewe ama Msukuma wamefanya hivi basi ni kazi kubwa kwa mtu mdogo kama mimi kuibadilisha kesi iwe ya Mtanzania - hasa ukiwa huna nguvu.

Mkandara,

Huu ugomvi wa majina hata hapa US unaendelea sana. Kama kuna issue ya minorities, utaisikia wanasema blacks, au hispanics, au jewish americans lakini kama ni issue ya weupe husikii mtu akisema kwenye news kuwa hao ni white americans.

Nadhani hili ni tatizo kubwa sana kuliko ninavyoweza kusema kwa sababu kama unakumbuka uchaguzi uliopita na huu unaendelea bado watu wametumia dini za watu kama Catholics na Mormon kutaja watu hapa.

Hili ni tatizo kubwa na ninaungana na wewe kupiga vita hizi labelz hapa (in this context).

Mwenye nguvu ataendelea kukuita hivyo hadi pale utakapoweza kumshinda kimsingi kama walivyoweza fanikiwa ndugu zetu weusi wa Marekani. Otherwise hii ni ndoto na nitazidi kusema kuwa hapahapa tunatumia neno waandamanaji kuwa ni Waislaam hali hao watu hawakubeba mhuri wa Uislaam usoni isipokuwa addressing, mabango, wao ni toka msikitini basi bila shaka hawa ni waislaam. Magazeti yote yakaandika Waislaam - which is true, kwa nini ifichwe? Lakini kulingana na matakwa yako haikutakiwa kusemwa hivyo. Mfano wa South America ni mzito sana kwani ndio nchi pekee duniani iliyokwisha adopt fully culture za Kigeni yaani wao ni Waspanish ama Portuguese. Wameihsa poteza kabisa identity yao huwezi kulinganisha na mgogoro utakao tokea Afrika, China ama India ambako rangi na dini bado ni ID ya wakazi..Mbona China inalaumiwa kwa kuwakandamiza wananchi wa Tibet hawatumiii neno Wachina isipokuwa dini yao - Budhism?.. how do we address that? wote Wachina hawa tofauti zao ni zinatokana na dini, na ajabu dunia nzima inaunga mkono haki ya watu hawa kuongozwa na dini, not muslims though...

Mkuu katika hili angalia kuwa hata wanaotetea maandamano hapa wamesema wenyewe kuwa haya ni maandamano ya waislam na wanatetea issue za waislam. Hapa ndipo nilipoingia katika debate hii ili kuondoa dhana kuwa hii ni issue ya dini fulani pekee (kumbuka mfano wangu wa wanafunzi wa mlimani).

Mwisho jamani hili halikuwa swala la waislaam kukataa ujio wa Bush, nitarudia kusema huwezi kumkataza Bush kuja nchini kwa maandamano hali mtu mwenyewe tayari yuko safarini... Sasa mabango ya nini ikiwa mtu huyo hatafika nchini kuweza kuyasoma?....
I Mean mbona Tanzania bado kabisa hatujafahamu maana ya maandamano?.. siku zote unaandamana kupinga kilichopo na kama hawakutaka aingie nchini nina hakika wangeenda uwanja wa ndege na kulala ktk runaway wakachukua virungu, ama wangechoma matairi ndege isipate kutua.
Hizi ni mbinu za magazeti yetu hasa yayayoongozwa na waandishi wenye nia chafu, sawa na baadhi magazeti ambayo ndio chombo chenye nguvu ya kutapakaza ujinga.

Nadhani part ya hii debate itaendelea kuelemisha katika hili na ninaikubali shule unayoendelea kutoa hapa.

Waislaam waliandamana kupinga American Policy nchi za nje chini ya Utawala wa Bush!..victims ni waislaam nahata kam wangekuwa wanawake na wakristu tungesema ama kuandika hivyo.

Kama wao hawakusema kuwa hayo ni maandamano ya waislam na badala yake ni vyombo tu vya habari vimetaja haya maandamano kama maandamano ya waislam, basi naungana nawe kupinga na kukemea hii label iliyotumika hapa. Otherwise nabaki kwenye hoja yangu ya kwanza kuwa ni vyema kama wangejitambulisha tu kwanza kama watanzania na watetezi wa haki badala ya kutenga wengine kwenye hili.
 
Nungwi

Senior Member
Sep 9, 2006
196
0
Mwanakjj.

Dalili za kushindwa hoja. Mkandara,Zomba,Chuma na wote muacheni huyu bwana ana frastuesheni. hana makaratasi ndio maana ana muabudu Bush.mtu ambaye hawezi kutoka marekani ameshindwa hata kuoa ndoa za magirini.

sehemu yake ya kujiliwaza ni JF, bongoradio.na Tanzania Daima.
rudi nyumbani ukafanye kampeni kama kweli wewe Mwanaume.
mwenzenu hapa ni nyumba kwake kila dakika yuko JF hata bila hoja. akitoka marekani hawezi kurudi. kifupi tunasema hana miguu(green card).

Hii kali na ya Mwaka ujanja wote wa Mwanakijiji kumbe hana karatasi(Leave to remain),jamani msaidie Mtanzania Mwenzetu aje nyumbani.

Mtalii- acha hizo ina maana ilipofungiwa JF mwenzetu alikuwa mgonjwa?

Mwanakijiji.

Kweli huwezi kutoka na kuingia Marekani?
 
Mkandara

Verified Member
Mar 3, 2006
15,536
2,000
Mwafrika wa Kike,
Mkuu katika hili angalia kuwa hata wanaotetea maandamano hapa wamesema wenyewe kuwa haya ni maandamano ya waislam na wanatetea issue za waislam. Hapa ndipo nilipoingia katika debate hii ili kuondoa dhana kuwa hii ni issue ya dini fulani pekee (kumbuka mfano wangu wa wanafunzi wa mlimani

Shukran, Kwanza soma sentesi yako ya kwanza inayohusu wenye nguvu, umesema hata Marekani hu - lebel watu hasa minority lakini sio sivyo inapokuwa ni Wazungu... Yet, umeshindwa kuelewa kuwa hawa minority wa Marekani watakapo andamana wataandamana kwa rangi zao na kijieleza hata kama watakuwemo Wazungu kati yao. Huwezi kupigania equal right Marekani bila kujieleza una represent kundi gani?.. hivyo basi hata Blacks Marekani hujitambulisha/hutambulishwa wao kama blacks pamoja na kwamba wanaoandamana sio wote blacks.
Ndivyo ilivyokuwa Dar, walioandamana hawakuwa wote waislaam, pili nilishasema kuwa neno Waarabu linakuwa lina limit mipaka ya malalamiko ya hawa waislaam kwani swala sio Iraq tu..lakini kinachowaunganisha wote hawa ni dini yao.
Mkuu, ebu jiulize hivi, pamoja na yote haya inakuwaje Obama anashangiliwa zaidi nchi za Kiislaam na ni hope ya wengi ikiwa Obama sio Muislaam na pia ni Mmarekani kama alivyo Bush.... Why mnashindwa kuelewa hilo ama kwa sababu Mnamtazama Bush kama ni mkristu, hivyo waislaam wana mpinga kwa sababu ana represent Wakristu!... Najua ndivyo walivyokuwa wakifikiria wazungu wengi enzi za Mkoloni - Ukipinga Ukoloni basi bila shaka unawachukia wazungu..Je, ni hiki mnachokiogopa?...kama ndivyo how come nchi hizo hizo zina mahusiano mazuri na nchi kama Italy, France, Germany na hata Vatican?

Unajua Mwafrika wa Kike nadhani kuna maswala mengine ni vigumu kwako kuelewa ikiwa wewe sio Muislaam kama vile tunavyoshindwa kuelewa mambo mengine ya wanawake!..
Mimi nilitegemea itakuwa rahisi kwenu kuelewa kwa sababu yamekwisha kufikeni, kwani Ubaguzi wa South Afrika na Zimbawe hatukuusema kwa makabila yaliyohusika (Wazuru, Nkosa, Washona ama Wandebele) wala hatukuwaita Wa south au Wazimbabwe wanaonewa! bali tulitumia kile kinachotuunganisha sisi sote nacho ni weusi wao kutokana na Apartheid yenyewe ilivyowatenga. Na hakika waliotengwa walikuwa weusi sii kwa makabila yao ama Itaifa wao. Huu ni ukweli ambao haupendezi masikioni but the fact remains kuwa weusi ndio waliopata matatizo ya Ubaguzi South, bila kujali kabila zao ama Utaifa wao. Na kama ingelikuwa kwa dini zao ni lazima tungetumia dini. Zipo nchi tunalalamika kuhusu uhuru wa Wakristu sehemu hizo na hatuwaiti ati Waarabu, bali ile sababu iliyofanya kutengwa.
Leo ktk swala la Iraq au Afghanstan mnataka tuseme Waarabu hali ubaguzi wa mzungu unasema wazi kuwa Magaidi (terrorists) ni Waislaam hawasemi Waarabu, hivyo wameidhinisha miswada ya kuwafuata huko huko kwao - Nchi za Kiislaam, regarless of their nationality.
 
Mwafrika wa Kike

JF-Expert Member
Jul 5, 2007
5,192
0
Shukran, Kwanza soma sentesi yako ya kwanza inayohusu wenye nguvu, umesema hata Marekani hu - lebel watu hasa minority lakini sio swala linapokuwa ni Wazungu... Yet umeshindwa kuelewa kuwa hawa minority wa Marekani watakapo andamana wataandamana kwa rangi zao na kijieleza hata kama watakuwemo Wazungu. Huwezi kupigania equal right Marekani bila kujieleza mna represent kundi gani?.. hivyo basi hata Blacks Marekani hujitambulisha/hutambulishwa wao kama blacks pamoja na kwamba wanaoandamana sio wote blacks.

Katika hili tumekubaliana mkuu na nimekuelewa.

Ndivyo ilivyokuwa Dar, walioandamana hawakuwa wote waislaam, pili nilishasema kuwa neno Waarabu linakuwa lina limit mipaka ya malamiko ya hawa waislaam kwani swala sio Iraq tu..
Mkuu, ebu jiulize hivi, pamoja na yote haya inakuwaje Obama anashangiliwa zaidi nchi za Kiislaam na ni hope ya wengi ikiwa Obama sio Muislaam na pia ni Mmarekani kama alivyo Bush....

Asante pia kufanua hili na ninadhani sasa tuko kwenye page moja zaidi katika hili kuliko tulipoanza.

Why is mnashindwa kuelewa hilo ama kwa sababu Mnamtazama Bush kama ni mkristu, hivyo waislaam wana mpinga kwa sababu ana represent Wakristu!... Najua ndivyo walivyokuwa wakifikiria wazungu wengi enzi za Mkoloni - Ukipinga Ukoloni basi bila shaka unawachukia wazungu..Je, ni hiki mnachokiogopa?...kama ndivyo how come nchi hizo hizo zina mahusiano mazuri na nchi kama Italy, France, Germany na hata Vatican?

Approval ya Bush hapa US ni chini ya asilimia 30. Hii itakuonesha ni wakristo wangapi wanampinga Bush - jibu rahisi ni kuwa ni wengi sana.

Unajua Mwafrika wa Kike nadhani kuna maswala mengine ni vigumu kwako kuelewa ikiwa wewe sio Muislaam kama vile tunavyoshindwa kuelewa mambo mengine ya wanawake!..
Mimi nilitegemea itakuwa rahisi kwenu kuelewa kwa sababu yamekwisha kufikeni, kwani Ubaguzi wa South Afrika na Zimbawe hatukuusema kwa makabila yaliyohusika (Wazuru, Nkosa, Washona ama Wandebele) wala hatukuwaita Wa south au Wazimbabwe wanaonewa! bali tulitumia kile kinachotuunganisha sisi sote nacho ni weusi wao kutokana na Apartheid yenyewe ilivyowatenga. Na hakika waliotengwa walikuwa weusi sii kwa makabila yao ama Itaifa wao. Huu ni ukweli ambao haupendezi masikioni but the fact remains kuwa weusi ndio waliopata matatizo ya Ubaguzi South, bila kujali kabila zao ama Utaifa wao. Na kama ingelikuwa kwa dini zao ni lazima tungetumia dini. Zipo nchi tunalalamika kuhusu uhuru wa Wakristu sehemu hizo na hatuwaiti ati Waarabu, bali ile sababu iliyofanya kutengwa.

Mkandara huu ni ukweli ingawa pia naona kuwa likishaingia suala la dini linatenga watu zaidi ya kuwaunganisha pamoja. Otherwise point yako nimeipata.

Leo ktk swala la Iraq au Afghanstan mnataka tuseme Waarabu hali ubaguzi wa mzungu unasema wazi kuwa Magaidi (terrorists) ni Waislaam hawasemi Waarabu, hivyo wameidhinisha miswada ya kuwafuata huko huko kwao - Nchi za Kiislaam, regarless of their nationality.

Mi sidhani kama nimeshauri nani aitwe mbaguzi lakini nadhani ukifuatilia number ya watu wanaopiga hizi vita za kichaka hapa US basi utaona jinsi hili swali linavyovuka mipaka ya kawaida ya dini na imani.

Asante sana kwa maelezo yako na nakuhakikishia kuwa nimekuelewa zaidi hapa na sina ubishi tena mkuu - yaani hoja yako imeshinda ya kwangu mkuu.

Asante
 
Asha Abdala

JF-Expert Member
Mar 21, 2007
1,133
0
Eti watu wanaandamana .....walikuwa wanapinga nini?

zile 700m USD,au joji mtembezi kichaka kuja bongo au marekani na sera zake za nje au marekani na sera zake za ndani au nini hasa...

maana naona wamechoma hadi bendera ya marekani ...

kazi kweli kweli....

Mtizedi

Na hawa walioandamana nao ni wakabila kama CHADEMA? Au na wenyewe ulijua tu watakereka?

Asha
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom