Taarifa: Usalama Wangu Hatarini

Taarifa: Usalama Wangu Hatarini

Cc.. Nape Mnauye mwandosya, Mwigule chemba, Ritz, taswira, Lumumba team, Kinana (weka mbali na tembo), mzee wa ndimi tatu, Rejao, Majebere, kova, Ighodu, Msangi.

Mtumaini Mungu mkuu, yeye ndiye muweza wa yote usiogope kifo kwani siku moja kila mtu ataonja mauti, Usimuogope mwanadamu hasa yule anayeua mwili tu, bali Muogope na muabudu kwa nguvu zote aliyekuumba na yule awezaye kuua roho
 
Mchambuzi,huwa unapitia sana marejeo ya Baba wa Taifa Mwl.J K Nyerere,alisema bila CCM kugawanyika hakutakuwa na ushindani makini,hivyo mlioko huko CCM ambao mko wasafi ni wakati wenu wa kuvunja tawi hilo safi na kuendelea na maisha yenu.Mahali popote penye pesa chafu basi hata maisha ya binadamu huwa hayana maana.Waopoaji wa maliasili za taifa letu hawataweza kuwavumilia mnaotaka kuwa nyang'anya kitumbua chao mdomoni au kukiweka kitumbua hicho mchanga.

Na ukitaka kulijua hilo baada ya muda mfupi wa kutuma post yako hii utapokea matusi,kejeli kutoka huko unakowapigania kwamba ni wakati wamageuzi na CCM inatakiwa igeuke na kuanza kujisafisha.Kaka yangu mti wenye matunda mema hauachwi huru bali kila mtu huutupia mawe ili kupopoa matunda yake.Pole na hongera kwa kusimamia unachoamini.
 
Pole sana,
Chukua hatua za haraka za kujihakikishia usalama wako. Baada ya hapo wasiliana na wadau wengine wakusaidie kuwa salama na kuendeleza unayodhani ni azma yako kwa faida ya nchi yako. Karibu Tanzania: Mungu akulinde.

Mchambuzi pole, Mkuu wewe ndiye MARCOSSY ALBINEY (KAMA SIJAKOSEA MAWANAHARAKATI), Kama ni wewe Kunauzi ulikuja humu kuwa umehama nyumbani kwako kwa vitisho kama hivi vya mchambuzi ni kweli ama-Thibitisha kama ndiye wewe ?? Kma siye wewe niwie radhii mkuu
 
Ndugu yangu Mchambuzi ; hamia CHADEMA. Hao CCM si watu wema. Mimi nimewasoma kwa muda mrefu na nimewatumikia kwa hali na mali kwa nguvu zangu zote lakini kwa kipindi chote tangu niwe na akili mpaka sasa nimekuwa nikiwasoma kwa makini na nimegundua CCM ni chama kinacho dhibitiwa na watu wachache wenye siri kubwa na malengo ambayo ni ya kutia shaka na pengine ya kuogopesha kwa mtu wa kawaida pale anapoyagundua..

Whaat! ni wewe kweli
 
Last edited by a moderator:
Unaweza kuwa salama nje ya ssm ndo uwaseme madhambi yao. Bahati mbaya wanajiona unattachable. 2015 ni mmwamuzi wa haya yote. Mlinzi wetu mkuu ni Mungu hata hao wanaokutishia hawewezi kuishi milele. Uzuri ni kwamba auaye kwa upanga atauawa kwa upanga. Amwagaye damu nayake itamwwagwa.
 
halafu ndugu yangu Mchambuzi unatakiwa uelewe kitu kimoja.Unapokuwa unampinga mtu ambaye unalala naye kitanda kimoja, halafu kumpinga kwako kuna ukweli, halafu kunaathiri maslahi yake, na yeye yupo pale alipo kwa sababu ya maslahi hayo, anaweza usiku akategea umelala akakukaba koo.Hivyo ni bora ukahama ukawa unalala nyumba ya jirani.Haina maana kama ukilala nyumba ya jirani ndio kama ana mpango wa kukudhuru hatoweza la! bali walau itamlazimu avunje mlango kwanza.Natumai umenielewa mkuu.
 
Last edited by a moderator:
Pole sana Mchambuzi. Kwa hali ilivyo ya kuua au kufanya vilema wale walio katika upande wa mwanasiasa fulani katika chama fulani basi uwe tu makini. Cha msingi hadi 2015 uwe makini sana kwa:
1. Kutotembea peke yako wakati wote. Jitahidi uwapo katika maneo hata garini muwe zaidi ya mmoja
2. Epuka marafiki wapya: Marafiki wapya wanatumwa kwa kasi kuonesha kuwa ni marafiki wa ukweli na utawaamini na watakusoma, uwe makini.
3. Kuwa makini na marafiki wa zamani: Nao hawa binadamu kawaida huwa ni kinyonga (wengi) ni rahisi kukubadilikia. Mwisho wa siku uwe na siri zako nyeti wewe tu na rafiki si lazima kuzifahamu hata mipango yako.
4. Omba mods fanya marekebisho kidogo kwenye ID
5. Andika list ya wabaya wako weka wazi nyumbani kwako na ikiwezekana waambie kabisa.

Ninaendelea kusema kuwa tuache udikteta. Tuache demokrasia ifuate mkondo wake. Tanzania nchi ya amani sasa inatia aibu kubwa sana. How dare unamtesa mtu hadi kuua kisa ni madaraka na uchama?
 
Mpwa kila nafsi itaonja mauti but kinachouma ni pale mauti yako yanapoharakishwa na wajinga fulani wachache wanaotaka kubakia madarakani daima...
 
Pole sana Mkuu Mchambuzi.....Ila ni vizuri tukajiuliza maswali yafuatayo:
  1. Wamekutambua pamoja na kutumia hiden ID?na kama ndivyo ni kwa kiasi gani JF members wapo salama katika hili wimbi la kung`olewa kucha?
  2. Ukiona vipi waachie lichama lao karibu huku....:rockon:
 
Unaweza kuwa salama nje ya ssm ndo uwaseme madhambi yao. Bahati mbaya wanajiona unattachable. 2015 ni mmwamuzi wa haya yote. Mlinzi wetu mkuu ni Mungu hata hao wanaokutishia hawewezi kuishi milele. Uzuri ni kwamba auaye kwa upanga atauawa kwa upanga. Amwagaye damu nayake itamwwagwa.
Mlinzi wako mkuu ni mungu? Mbona unaloki mlango ukiingia kulala?
 
Whaat! ni wewe kweli

Usiogope mkuu, ni yeye huyo betlehem, amebadilika siku hzi ni chadema damu, amejiunga na CDM wiki kama mbili zimepita, alileta uzi hapa, wa kujiunga na CDM, na vijana wa KINANA pale lumumba yote wakiongozwa na Ze marcopolo, wingu,Ritz, na taswira walimsema sana , so ni kamanda huyo usimshuku mkuu
 
Uliyoandka ni mazur ya kujifunza kwa vyama vyote. Hili la kutishiwa wahi polisi toa taarifa ili kujihami na wang'oa kucha.
 
Mchambuzi,

Kwa mawazo yangu ni kuwa au uache SIASA hadi hapo Siasa za CCM zitaanza kuwa za karne ya 21 kwenye nchi ya vyama vingi au uhame chama. Vinginevyo, kuna Wabishi hapa ambao wako tayari kuuwa hata bila ya amri kutoka kwa Viongozi wake, utakuwa hatarini. Nafikiri CCM wanatumia maneno ya Presidend George W. Bush kuwa "Au upo na sisi, au unapingana na sisi" yaani hakuna kuwa Neutral.

Pole kwa yanayokukuta na nina amini kuwa kama mapenzi ya Mungu yalivyo, hakuna kitakachokukuta. Maadamu sisi wote siku moja tutakufa, basi kifo chako kitakuwa kile ulichopangiwa na Mungu na si alichopanga binadamu. Nimeshaona story nyingi za wanajeshi waliorudi kutoka vitani na siku kadhaa baadaye kuja kuuawa wakiwa kwao nyumbani.

Bado narudia tena kuwa "Au ujitoe kwenye Siasa" au "waachie chama chao." Muda ukiwa umewiva, basi utarudi kwenye Chama chako ukipendacho. Wakati wa Siasa za ubaguzi wa rangi, wengi walikimbia nje ya South Africa ila si kuwa waliacha kupigana. Nilishakutana na jamaa ambaye anasema kuwa alipokuja Tanzania, kila siku alikuwa akitaka kwenda kuiona nchi ya Ahadi ya Black South Africans wakati ule yaani Mazimbwe-Morogoro. Siku alipofika hapo, ilikuwa kama amefika Mecca na anasema alishindwa kujizuia kulia kwa kujua kuwa ni hapa alikuwa akiota miaka mingi kufika ila leo anafika kwa muda tu na kuondoka.

MUDA HUTIBU MENGI.
 
Haaa! Na wewe nilikuwa nadhani mjanja kumbe uko hili chama? Na bora "WAKUFANYIZIE" ili ujifunze kuwa unaishi na "WANYAMA"
 
Mchambuzi haufit kuwa mwana CCM. Wana CCM weng humu JF ni vila.za sana. Wewe una akili zaidi yao ndio maana wanapanga njama za kukudhuru.. Simama imara kama Deo Filikunjombe
 
Last edited by a moderator:
Ndugu yangu Mchambuzi ; hamia CHADEMA. Hao CCM si watu wema. Mimi nimewasoma kwa muda mrefu na nimewatumikia kwa hali na mali kwa nguvu zangu zote lakini kwa kipindi chote tangu niwe na akili mpaka sasa nimekuwa nikiwasoma kwa makini na nimegundua CCM ni chama kinacho dhibitiwa na watu wachache wenye siri kubwa na malengo ambayo ni ya kutia shaka na pengine ya kuogopesha kwa mtu wa kawaida pale anapoyagundua..

Am I dreaming or what? Its really you and not somebody stole your password?
 
Mchambuzi,

Watu kama ninyi huko CCM hamuwezi kuwa na tija.Mpo wachache na mmezingirwa sana na wanaojiita chama cha mapinduzi huku wakizuia mapinduzi ya fikra

Nakushauri chukua tahadhari,wengine tumeshazoea siasa za vitisho.Hata humu humu JF inbox za watu zingewekwa hadharani ungeshangaa

Hii do or die mentality katika siasa zetu zitlipeleka taifa pabaya.Tusikubali tusimame kidete ndani na nje ya vyama vyetu
 
Back
Top Bottom