Taarifa: Usalama Wangu Hatarini

Taarifa: Usalama Wangu Hatarini

Ndugu yangu Mchambuzi ; hamia CHADEMA. Hao CCM si watu wema. Mimi nimewasoma kwa muda mrefu na nimewatumikia kwa hali na mali kwa nguvu zangu zote lakini kwa kipindi chote tangu niwe na akili mpaka sasa nimekuwa nikiwasoma kwa makini na nimegundua CCM ni chama kinacho dhibitiwa na watu
wachache wenye siri kubwa na malengo ambayo ni ya kutia shaka na pengine ya kuogopesha kwa mtu wa kawaida pale anapoyagundua..

Kauli yako ina ukweli mzito (Kumbe tuko wengi!)
 
Last edited by a moderator:
kama mtu anania ya kukudhuru hawezi kuja kukutishia, huo unaitwa mkwara. Jamaa kama anania mbaya na wewe anafanya kweli.

yah ni kweli mkuu, kama mikwara mliowafanyia,nyerere, kombe, kolimba, mwakyembe na baba yake nape ( mwandosya)- ni mikwara tu hiyo. Mia,
 
Huko nako kuna "GAIDI" Lwakatare?? Labda Nchemba

Kama yale kwenye ile video ni ya kweli kama si ya kupandikiza hakika nakuambia Lwakatare naye ni pandikizi ndani ya CDM sema mziki hakuujua kuucheza vizuri maana video inaonesha kabisa kuwa alikuwa attention kutekeleza jambo fulani. Lwakatare ni pandikizi ila by 2015 mapandikizi yote yatajitokeza tu. By the way, hata issue ya Lwakatare haijasisimua umma maana upande wa pili wanatumia deal ambazo ni outdated na watanzania walishajua njama zao. I tell you hakuna kitu chochote kitakuwa planted na upande mwingine au ndani ya mapandikizi CDM kitaitetemesha CDM na badala yake mnakifanyia promosheni!! Aibu kubwa sana.
 
Nimeagiza container mbili toka China yamejaa meno bandia na kucha bandia. Najua soon biashara hii itakuwa inalipa sana hapa Bongo.
 
nani amekutishia maisha? Mtaje
Hili jambo la kumtaja alietishia maisha ni jambo zuri na lenye manufaa.Waswahili husema "ukishamjua mchawi na ukamuambia (ukamuweka wazi ) hawezi kukuloga tena".Mkuu Mchambuzi ; ukiwataja wahusika wataogopa kuendelea kufanya njama za kukuhujumu kwani ikitokea ukidhurika, bundi atalia upande wao.Kadhalika wale wasiojua kwamba ni nani adui wa nchi hii nao watajua sasa! mkuu Mtambuzi wataje watu hao maana hata hivyo hakuna haja ya kumuonea haya mtu asiyekuwa na utu.Kwa kufanya hivyo pia utaviweka vyombo vya usalama katika hali ya tahadhari.Ila usifanye hivyo kama huna ushahidi wa kutosha na wakuaminika maana inaweza kukugharimu vibaya.
 
Last edited by a moderator:
Mkuu,

I have always appreciated unachoandika hapa jamvini. Nimejifunza mengi sana kutoka kwenye threads na posts zako hasa kwenye masuala ya siasa na uchumi. Kama ulichokiandika leo ni kweli au ni uongo, kwa kweli siwezi kujua.

Utakubaliana na mimi kuwa kutokana na yanayotokea nchini hivi karibuni inakuwa vigumu sana kwa a reasonable person kuamini kile anachosema mwanasiasa kuhusiana na yeye binafsi au kinachosemwa na wengine juu ya mwanasiasa kuhusiana na yeye binafsi.

Kutokana na hili basi nimeamua kuwa sitaamini tena kinachosemwa juu ya wanasiasa personally au watakachokuwa wanakisema wanasiasa and other related kuhusiana na mambo yao binafsi ya kisiasa.

Otherwise, nategemea kukutana nawe kwenye hard talk hapa jamvini and wish you all the best.
 
You are coward and i don't think wewe ni mpiganaji wa ccm kama niaje angalia uwezekano...,ccm ina wanajeshi wakutosha wa kukipigania si kama cdm inanguzo chache moja ikidondoka nacho kinapumulia machine .
 
Mkuu,

Umeingia shirika na wachawi, leo unawasema hadharani, sasa unashangaa nini kusikia ya kuwa sasa wanapanga kukutoa kafara na wewe?

Pole sana lakini hivyo ndivyo ngoma ya wanga inavyochezwa!

Tunakuombea mkuu Mungu Akulinde na kukuepusha na mabaya yote wanayoyapanga.

Siku ingine ukisikia watu tunalalamika kuhusu magamba na umafia uliokithiri kwenye serikali ya ccm nafikiri utatuelewa na kukubaliana nasi ya kuwa muda umefika wa kuwaondoa kabla hatujatolewa kafara wote kwa uchu wa watu wachache!

Mungu Ibariki Tanzania!

Hahaa Kafara imefika zamu yake anapiga kelele?
Ndio Raha ya Uchawi, kama ulikula nyama zao sasa zamu yako na wewe toa yako.

Naamini Hata Nyerere, Kolimba, Malima wangewahi kuamia Upinzani mapema wasinge uliwa.
Malima alichelewa kidogo sana na NRA.
 
Naona salia jingine linajiandaa kujipenyeza CHADEMA kwa ajili ya mpango mzima kuelekea 2015. CHADEMA kuweni makini!
 
I really feel sorry for u...trying to feel and share the situation and pains you are facing.

Lakini sasa, Mchambuzi... unamaanisha kwamba wanaokusaka kukung'oa kucha, kukutoa macho au kutaka uhai wako, kwa sababu tu umeamua kufikiria tofauti, ni WAZEE!

Aisee, so vijana wote kwenye chama chenu uko pamoja nao kwenye fikra zako kwa ajili ya chama chenu. Na unataka kutuaminisha kuwa vijana, tena wengine viongozi wakubwa tu, ndani ya chama chenu na walioko kwenye serikali ya chama chenu ni watakatifu na wazeewote ni wapika majungu, wafitini, wanafiki na every kind of such stuff.

Naona kama unakosea katika kujenga premises na hatimaye conclusion. Iangalie vyema ili tusiache jiwe bila kugeuzwa. Uhalisia unaonesha, vijana ni wabaya sana pia, maana wanakabidhiwa mikoba.

Lakini pia wamekuwa wabaya zaidi kwa sababu tu, wanaona wazee wako tayari kuondoka, wakati wao (vijana) hawajala na kujinufaisha na nafasi wanazopewa vya kutosha. So they are ready for anything...torturing, kidnapping and killing their opponents, by any means necessary. Wameshafanya hivyo na bila shaka wanaendelea kupanga hivyo.


Vijana hao hawawezi kabisa kufanya siasa za ushindani wa kuchanyata mawazo na fikra. Tumewaona. Wanajulikana, kwa matendo na maneno yao, hadharani na sirini.

By Mchambuzi

...vijana tuna haja ya kuacha kuiga siasa za wazee zilizojaa majungu,fitina na visasi,badala yake...
 
Hii sasa hatari! Naona karibu kila mwanasiasa sasa anadai maisha yake yapo hatarini.
 
Pole sana kaka Mchambuzi,hii ni kutokana na uchambuzi wako ktk hoja mbalimbali hivyo jamaa wameona umewaumbua na unavyojua hawapendi kuusikia ukweli.Kaka nakushauri utafakari upya gharama za kubaki ccm au kuondoka huko.MUNGU akutangulie kwa yote.
 
nani amekutishia maisha? Mtaje

Soon mtasikia Bujibuji na Boflo wanatafutwa na wang'oa kucha na meno bila ganzi kwa kurusha thread zisizo na kichwa wala miguu JF uploadfromtaptalk1364225143266.jpg
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom