Nimeamua kuungana na watetezi wa nchi hii "Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutetea rasilimali za nchi, uongozi bora, uadilifu na katika kusimamia masuala mbalimbali yanayohusu uongozi kwa ujumla.
Nimefikia hatua hiyo baada ya kuona Chama changu (CCM) ambacho kwa hakika nilikipenda kimepoteza muelekeo kwa kiwango kikubwa na baada ya kupima nimegundua hakiwezi kurejea kwenye njia tena.Nimefikia uamuzi huu baada ya kuona chama nilichokuwa kimegeuka kuwa adui wa watu badala ya kuwa rafiki wa wananchi,kuwa wanyonyaji wa wananchi badala ya kuwa watetezi wa wananchi, kuwa watu wasiowajibika, wasioshaurika, wasiojishugulisha, wasiojirekebisha, wasiosikiliza wanachoambiwa na wananchi na wanaotumia mamlaka waliyopewa kujinufaisha kwa njia za hila.
Kwa kipindi kirefu nimekuwa nikiitetea CCM kwa dhahiri na kwa siri kutokana na mapenzi niliyo kuwa nayo kwa chama hicho licha ya udhaifu uliokuwa unaonekana ndani ya chama cha CCM kwa ku amini kwamba wangejirekebisha pengine, lakini naona uziwi na upofu umekuwa ukizidi siku hadi siku hata kuamini yale waliyosema wahenga kwamba "mtu anapokaribia kufa hawezi kuona wala kusikia tena mambo ya ulimwengu huu".
Nimejipatia kadi yangu ya CHADEMA jana Tarehe 13/03/2013 na nina nia ya dhati kushirikiana na wanachadema katika harakati za kutetea ujenzi wa taifa imara, adilifu, na lenye uongozi imara na unaowajibika.Nawasihi na wenzangu wenye mapenzi mema na nchi hii wajiunge na CHADEMA ili kulinda haiba, utu, heshima na taaluma zao kuliko kuendelea kuitetea CCM Huku viongozi wake wakiendelea kuhujumu nchi kwa hila.
Mwisho nawasihi watanzania wote tuchangie harakati za CHADEMA kwa hali na mali ili tuweze kufikia ukombozi wa kweli ili akili ndogo zisiendelee kutawala akili kubwa.
Wenu katika ujenzi wa taifa,
Betlehem,
wa JF.