Taarifa: Usalama Wangu Hatarini

Taarifa: Usalama Wangu Hatarini

Nawashukuru nyote kwa kunipa moyo pamoja na ushauri juu ya jinsi gani naweza kukabiliana na hili,kwa njia za kujihami lakini pia kwa njia ya sala;lakini muhimu zaidi - nafarijika sana kwamba maoni na ushauri wenu unatoka kwa watanzania wote bila ya kujali kwamba mitazamo na itikadi zetu za kisiasa zinatofautiana,kwa mfano ben saanane na wengineo,that's the revolution that we need,siasa za masimango,chuki na visasi tuwaachie wazee;sisi kama vijana tunaweza tofautiana kiitikadi na mtazani lakini tukiwea mbele maslahi ya taifa,tofauti hizi hazitabomoa bali zitajenga taifa letu kama ilivyo katika demokrasia zenye mafanikio kama marekani,uingereza,japan,s.korea n.k;

;Lakini kwa wale pia ambao wananikejeli katika hili,nachukulia kejeli hizo positively kwani zinachangiwa zaidi na kuchoka kwenu na matatiizo sugu ya kila nyanja yanayolikabili taifa letu huku waathirika wakubwa ikiwa na walipa kodi na wakulima wanaotulisha na pia kutufanya tutembee vifua mbele kwamba siku moja na sisi tutakuwa taifa linalo jitegemea na la kipato cha kati;

Mwisho,niwahakikishie tu wale wote wenye kuniunga mkono katika hili kwamba sitaacha nachofanya kwani situmikii mtu bali moyo wangu;vinginevyo kama ningekuwa mwoga na dhaifu,ningeacha siku nyingi baada ya mzee wangu balozi mwambulukutu kuvamiwa afrika kusini mwaka 2007 kwa nia ya kuuwawa kwa sababu za kisiasa huku taarifa za nyumbani Tanzania zikisambazwa kwamba ilikuwa ni tukio la ujambazi huku uchunguzi juu ya tukio husika afrika ya kusini ukishinikizwa usimamishwezi;anyways,hayo yalishapita,kikubwa ni uzima ingawa wahusika wamefaniwa kumpofua macho;

Again,shukrani na pamoja sana;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Dha dha dha dha!!! Lakini Yuko Mungu aliye hai!! Mwamini Malaika wako mlinzi kuwa yuko tayari kwa lolote!!
 
Kwani akihama itasaidia nini kulinda usalama wake? mbona mnaandika utafikiri unakimbizwa? Kutishiwa kwake si kwasababu ya UCCM wake bali maneno yake yanawachukiza wanaoguswa! @Dr Slaa yuko Chadema mbona anawindwa kila siku?

Magamba hawawezi kumuwinda "Mchambuzi", yakimtaka yanamkamata kama kuku! Magamba yanawinda mtu aliyeyaa gamba kisha anawachokonoa huku naye anafaidi matunda ya ufisadi, umesahau alivosema EL kuwa, maadui wake wabaya ni wale walioko ndani ya CCM, walioko nje ya CCM hawamsumbui hata kidogo kwani ni rahisi kuwashughulikia!

Sisi kama watanzania tutaonea huruma wangapi wanaolamba viatu vya mafisadi kwa unafiki wao? Sita kila siku anawasema mafisadi live na halalamiki kuwa wanataka kumtoa meno! Mchambuzi ni mjinga (natumia neno zuri 'mjinga' siyo mpumbavu), sasa tuna muelimisha ujinga umtoke ili avue gamba. Kama taendelea kukaa huko watam-sodomize ndipo atakapopata akili ya kuhama!
 
Mwandishi wa makala katika gazeti la raia mwema anaeitwa Joseph Mihangwa, alishawahi kuandika makala yenye kichwa "TAIFA LETU MIKONONI MWA GENGE LA MAFIA"
 
pole sana Kamanda,mapinduzi daimaa,usirudi nyuma,ulizaliwa mala moja na utakufa mala moja,hata atakayekudhuru nae atakufa mala moja,hakuna atakaye baki ktk hii dunia.
ujio wa xijiping ni matunda ya baba wa taifa,aliweka misingi na sasa wanaofaidi ni sisi,nawe usihofu,weka misingi imala na manufaa yake utayaona,hata kama hutofaidi wewe na mimi watafaidi vijana wetu
Tupo pamoja ktk hili na ikiwezekana lipoti visa hivi polisi ili likitokea wajue wapi pa kuanzia
 
Ndugu wana JF, hasa wadau wenzangu jukwaa la siasa,nimeona kuna umuhimu wa kuwapa tu taarifa kwamba nimepotea kidogo humu ili kujipanga kutokana na vitisho navyokumbana navyo kutokana na michango yangu mbalimbali humu,hasa kuhusiana na misimamo yangu dhidi ya madhaifu ya chama changu cha CCM kuelekea 2015;kwa wengi,naamini watakubaliana nami kwamba lengo langu limekuwa ni kujenga,sasa hawa wachache kwa mtazamo wao ni kwamba nabomoa chama (CCM) kuelekea 2015; vitisho hivi havijaanza leo lakini hivi karibuni,kasi imekuwa kubwa zaidi; mbali ya kupokea vitisho,pia nimedokezwa na vyanzo vyangu vya kuaminika sana kuhusu mpango uliopo wa kunidhuru,hivyo niwe makini hasa in the public arena na nimetajiwa wahusika kwa "majina" na "kitaasisi"!

Ndugu zangu,ningependa kuwahakikishia kwamba pamoja na vitisho hivi ambavyo vinaweza kupelekea mtu kuteswa, kuwa sodomized na hata kuuwawa kijasusi, sitaacha kukipigania chama changu cha CCM kwani nafanya hivyo kwa msukumo wa ninacho kiamini,lakini hasa mapenzi yangu kwa nchi yangu ya Tanzania,na nina amini kwa dhati kabisa matatizo ya sasa ya ccm ni matokeo ya waharibifu wachache ambao watapita tu na kwenda zao na kutuachia chama ambacho ili kirudi katika uimara wake,kitahitaji ujenzi mpya (ndani au nje ya ikulu) wa kuzungumza tena na the common man na kuelewana nae, na hivyo ndivyo tutaweza kuleta ushindani wa kweli dhidi ya chama makini cha chadema au chama chochote kingine; Lakini ni muhimu kwa wana ccm wenzangu tukubali ukweli kwamba sasa ni chama cha watu,sio chama cha viongozi;pia tuwe consistent,tusiwe watetezi wa ccm kutokana na awamu au nani yupo ikulu basi tuwe watetezi wa ccm kutokana na mapenzi yetu ya kwa taifa ambapo chama ni njia pekee ya kuboresha taiga hilo kupitia uongozi;

Vinginevyo CCM kamwe haiwezi kufa lakini pia ni dhahiri kwamba Chadema nayo haiwezi kufa,kwahiyo wana ccm wenzangu,hasa vijana wa sasa na wa baadae, tusipoteze muda kwa kujidanganya juu ya hilo; nadhani ni muhimu sasa tufikie level of maturity in liberal democracy na kukubali kwamba chadema is here to stay,and just like sisi ccm,chadema (na wapinzani wengine) wana haki ya kutafuta ridhaa ya wananchi kushika dola ili kuwaongoza kuelekea Tanzania yenye neema; CCM tukifanikiwa kutambua ukweli huu, basi uelewa huu utakuwa ni mwanzo mkubwa sana wa mageuzi makubwa sana ndani ya chama chetu kwani kwanza tunahitaji mageuzi ya fikra;tukiweza hilo, tutaanza kuwa washindani wa hoja badala ya viroja na jazba na hivyo kufanikiwa kurudisha imani ya umma kwa chama chetu ambayo inazidi kuzorota kuelekea 2015; Vijana wenzangu,tuhamie kwenye siasa za hoja mbele ya wananchi zenye outcome ya kupokezana vijiti kwa amani na utulivu kwani hiyo ndio maana ya kukubali demokrasia ya uliberali 1992;kwenye demokrasia nyingi zenye mafanikio, vyama hupokezana uongozi wa nchi kwa amani na utulivu,na anayeshindwa huchukulia hilo kama changamoto ya kujipanga upya;Chadema kutushinda CCM uchaguzi ngazi ya udiwani,ubunge na hata urais doesn't mean it is the end na badala yake it should mark a new beginning and an era inayotawaliwa na mapinduzi ya kifikra; Kujiita chama cha mapinduzi sasa iwe na maana ya mapinduzi ya fikra;katika hili,naamini kabisa ndani ya ccm huko Lumumba na kwingineko kwenye nafasi za maamuzi, wapo vijana wenye uwezo to set a precedent kwa wadogo zetu waliopo huko mashuleni,vyuoni n.k,hasa wale ambao bado wana imani na CCM;ni suala la uamuzi tu kwa vijana wana ccm katika nafasi husika,na pia, mshikamano miongoni mwao hasa dhidi ya divisive forces, na vile vile kuweka maslahi ya taifa mbele kabla ya maslahi ya chama; the precedent ni muhimu kwa vijana watakaotufuatia baadae kuja kuimarisha na kugeuza utamaduni wa ovyo na ubabaishaji mkubwa ndani ya CCM ya leo;

Vijana wenzangu,muwe ni wana ccm au wana,chadema...naamini kabisa kwamba wengi wetu lengo ni moja - kuboresha maisha ya watanzania,na iwapo inatokea tunapishana,basi ni juu ya jinsi gani au njia bora zaidi ya kufikia lengo husika; Kama zitto alivyopata nena kwenye kipindi kimoja cha star tv mwishoni mwa mwaka jana,vijana tuna haja ya kuacha kuiga siasa za wazee zilizojaa majungu,fitina na visasi,badala yake tuungane kujenga taifa letu kwa ari mpya,na iwapo tunatofautiana basi iwe kwa hoja juu ya jinsi gani kila chama kinaamini njia ipi ni bota katika kufikia Tanzania yenye neema kwa maslahi ya walio wengi,huku tukiachia wananchi kufanya maamuzi baada ya kuchekecha hoja;

Nahitaji sana sala zenu,

Mungu ibariki Tanzania.


Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Jipange upya kuongopa ktk mazingira ya kificho hapo umecheka hizo ni sanaa ndogondogo sana
 
You are coward and i don't think wewe ni mpiganaji wa ccm kama niaje angalia uwezekano...,ccm ina wanajeshi wakutosha wa kukipigania si kama cdm inanguzo chache moja ikidondoka nacho kinapumulia machine .

huko magambani mnapigania nini?
 
........vinginevyo kama ningekuwa mwoga na dhaifu,ningeacha siku nyingi baada ya mzee wangu balozi mwambulukutu kuvamiwa afrika kusini mwaka 2007 kwa nia ya kuuwawa kwa sababu za kisiasa huku taarifa za nyumbani Tanzania zikisambazwa kwamba ilikuwa ni tukio la ujambazi huku uchunguzi juu ya tukio husika afrika ya kusini ukishinikizwa usimamishwezi;anyways,hayo yalishapita,kikubwa ni uzima ingawa wahusika wamefaniwa kumpofua macho;

Again,shukrani na pamoja sana;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums

Daaaah, mkuu una moyo wa ajabu sana, kwa haya tu inaonyesha huna sababu ya kuwa CCM
 
Hivi nchi yetu inaelekea wapi? Kwani kutofautiana kwa mtazamo unakuwa adui wa kuuliwa?
 
Mchambuzi pole, Mkuu wewe ndiye MARCOSSY ALBINEY (KAMA SIJAKOSEA MAWANAHARAKATI), Kama ni wewe Kunauzi ulikuja humu kuwa umehama nyumbani kwako kwa vitisho kama hivi vya mchambuzi ni kweli ama-Thibitisha kama ndiye wewe ?? Kma siye wewe niwie radhii mkuu

Alishajitaja mwenyewe hapa jamvini,anaitwa Mpoki
 
Magamba hawawezi kumuwinda "Mchambuzi", yakimtaka yanamkamata kama kuku! Magamba yanawinda mtu aliyeyaa gamba kisha anawachokonoa huku naye anafaidi matunda ya ufisadi, umesahau alivosema EL kuwa, maadui wake wabaya ni wale walioko ndani ya CCM, walioko nje ya CCM hawamsumbui hata kidogo kwani ni rahisi kuwashughulikia!

Sisi kama watanzania tutaonea huruma wangapi wanaolamba viatu vya mafisadi kwa unafiki wao? Sita kila siku anawasema mafisadi live na halalamiki kuwa wanataka kumtoa meno! Mchambuzi ni mjinga (natumia neno zuri 'mjinga' siyo mpumbavu), sasa tuna muelimisha ujinga umtoke ili avue gamba. Kama taendelea kukaa huko watam-sodomize ndipo atakapopata akili ya kuhama!

Hapo kwenye red ndio kunakufanya useme yote hayo!
 
Pole sana Mkuu Mchambuzi.....Ila ni vizuri tukajiuliza maswali yafuatayo:
  1. Wamekutambua pamoja na kutumia hiden ID?na kama ndivyo ni kwa kiasi gani JF members wapo salama katika hili wimbi la kung`olewa kucha?
  2. Ukiona vipi waachie lichama lao karibu huku....:rockon:

Tatizo anatumia picha yake halisi
 
That is the thing...nakubaliana nawe Ngalikihinja. Hiyo ndiyo ilipaswa kuwa hoja. Pamoja.

Tumani wewe wakati mwingine una matatizo sana, unakosa staha za kichadema. Mwenzako katishwa maisha wewe unajenga hoja uchwara hapa. Wakati mwingine unakosoa hadharani hata thread za viongozi wenzako wa Chadema hadharani. Halafu sisi wengine mnatufundisha nini?
 
Nyerere mwenye(RIP),nahisi walimfanyia.Kuna Sokoine,Kolimba,Mwakyembe,Mwandyosa na wengineo wengi tu,achilia mbali walioteswa na kuuwawa chini ya serikali ya ccm kama kina Dr Ulimboka,Kibanda,Mwangosi na wengineo wengi tu.

CCM walishawahi hadi kuwekeana uchawi bungeni wakati wa issue ya "unga unga" wa kina Chenge.

Mkuu kama ni kweli huogopi kufa na unaipenda ccm kiasi hiki,basi kila la kheri.
 
pole sana Mchambuzi

vema umelitambua hilo mapema

hao watishaji wanaamini wakikumaliza ndio moto wa mapinduzi utazimika?
 
huko magambani mnapigania nini?

maslahi ya watanzania wote kwa ujumla si ya sehemu flani au kabila au dini.
Chama cha CCM kina wajali wananchi wake si chama cha kusacrifice watu kwa manufaa ya wachache.
 
Tunapitia katika kipindi cha mateso. Watesaji ni Watanzania wenzetu wanatumia kodi zetu kututenda. Kwa post hii inaminisha kabisa watoa meno, kucha, macho, wauaji nk ni viongozi wa CCM wakitumia wanausalama wetu.

Ukiishi naye lazima ukubaliane naye, ukipingana naye hawezi kukupenda wala kukubali ndio maana wengi wakamkimbia.
Mchambuzi sioni ni kwa jinsi gani utaweza kuibadilisha CCM ukiwa ndani.

Moja unaowaita wazee tayari wameandaa vijana wenye mawazo kama yao, utesaji kama wao na kulindana. Tayari vijana walio wengi wa CCM wameshiriki kumtesa mtanzania kwa wizi, rushwa, ufisadi,hujuma nk haiwezekani hawa vijana wa CCM kuja kuwa bora hata siku moja.

Angalia Mwigulu na matukio yote ya utesaji, mauaji anatajwa, Sikiliza Nape alivyokeli kuteswa kwa Kibanda. Sikiliza Riz alivyolihadaa taifa kwa kukana maandishi yake, wapi Ngeleja na masha na utendaji wao. Wapo Jerry Slaa na matamshi yake. Je hawa ni wazee mkubwa???

Watesaji na wauaji wako ni vijana ambao kwao ndio anguko la CCM ni hatari kuliko wazee. Vijana wa CCM ndio wabaya zaidi kuliko hao wazee unaowaogopa. Kwa kifupi ukipingana na CCM ndani ya CCM kila mmoja mzee na kijana atakutoa menu na kucha bila ganzi.

Vitisho ni real, na lazima uwe makini, ila kama tayari fungu la kukutoa kucha limeshatolewa kaka sioni pa kutokea. Mwakyembe aliripoti kila sehemu mpaka ikulu ila walimkabidhi kitu yake.

Maaskofu walitoa ripoti za kuuwawa wao na mapadri ila haikusaidia kubeep watawala wakafanya kweli. Mwangosi aliwapelekea taarifa za vitisho wakamaliza wenyewe. Kama wamempofua dingi na wameishi naye kwa miaka mingi wanajuana vizuri ijekuwa wewe ???

Unatetea vipi mfu? Ili CCM iwe imara lazima ife kwanza. Uhai wako ni bora sana, ni vyema ungetumia busara kupima kama unatetea mabadiliko au unapoteza nguvu kutetea wafu. Hakuna kitu wanaCCM viongozi hawajui wameamua kufanya wafanyavyo kwa makusudi. wanajua kabisa kwamba wao ni wezi, wavivu, walafi, hawana huruma, wanyama, wako tayari kula rushwa kuliko kutengeneza choo wanachotumia. Angalia ofisi zao zilivyochafu, angalia hospitalia zao zilivyo mbovu. Mtu asiyejijali yeye mwenyewe hawezi kukujali wewe.

Kubali kung'olewa kucha au achana na wang'oa kucha.
 
I really feel sorry for u...trying to feel and share the situation and pains you are facing.

Lakini sasa, Mchambuzi... unamaanisha kwamba wanaokusaka kukung'oa kucha, kukutoa macho au kutaka uhai wako, kwa sababu tu umeamua kufikiria tofauti, ni WAZEE!

Aisee, so vijana wote kwenye chama chenu uko pamoja nao kwenye fikra zako kwa ajili ya chama chenu. Na unataka kutuaminisha kuwa vijana, tena wengine viongozi wakubwa tu, ndani ya chama chenu na walioko kwenye serikali ya chama chenu ni watakatifu na wazeewote ni wapika majungu, wafitini, wanafiki na every kind of such stuff.

Naona kama unakosea katika kujenga premises na hatimaye conclusion. Iangalie vyema ili tusiache jiwe bila kugeuzwa. Uhalisia unaonesha, vijana ni wabaya sana pia, maana wanakabidhiwa mikoba.

Lakini pia wamekuwa wabaya zaidi kwa sababu tu, wanaona wazee wako tayari kuondoka, wakati wao (vijana) hawajala na kujinufaisha na nafasi wanazopewa vya kutosha. So they are ready for anything...torturing, kidnapping and killing their opponents, by any means necessary. Wameshafanya hivyo na bila shaka wanaendelea kupanga hivyo.


Vijana hao hawawezi kabisa kufanya siasa za ushindani wa kuchanyata mawazo na fikra. Tumewaona. Wanajulikana, kwa matendo na maneno yao, hadharani na sirini.


Afadhali baada ya kuedit kidogo. Lazima ujue nafasi yako siyo kukosoa tu kila kitu. Unatuaibisha wakati mwingine.
 
Back
Top Bottom